Kagera: Mbunge Ndaisaba Ashiriki Zoezi la Ugawaji wa Miche Takriban Milioni Moja ya Kahawa

Kagera: Mbunge Ndaisaba Ashiriki Zoezi la Ugawaji wa Miche Takriban Milioni Moja ya Kahawa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro alishiriki zoezi la ugawaji wa Miche ya Kahawa lililofanyika Octoba 4, 2023 katika Kijiji cha Kashinga - Nyakisasa.

Miche hii ni matokeo mazuri ya Jitihada za Mhe. Mbunge katika kulikuza zao la Kahawa ili kuongeza mapato kwa Mkulima mmoja mmoja.

Tukumbuke tangu Mhe. Ndaisaba Ruhoro alipoingia madarakani amekuwa akipambana kuhusu zao la Kahawa Ngara kutokana na ukweli kuwa, Wakulima wa Ngara walikua wakinufaika kidogo sana kutoka kwenye zao hili, Wakati Wakulima wa maeneo mengnine wakiuza Kahawa yao kuanzia TZS 2200 kwa kilo na kuendelea, Wakulima wa Ngara walianzia TZS 900 pekee kwa kila Kilo.

Mhe. Mbunge aliiomba Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza motisha kwa Wakulima wa Kahawa Ngara, ambapo Mhe. Rais aliridhia na kutenga kiasi cha TZS 300,000,000 kupitia kwa Bodi ya Kahawa, kiasi kilichotumikia kuandaa miche hiyo.

Mhe. Mbunge alishiriki zoezi la kupanda mche wa kahawa kama ishara ya kufungua rasmi zoezi la upandaji wa zao hilo kwa wakulima wote

Katika shughuli hiyo Mhe. Mbunge aliongozana na Katibu wa CCM Wilaya, Ndg. Annastazia Amos Amas na Mwakilishi kutoka Bodi ya Kahawa Kanda ya Ziwa Ndg. Edmond Zani

Sarah Kenneth
Kaimu Katibu wa Mbunge
Ngara; Octoba 10, 2023
KUTOKA MAKTABA

WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.55.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.55(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.53.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.54(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.32.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-11 at 21.23.55(2).jpeg
 
Back
Top Bottom