Hapo sasa ndipo utakapowaona watawala wetu na viongozi wengine wa chama na serikali, wakiwa wamevaa suti/nguo zao nyeusi, huku wapita mbele ya majeneza ya marehemu, na nyuso zao za huzuni!
Uwezo wetu ni mkubwa sana kuandaa matukio yenye kiki, sifa na utukufu kwa watawala.
Hapo jina la rais (hata kama hayupo) litatajwa mara nyingi sana na kumwagiwa sifa kemkem!
Hayo tunayaweza sana! Ila yale ya dharura hatuwezi kabisa!
Hakika tumeishangaza dunia. Fuatilia hizi picha:
1. Ndege ilianguka mita 100 kutoka uwanjani
2. Waliivuta kwa kamba za mikono
3. Masaa kadhaa baadae akafika PM
4. Maandalizi ya kuaga miili