Kagera Sugar mnatuzoea sana,tunaenda kuwachakaza

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Ukicheka na nyani utavuna mabua! Hawa mabwana mdogo wa Kagera Sugar wamekuwa na mazea mabaya sana na Simba SC.

Hatujasahau mwaka jana wametuaibisha mbele ya Rais sambamba na kutibua record mujarabu ya kumaliza ligi bila kufungwa.

Hatujasahau juzi kati wakatupiga mbili tukiwa kwenye kampeni ya kula viporo huko kwao Kaitaba.

Sasa kesho watataka kuleta tena mazeoea na jeshi hatari la Aussems.

Nimeongea na wachezaji wawili washkaji zangu,tumekubaliana kukataa mazoea ya kijinga. TUTAWACHAKAZA hapo kesho.

Kuna overdose tumetoea Jana kwa Coastal Union,hizo ni salamu japo tumetoea dozi kali ya Ebola kwa mtu mwenye UTI tu.

Mjiandae kisaikolojia,msije kusema hamkuambiwa. Malalamiko FC kaeni mkao wa kula kuonyesha jinsi tunavyobebwa na marefa.

Kwa kheri
 
Nani kakwambia nafatilia mechi za mabonanza?endeleeni nayo nafatilia ligi zinazojitambua sio mabonanza ya viporo
 
Nani kakwambia nafatilia mechi za mabonanza?endeleeni nayo nafatilia ligi zinazojitambua sio mabonanza ya viporo
Kila nchi yenye timu CAF tournaments basi ligi yake ilikua na viporo. Sababu ni kua CAF walibadili ratiba mashindano yaishe miezi hii sawa na mashindano ya mabara mengine kama Ulaya badala ya kuisha mwishoni mwa mwaka kama ilivyokua miaka iliyopita.

Matokeo yake ni michezo ya CAF kufanyika karibu karibu hali iliyopelekea timu hizo kukosa muda wa kucheza ligi ya nyumbani. Fanya research kwenye ligi za nchi kama Misri, SA, Tunisia, etc utaona hili.

Na pengine kwa sasa sababu timu nyingi hazipo tena CAF ndio viporo vimepungua, lakini kipindi kile cha makundi ungeangalia league tables zao ungegundua hili
 
Unachosema ni kweli,lakini hakuna nchi viporo vilizidi vinne, huku kwetu vilifika 10 hapo ndiyo radha ya ligi ilipopotea.
 
manunuzi FC itafanya yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…