Katulanda:
KUMBUKUMBU YA SIMBA KUKATWA (KUPOKWA) POINTI
Mwaka 2006 Simba SC ilimchezesha Musa Hassan Mgosi kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera na kushinda mchezo huo, lakini walikatwa point 3 kwa kumchezesha Mgosi wakati akiwa na kadi 3 za njano na hatimaye Simba kukosa ubingwa ambao ulikwenda kwa mahasimu wao, Yanga.
Mwaka 2004, Simba SC kwa mara nyingine walikuwa wahanga wa kukatwa pointi. Safari hii walikatwa pointi 6. Hii ilikuwa baada ya timu ya Mji Mpwapwa ya Dodoma kushindwa kuendelea na ligi kutokana na ukata na hivyo kulazimu TFF kuzikata timu zote pointi zilizokuwa zimecheza na Mji Mpwapwa. Ikumbukwe Simba alikuwa anakaribia ubingwa na hatimaye Yanga kuubeba ubingwa huo kwa kuwa wao walikatwa point 3 tu sababu walicheza mchezo mmoja na Mji Mpwapwa.
Mwaka 2007/2008, Simba SC hii hii walikuwa wahanga wa kukatwa pointi kwa mara nyingine tena mara baada ya kumchezesha mchezaji Juma Nyoso kwenye mchezo dhidi ya Costal Union ya Tanga. Ikumbukwe hapo kabla mchezaji huyo alipewa kadi nyekundu akiwa ana timu ya Ashanti iliyoshuka daraja.
Sasa Simba SC walivyomsajili Nyoso hawakuwa na kumbukumbu za kuwa alikuwa na kadi nyekundu akiwa Ashanti United, hivyo kumchezesha mchezo dhidi ya Coastal Union kinyume cha kanuni za ligi. Simba SC walikatwa point 3 zote baada ya Coastal Union kukata rufaa.
Kumbukumbu hizi zinatolewa kutokana na kuwapo baadhi ya wana soka ambao wameanza kusema Simba anabebwa baada ya jana kumkatia rufaa mchezaji Mohamed Fakhi wa Kagera Sugar.
Sasa swali la kujiuliza wakati Simba SC anakuwa muhanga wa hayo matukio, walikuwa wapi wanaobeza leo mpaka wasiwe na kumbukumbu?
Fakhi ana kadi tatu za njano zote za ligi kuu.
1. Mbeya City 0-0 Kagera Sugar. Disemba 17, 2016
2. Kagera Sugar 2-1 African Lyon. Januari 18, 2017
3. Kagera Sugar 1-0 Majimaji. Machi 4, 2017.
Hao wanaosema kadi moja ilikuwa FA Cup ni Kagera Sugar wenyewe kwa sababu mechi ya African Lyon walisahau kama Fakhi alioneshwa kadi???...