Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Bukoba, Jeshi la polisi mkoani Kagera linamtafuta mtu mmoja anayeshukiwa kuhusika na mauaji ya mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 11 mwanafunzi wa darasa la nne, shule ya msingi Kahororo manispaa ya Bukoba.
Mwanafunzi huyo alibakwa, kulawitiwa na kisha kupigwa na kitu kizito bila huruma.
RPC mkoa wa Kagera amesema mwanafunzi huyo alipotea baada ya kutumwa na mama yake kwenda kununua sabuni siku ya April tano.
Baada ya kutorudi nyumbani mama wa mtoto huyo aliamua kwenda kuulizia dukani alipomtuma na aliambiwa kuwa hakufika.
Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mtoto huyo alibakwa kulawitiwa na kisha kupigwa na kitu kizito. Kamanda Malimi (Rpc Kagera) ameomba msaada kwa jamii nzima kutoa msaada mtuhumiwa akamatwe.
Kwa hisani ya Mwananchi