Uchaguzi 2020 Kagera: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia

Uchaguzi 2020 Kagera: Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Wakuu,​


Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi Mkuu 2020 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Kagera. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.

Mkoa wa Kagera una jumla ya majimbo ya uchaguzi 9 ambayo ni:-

Bukoba Mjini:
Stephen Byabato (CCM) - Kura 29,208
Adronicus Chief Kalumuna (CHADEM) - Kura 17,348

Bukoba Vijijini:
Jackson Rweikiza (CCM)

Biharamulo:
Ezra Chiwelesa (CCM)

Karagwe:
Innocent Bashungwa (CCM) - Kura 68,371

Kyerwa:
Innocent Bilakwate (CCM)

Muleba Kusini:
Oscar Kikoyo (CCM)

Nkenge:
Frolent Kyombo (CCM) - Kura 58,051
Magreth Kyai (Chadema) - Kura 4,803

Ngara:
Ndaisaba Luhoro (CCM)

Muleba Kaskazini:
Charls Mwijage (CCM)

ZINGATIA: Mikoa yote ina mada yake ya 'Update' ili kuweka wepesi katika ufuatiliaji.
 
Jimbo lenye ushindani ni Bukoba Mjini Tu, mengine CCM wanapeta kama ilivyo miaka yote.
 
Kagera tunafuta rasmi Wasaliti wa Nchi CHADEMA
 
Muleba Kusini kinaweza kunuka ndugu yake Prof Anna Tibaijuka alikatwa. Hasira za maccm zinaamia kwa wapinzani
 
Bukoba hiyo jamani Bodaboda wamebaini Gari lililokuwa na masanduku kibao ya kupigia kura wakalifukuza likakimbilia polisi, sasa polisi wameweka vizuizi hakuna mtu kuingia na wanatishia kutumia silaha.

Gari la pili limebainiwa na Bodaboda Bukoba, polisi tayari wameliweka kituoni. Gari linapasuliwa vioo na polisi wameweka vizuizi hakuna raia kuingia barabara ya Polisi.

 
Bukoba askari wamemwagwa kila kona aisee, ila wananchi bado wabishi wako mita 0 wanasubiri matokeo vituoni.
 
"Namkataa shetan na kazi zake zote na mambo yake yotee..." baada ya kauli hii matangazo yalizimwa now kuna bwege linakuja linasemaa ccm imepita...😂😂😂
 
BUKOBA MABOMU YAANZA KURINDIMA USIKU HUU
 
Back
Top Bottom