Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

Nadhani hili la CRDB kuhushishwa na ufisadi inabidi kulimulika kwa umakini zaidi. Kuna thread niliwahi kuisoma kule kwenye celebrities forum iliyokuwa inamhusu Kimei wa CRDB. Kuna claims kwamba alikuwa anapata 10% kwenye hizi deals za EPA na deals nyingine chafu chafu kama Richmond etc. I think its time haya masuala kumulikwa kisiasa zaidi na kuona kama kuna links chafu chafu zozote kati ya CRDB na ufisadi. Kufungua accounts sita kwenye different branches na zote zikawa na sequence ya number za kufuatana its not a coincidence. I smell a rat!
 
Wananchi wengi ni wenye hisa katika benki ya CRDB, kwahiyo wanahaki ya kumuuliza Kimei wanapokuwa na AGM yao ilikuwaje wakafungua accunts za namna hiyo za Kagoda? Ikumbukwe kuwa fedha walizoiba hawa Kagoda ni za wananchi pamoja nahao wanahisa wa CRDB; kwahiyo benki yao wenyewe ilitumika kuwaibia mali yao wenyewe lazima wapate maelezo ya kina toka kwa menejimenti.
 
Kama ni kweli hizo pesa CCM walipanga kuiba kwa ajili ya uchaguzi, kweli wangechukua siku tatu kabla ya uchaguzi wenyewe? Siku tatu zingesaidia nini? Walizigawa lini kwenye majimbo husika?

Labda waliiba ili kulipa madeni. Vinginevyo timeline ni kama hai make sense.

Hivi uchaguzi uliahirishwa tarehe ngapi? Kama walichota baada ya uchaguzi kuahirishwa, hapo ina make sense.

Huenda wajanja wachache walitumia vurugu za kwenye uchaguzi ili kutuibia.
Hii ilikuwa dili ya wizi, iliandaliwa ikawa inasuburi muda wa kuipitisha bila watu kushtuka; hebu fikiria siku 3 kabla ya uchaguzi na viongozi wengi serikalini wakati ule hawakuwa na uhakika wa kushinda majimbo yao!

Ukifuatilia wahusika wote wa EPA utagundua karibu wote wana rekodi ya utapeli; walichofanya baada ya kupata pesa ni kununua heshima kwa kufadhili shughuli za kisiasa zainazohusisha chama tawala.
 
Mimi ninashangaa sana. Yaani, mnataka kuniambia mlikuwa hamjui CCM baada ya Nyerere kilikuwa kinaishi kama mtoto yoyote wa mjini.

Unawapa tenda jamaa, kisha mfadhili anakupa fedha ya chakula kutokana na tishio la njaa. Jamaa hao wanaagiza vyakula vibovu. Bora nini kufa njaa, au kula chakula kibovu? Jibu mwenyewe!

Kisha nunua rada mbovu, Nolan kafa (RIH) 'rest in hell' and other shall follow! Nunua dege la rais, nunua mitambo mibovu ya updown or downdown sawa! Uwizi mtuuuuuupu!

Tatizo ni kuwa makuwadi wa chama hicho na wanaowatumia kufanya biashara hii chafu wanawazidi ujanja. Sishangai kwamba kati ya bilioni 50 zilizoibwa kabla ya uchaguzi wa 2005 kama CCM imepata sana basi ni tubilioni tuwili au nne hivi basi! Zingine zimeishia kwenye mifuko ya watu wanaoishi kifahari kuliko Mfalme na Malkia wa Uingereza, Norway, Sweedn, Denmkark na kadhalika ambao ni matajiri mara elfu kuliko Tanzania!

Tukipiga kelele katiba ibadilishwe ndio maana ya masuala kama haya. Kwamba Watanzania wanaibiwa nje na ndani kwa kutumia KATIBA YA NCHI ILIYOPITWA NA WAKATI. Katiba inayotoa mwanya sio tu kwa chama tawala kuwa mwizi bali kufanya chochote kile itakacho ikiwa ni pamoja na kuvizuia vyama vingine visitowe mchango vinavyoweza katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania walio wengi!
 
Kemei apelekwe Mahakamani kuhusu kuruhusu CRDB kutumika kupitishia pesa za EPA na kulisabibishia taifa hasara. Pili alitoa LC kwa Richmond wakati benki nyingine zilikataa.
 
Je ikithibitika uchaguzi wa 2005 umetumia fedha za EPA Viongozi waliopo madarakani watakuwa halali kweli?Wanasheria mtusaidie kwa hili,taamaa ya mali inadidimiza Nchi yetu.
 
Kama ni kweli hizo pesa CCM walipanga kuiba kwa ajili ya uchaguzi, kweli wangechukua siku tatu kabla ya uchaguzi wenyewe? Siku tatu zingesaidia nini? Walizigawa lini kwenye majimbo husika?

Labda waliiba ili kulipa madeni. Vinginevyo timeline ni kama hai make sense.

Hivi uchaguzi uliahirishwa tarehe ngapi? Kama walichota baada ya uchaguzi kuahirishwa, hapo ina make sense.

Huenda wajanja wachache walitumia vurugu za kwenye uchaguzi ili kutuibia.

