Kagera: Mbaroni kwa kosa la kukutwa na vifaa tiba vya Sh milioni 122

Kagera: Mbaroni kwa kosa la kukutwa na vifaa tiba vya Sh milioni 122

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mbaroni kwa kosa la kukutwa na vifaa tiba vya Sh milioni 122

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linamshikilia, Anicetha Johannes (24) mkazi wa Omukigusha kata ya Bilele muuzaji wa vyuma chakavu kwa kosa la kukutwa na vifaa tiba vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 122.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Awadhi Jumaa amesema leo kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na vifaa mbalimbali ikiwa ni vifaa Tiba na miundombinu ya umeme.

Amevitaji vifaa hivyo kuwa ni mikasi ya kufanyia tohara 2,298 yenye thamani ya Sh milioni 27.576, (Discting Force Pcs 1412) zenye thamani ya Sh milioni 14, Needle holder 5,000 zenye thamani ya Sh milioni 50, Straight Artery force Pcs 3,047 zenye thamani ya Sh milioni 30.47.

Pia mtuhumiwa huyo amekutwa na miundombinu ya umeme mbalimbali.
 
Back
Top Bottom