Kwanini wasipelekwe moja kwa moja kwenye mahakama ambayo ina uwezo wa kusikiliza kesi husika,mara baada ya taratibu kukamilika,kuliko kuwapeleka mahakama ambayo haina uwezo,kupoteza muda tu?
Hivi hata huko Ulaya kuna mambo kama haya,ambako tunaiga?
Labda nikupe maelezo mafupi kuhusu uendeshaji wa mashauri ya jinai hususani kesi za mauaji kwa mujibu wa sheria zetu.
Ipo hivi mtuhumiwa wa kesi ya mauaji mara tu atakapokamatwa kwa kutuhumiwa kutenda kosa la mauaji, kwanza ni kesi ambayo haina dhamana maana yake mtuhumiwa atasota mahabusu hadi kesi isikilizwe.
Mahakama yenye mamlaka kusikiliza kesi ya mauaji ni Mahakama kuu, mtuhumiwa wa kesi ya mauaji akishakatwa anatakiwa kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi au mahakama ya wilaya kwa ajili ya kusomewa shtaka lakini hatakiwi kujibu chochote kwa wakati huo.
Lengo la kumpekeleka mahakama ya chini isiyo na mamlaka ni kumpa taarifa nini kitamkabili mtuhumiwa mbele yake, kama upelelezi hadi hatua hii utakuwa umekamilika polisi wataandaa jarada la kesi pamoja na ushahidi na kuupeleka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka nchini.
Mkurugenzi wa mashtaka atapitia ushahidi ulioptikana dhidi ya mtuhumiwa, akisha jiridhisha ushahidi uliopo unatosha kuendesha shauri hilo la mauaji, Mkurugenzi wa mashtaka ataandaa hati ya mashtaka (information) na kuipeleka mahakama kuu kwa msajili wa mahakama kuu.
Mara tu msajili wa mahakama kuu atakapo pokea hati ya mashtaka kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka nchini, sheria inamtaka kurudisha jarada la kesi toka mahakama kuu na kupeleka mahakama ya chini ambako mtuhumiwa alisomewa shitaka kwa mara ya kwanza na alitakiwa asijibu chochote.
Wakati huu kesi inaporudi mahakama ya chini inaenda kufanyiwa mchakato unaitwa (Committal Proceedings) kwa bahati mbaya kiswahili chake sifahamu, ila nitaelezea lengo la committal proceedings na inafanyikaje.
Kwenye committal proceedings sheria inataka mtuhumiwa kusomewa tena shitaka lake, na wakati huu pia hakimu anatakiwa kumwambia mtuhumiwa hatakiwi kujibu chochote kwani kesi yake itasikilizwa mahakama kuu.
Baada ya shikata kusomwa tena na mtuhumiwa kukaa kimya bila kujibu chochote, hatua inayofuata upande wa Jamhuri ambao unashitaki utatakiwa kutoa idadi ya mashahidi wake itakao waita mahakama kuu kwenye usikilizaji wa kesi, pia maelezo mafupi ambayo kuhusu ushahidi utakaotolewa na hao mashahidi wa jamhuri.
Lakini pia jamhuri itatakiwa kutoa idadi ya vielelezo watakavyo wasilisha kwenye usikilizaji wa kesi huko mahakama kuu. Baada ya hapo upande wa jamhuri watakuwa wamemaliza kazi yao, sheria inataka mtuhimiwa na yeye kupewa nafasi ya kusema ataleta mashahidi wangapi pamoja na vielezo vya kutoa kama anavyo.
Hadi kufikia hapo Committal inakuwa imekamilika, hakimu atamtaarifu mtuhumiwa kwamba mchakato wa maandalizi kwa ajili ya kumpeleka mahakama kuu umekamilika hivyo atatoa amri rasmi ya kwamba anapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya kesi yake kuanza kusikilizwa rasmi.
Kwanini huu mchakato wa committal huwa unafanyika japo umekuwa ukilalamikiwa kuchelewesha usikilizwaji wa kesi ya msingi, ni kwamba sababu ya kufaya committal ni kumuandaa mtuhumiwa ili ajipange ajue nini kitaenda kujili mahakama kuu na aandae utetezi wake ulioshiba( principle of fair hearing)
Lakini kingine majaji wamekuwa wakisema committal inafanyika huku chini ili kuchambua vitu vya msingi vya kwenda kuwasilisha mahakama kuu sio kila facts hasa zile zisizokuwa na msingi zifike kule juu.
Tafiti mbali mbali zimeshafanyika kupinga utaratibu wa committal proceedings lakini bado huo utaratibu upo kwenye sheria zetu.