Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Watuhumiwa tisa wa mauaji ya mtoto Asimwe Novart aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (ualbino) aliyeripotiwa kuibiwa nyumbani kwao Mei 30, 2024 na mwili wake kupatikana June 17, 2024 ukiwa umeondolewa baadhi ya viungo vyake, leo June 28, 2024 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba na kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia.
Mkuu wa mashtaka Mkoa wa Kagera Waziri Mangumbo akisaidiana na wakili wa Serikali, Erick Mabagala wamewasomea mashtaka watuhumiwa hao tisa kuwa wanakabiliwa na shitaka la kuua kwa kukusudia , huku akisema kuwa uchunguzi wa shauri hilo no 17740 la mwaka 2024 tayari umekamilika.
Shitaka hilo limesomwa mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba, Elipokea Yona Wilson ambaye amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hivyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote, ambapo watuhumiwa wote wamerudishwa rumande mpaka July 12,2024 ambapo kesi yao itatajwa tena.
Watuhumiwa hao ni, Elpidius Alfred Rwegoshora miaka 49 ambaye ni padri,Novat Venant miaka 24 ambaye ni baba wa mtoto, Nurdin Ahmada, Ramadhan Selestine,Rwenyagira Alphonce,Dastan Buchard, Faswiu Athuman,Gozibert Arikad na Dezdery Everigist.
Mwili wa mtoto Asimwe Novath ulikutwa ukiwa umetupwa kwenye karavati na kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili katika kijiji cha Marere Kata ya Ruhanga wilaya ya Muleba.
Soma:
- Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji
www.jamiiforums.com

Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi limewakamata watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novath (2). Mei 30, 2024 Asimwe anadaiwa alichukuliwa na watu wasiojulikana nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera na juhudi za...