DOKEZO Kagera: Mkataba wa mabilioni ulisainiwa kujenga kingo za Mto Kanoni, lakini hakuna kinachoendelea

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Julai 2025 ulisainiwa Mkataba wa ujenzi wa kingo za Mto Kanoni, ulioko katika Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera na kukabidhiwa kwa mkandarasi wa kigeni, Kampuni ya Shandon Luqiao Group Company Limited, inayofahamika kama Shandong, kwa gharama ya Shilingi bilioni 21.3. Mradi huo ni sehemu ya miradi inayotekelezwa kupitia mpango wa TACTIC.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa kingo za Mto Kanoni kwa urefu wa kilometa 7.3, pamoja na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 10.75 na uwekaji wa taa 423 za barabarani ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Kwa mujibu wa mkataba, mkandarasi alipewa muda wa miezi 15 kutekeleza mradi huo, kuanzia Julai 15, 2025 hadi Oktoba 14, 2026. Hata hivyo, hadi sasa utekelezaji wa mradi huo ni kama umekwaa kisiki. Hakuna hatua kubwa inayoonekana kupigwa, wakati muda wa mkataba ukielekea ukingoni.

Badala yake kumekuwepo na kauli mbalimbali, ikiwemo za kisiasa, kuhusu mradi huo, lakini wananchi bado hatuoni uwajibikaji unaoendana na ukubwa wa tatizo. Awali, ilielezwa kuwa msimu wa mvua pamoja na taratibu za kumpata mshauri wa mradi vilisababisha mradi kushindwa kuanza katika kipindi cha takribani miezi sita ya mwanzo tangu mkataba uliposainiwa. Hata hivyo, hadi sasa hakuna hatua ya maana inayoonekana katika eneo la mradi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Jacob Nkwera, aliwahi kunukuliwa akisema kuwa ujenzi wa kingo za Mto Kanoni unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 28 Februari 2026, mara baada ya kukamilika kwa taratibu za kumpata mshauri wa mradi. Hadi sasa, takribani miezi sita imepita tangu tarehe iliyotajwa kwa utekelezaji utaanza.Msimu mwingine wa mvua ukikaribia, lakini hakuna dalili zinazoonekana za mradi kuanza.

Kinachotajwa kuwa kinaendelea katika eneo hilo ni uwepo wa siasa zinazodaiwa kukwamisha utekelezaji wa mradi. Aidha, kuna madai kwamba mkandarasi huyo hagusiki na kwamba kuna baadhi ya watu wanaomkingia kifua kwa kuwa mmoja wao ana maslahi katika eneo ambalo mradi huo unatakiwa kupita. Madai haya yanahitaji kuchunguzwa na mamlaka husika ili ukweli uwekwe wazi na hatua zichukuliwe.

Wananchi tuliamini kuwa tumepata neema ya kuondokana na tatizo la mafuriko baada ya kusikia kwamba mradi huo umesainiwa rasmi. Hata hivyo, matumaini hayo yameanza kutoweka kutokana na kutokuwepo kwa utekelezaji unaoonekana. Mkandarasi haonekani katika eneo la mradi, huku kukiwa hakuna taarifa za uhakika kuhusu hatua zinazochukuliwa kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa wakati.

Tunatoa wito kwa Serikali, kupitia Wizara ya TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu, kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo. Ikiwa kuna kikwazo kinachochelewesha utekelezaji wake, kiwekwe wazi na hatua zichukuliwe kukiondoa. Aidha, ikiwa kuna wahusika wanaokwamisha mradi huo kwa maslahi yao binafsi kama inavyotajwa, hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Wananchi wa Kata ambazo zilitarajiwa kunufaika na mradi huo sasa tumeanza kuingiwa na hofu, hasa kutokana na msimu wa mvua unaokaribia. Tunaiomba Serikali ichukue hatua za haraka ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa na wananchi wanaepushwa na madhara ya mafuriko ambayo yamekuwa yakiwakabili.

Pia soma ~ Fatma Mwassa: Ifanyike tathimini waliojenga eneo la Mto Kanoni (Bukoba). Inadaiwa wamepelekea ujenzi wa daraja kusuasua
 
Kwa sasa hakuna wa kuchukua hatua, watu (viongozi) wako kwa ajili ya mambo yao binafsi, hata matatizo na changamoto zinazowakabili wananchi wao hutumia kama fursa ya kupiga na kibaya zaidi ni kwamba kuna wakati matatizo hutengenezwa ili tu kupata mwacha wa kupiga.
 
Back
Top Bottom