Kagera Sugar wapokonywa pointi 3 na kupewa Simba

Katulanda:
KUMBUKUMBU YA SIMBA KUKATWA (KUPOKWA) POINTI

Mwaka 2006 Simba SC ilimchezesha Musa Hassan Mgosi kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera na kushinda mchezo huo, lakini walikatwa point 3 kwa kumchezesha Mgosi wakati akiwa na kadi 3 za njano na hatimaye Simba kukosa ubingwa ambao ulikwenda kwa mahasimu wao, Yanga.

Mwaka 2004, Simba SC kwa mara nyingine walikuwa wahanga wa kukatwa pointi. Safari hii walikatwa pointi 6. Hii ilikuwa baada ya timu ya Mji Mpwapwa ya Dodoma kushindwa kuendelea na ligi kutokana na ukata na hivyo kulazimu TFF kuzikata timu zote pointi zilizokuwa zimecheza na Mji Mpwapwa. Ikumbukwe Simba alikuwa anakaribia ubingwa na hatimaye Yanga kuubeba ubingwa huo kwa kuwa wao walikatwa point 3 tu sababu walicheza mchezo mmoja na Mji Mpwapwa.

Mwaka 2007/2008, Simba SC hii hii walikuwa wahanga wa kukatwa pointi kwa mara nyingine tena mara baada ya kumchezesha mchezaji Juma Nyoso kwenye mchezo dhidi ya Costal Union ya Tanga. Ikumbukwe hapo kabla mchezaji huyo alipewa kadi nyekundu akiwa ana timu ya Ashanti iliyoshuka daraja.

Sasa Simba SC walivyomsajili Nyoso hawakuwa na kumbukumbu za kuwa alikuwa na kadi nyekundu akiwa Ashanti United, hivyo kumchezesha mchezo dhidi ya Coastal Union kinyume cha kanuni za ligi. Simba SC walikatwa point 3 zote baada ya Coastal Union kukata rufaa.

Kumbukumbu hizi zinatolewa kutokana na kuwapo baadhi ya wana soka ambao wameanza kusema Simba anabebwa baada ya jana kumkatia rufaa mchezaji Mohamed Fakhi wa Kagera Sugar.

Sasa swali la kujiuliza wakati Simba SC anakuwa muhanga wa hayo matukio, walikuwa wapi wanaobeza leo mpaka wasiwe na kumbukumbu?

Fakhi ana kadi tatu za njano zote za ligi kuu.

1. Mbeya City 0-0 Kagera Sugar. Disemba 17, 2016

2. Kagera Sugar 2-1 African Lyon. Januari 18, 2017

3. Kagera Sugar 1-0 Majimaji. Machi 4, 2017.

Hao wanaosema kadi moja ilikuwa FA Cup ni Kagera Sugar wenyewe kwa sababu mechi ya African Lyon walisahau kama Fakhi alioneshwa kadi???...
 
bora na simba washinde ligi mwaka huu ili yanga tujtathimin, timu haiwez kumtegemea mtu mmoja tu. Halafu kuhusu hili la point 3za kagera naona zpo kihalali, jamani mechi yenye harufu ya rushwa ni mechi ya simba na mbao. Hasa yule golkipa
 

Honereni kwa kuchukua Ubingwa wa mezani..

Yanga SC ni klabu kubwa, hata kama tungekuwa na ukame wa kutokubeba ndoo wa miaka mia nane,,,Tusingeupigania ule wa mezani
 
Honereni kwa kuchukua Ubingwa wa mezani..

Yanga SC ni klabu kubwa, hata kama tungekuwa na ukame wa kutokubeba ndoo wa miaka mia nane,,,Tusingeupigania ule wa mezani
Yanga nayo itapewa point tatu basi za afrika lyon, hapo je?
 
Hizi ni habari mbaya kwa vyura wa jangwani......

Hakika wanapitia kipindi kigumu sana...,,

Pamoja na kutumia gharama kubwa kununua mechi lakini bado ubingwa wanaukosa hivi hivi.....

Inauma sana.....
Ivi simba hamuoni aibu kupewa point tatu bila kuzitolea jasho, siku mkichukua ubingwa utashangilia kweli ndio maana mpira wa bongo hauendelei tukitoka nje ya nchi tupigwa vilivyo kwa ajili ya utumbo huu, kwel ligi ya bongo kichefu chegu Acha niendelee kushabikia ulaya tuu, bongo hatuna ligi zaidi ya majungu tuu
 
Ukitinga mahakamani tunaishisha timu yako daraja ndio sheria zinasema
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] tff waishushe yanga wakose mapato [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] ondoa hizo Akili mgando aisee
 
Hivi mbona wewe kilaza kwani match haikuchezwa??? Au simba walienda uwanjani wakasimama mpk mpira ukaisha tena simba walikimbizwa mno hadi jasho jembamba, mpka zikaingia 2. Kumbe jamaa wameweka mamluki hahaha[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15]
 

Huko ulaya unakoshabikia.....Juventus alishawahi kupewa ubingwa wa mezani baada ya Inter Milan na AC milan kukiuka taratibu za ligi....!!!??

Kwa hiyo ili soka likue ni lazima taratibu zivunjwe....!!??

Mbona unashangilia Serengeti boys....ambao wamepata nafasi hiyo baada ya kamati kukaa na kutengua ushindi wa DRC.......kwa hiyo DRC walitakiwa kuendelea hata kama walikiuka taratibu za mchezo husika.....!??

Mbona Yanga walikata rufaa dhidi ya African lyon baada ya kuhisi kuwa kuna taratibu zilikiukwa....!??

Hauwezi kuwa sawa labda kama wewe sio mwanamichezo bali ni mshabiki wa michezo.....
 
Ww unaetoka nje kitu gan kkbwa umefanya kzid simba sc zaid tu ya kshriki na kua msindikzaji kla mwka huon ww chura sc ndo unaharbu mpra kwa kuhonga na kupulizia dawa wachezaji wa timu pinzan ili ushinde ww bwna mwaka huu mateja sc
 
Nilikuwa naomba magoli mawili aliyopewa simba apewe kichuya!!!
 
Ukiona figisu figisu za kutafuta point mezani ujue tayari maji ya shingo tayari.
 
Ngomai inapelekwa Mahakamani.Simba will be yo-yoing until the end of this crazy VPL.
 
Kinacho leta ukakasi ni kuchezewa kwa kanuni ili kuibeba simba, mwaka 2015 Ajibu wa simba alicheza akiwa na kadi 3 za njano, kamati yenu ikautangazia umma wa wadanganyika kwamba kanuni zimebadilika, mchezaji anaweza kuchagua mechi za kutumikia adhabu, kwanini kanuni hiyo haijatumika kwa Fakhi? Hapo ndipo wapenzi wa soka tunapoona kwamba ni mazingira ya mbeleko
 
Hivi mbona wewe kilaza kwani match haikuchezwa??? Au simba walienda uwanjani wakasimama mpk mpira ukaisha tena simba walikimbizwa mno hadi jasho jembamba, mpka zikaingia 2. Kumbe jamaa wameweka mamluki hahaha[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15]
We utakuwa bashite sasa walishinda
 
Ww unaetoka nje kitu gan kkbwa umefanya kzid simba sc zaid tu ya kshriki na kua msindikzaji kla mwka huon ww chura sc ndo unaharbu mpra kwa kuhonga na kupulizia dawa wachezaji wa timu pinzan ili ushinde ww bwna mwaka huu mateja sc
Me siongelei upuuzi wako angalia tz ni yangapi kisoka kwa upuuzi huu wa simba na yanga tutasubir sana
 
Acha ushabiki maandazi wewe! Kwani sheria si zinaeleweka wazi kwamba ukiwa na straight yellow tatu kinachofuata na ukacheza mchezo unaofuata lazima timu itakatwa points! Hiyo ni sheria sio mimi! Sasa hapo siasa ipo sehemu gani?
But kanuni za mpira ulimweguni zinasema kwenye pre-match meeting kwa TZ TFF walipashwa kuwakumbusha kagera sugar kuhusu hizo kadi na matokea yake kama wakimchezesha huyo mchezaji lakini kwa hili hakukuwa na tahadhari yoyote kutoka either TFF au chama cha mpira mkoani!!! Ni ouenevu ulio pitiliza kwa sababu vyama vyote vya mpira hawakutimiza wajibu wao kinyume cha kanuni tena ndio hao hao walioamuwa kudhulumu! Mpira nchi hii tutasubiri sana kwani vyombo vya haki na vyenyewe havija fanya wajibu wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…