Mkuu Mtanzania hoja yako ina nguvu lakini ukisoma post yangu hapo juu kuhusu kifo cha Jumbe utabaini nini maana ya KAgoda. Kwanza kuna wakati Zitto aliuliza CCM walijuaje kwamba Mgombea Mwenza wa Mbowe atakufa hadi wajipange kwa uchaguzi wa marudio? Ukifuatilia kwa makini utabaini kuna maswali mengi kuliko majibu na ndio maana kuna mahali nimesema Kagoda ni suala nyeti nyuma ya pazia lina mambo mengi mazito na ndio maana mama Meghji alitoswa kwa kumshauri JK awashughulikie Kagoda kwa kuwa haikuwa na chembe ya Usalama wa Taifa wakati wenzake wanataka tuamini ni ya Usalama wa Taifa.
 
Unajua hapa CRDB benki wanakesi mbili hadi hivi sasa 1.kutoa LC kwaajili ya kuchota fedha za mradi mbovu wa Richmond,2.kufungua akaunti za kupitishia fedha haramu;kwa kifupi ni benki ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kulitia Taifa hasara.
Hivi kweli akaunti zote under one roof zinaingiza fedha kiasi hicho halafu wanakaa kimya bila hata kuchukua tahadhari za kuhoji fedha hii inatoka wapi?Kagoda kama kampuni wanafanya biashara gani na je mapato hayo ni sahihi kulingana na nature ya shughuli zinazofanya na Kagoda?!
Hii hatua sidhani hata kama inahitaji mtu kwenda kusomea na kuja kuanza kufanya upekuzi wa kuhusu uhalali wa mapato haya ya Kagoda yanavyoingia na kutoka!
Ombi langu naomba DPP awafungulie mashtaka CRDB benki kwa kushiriki katika wizi wa fedha za BOT-EPA.
 
Kagoda njia nyeupe

• DPP, waziri wanawa rasmi mikono

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

NDOTO za Watanzania kuona Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd iliyochota kiasi cha sh bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinaendelea kufifia baada ya kubainika kuwa serikali haina ushahidi wa kutosha kuiburuza mahakamani.

Kukosekana kwa ushahidi huo kunaelezwa ni mipango madhubuti iliyoandaliwa na baadhi ya viongozi waliopo na waliondoka serikalini kwa kushirikiana na wafanyabiashara maarufu kupoteza nyaraka zote ambazo zingesaidia kampuni hiyo kufikishwa mahakamani kama walivyofikishwa baadhi ya watuhumiwa wengine waliochota fedha kwenye akaunti hiyo.

Pamoja na Rais Jakaya Kikwete, kukabidhi mafaili ya watuhumiwa wote wa wizi wa EPA kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi, miezi miwili iliyopita, ofisi yake imeshindwa kupata ushahidi wa kutosha kuishtaki Kagoda kama iliyotarajiwa na wengi.

Kampuni hiyo ambayo umiliki wake unahusishwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) inadaiwa walichota fedha hizo kwa ajili ya kusaidia kampeni ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 ambao CCM iliibuka na ushindi wa kishindo.

Chanzo cha habari kutoka ofisi ya DPP, kiliiambia Tanzania Daima Jumapili, kuwa wamiliki wa Kagoda walijua nini kitatokea baada ya wizi huo, hivyo kwa kushirikiana na viongozi walifanya kila njia kuhakikisha hawaachi nyaraka zozote ambazo zingekuja kuwaleta matatizo siku za usoni.

Miongoni mwa mbinu zilizotajwa kutumiwa na wahusika hao ni kwenda benki na kunyofoa nyaraka zote zilizokuwa zikionyesha mtu na akaunti ambayo fedha hizo ziliingia, nyaraka za umiliki wa kampuni katika Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (Brella) nazo mpaka sasa hazijulikani zilipo.

Chanzo hicho kimeongeza baada ya kelele za ufisadi kuzidi hapa nchini na Kampuni ya Kagoda kuandamwa, wamiliki halisi walianza kujawa na hofu ya kutajwa hivyo wakaamua kuwaendea baadhi ya viongozi na kutoa tishio kuwa kama hawatalindwa katika kashfa hiyo basi watakuwa radhi kuueleza umma walivyoshirikishwa katika wizi huo.

Kutokana na tishio hilo, baadhi ya viongozi waliopo serikalini na wale waliomaliza muda wao waliwahakikishia wamiliki hao kuwa kamwe hawataguswa kwa kuwa kampuni hiyo imebeba siri nzito ambayo ikiwekwa hadharani taifa litatikisika.

"Wamiliki wa Kagoda wanajulikana lakini serikali haiwezi kuwakamata kwa kuwa hakuna ushahidi lakini pia wana siri nzito, ndiyo maana wizi wa nyaraka ulifanyika kwa kiwango cha juu," kilidokeza chanzo chetu.

Sakata la Kagoda linaonekana kukosa mwelekeo uliotarajiwa na Watanzania baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe juzi kuweka bayana kuwa hawawezi kuishitaki kampuni hiyo kwa kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kufanya hivyo.

Chikawe alikaririwa na vyombo vya habari kuwa serikali kamwe haiwezi kumuonea mtu kwa kumpeleka mahakamani bila ya kuwa na ushahidi wa kutosha ndiyo maana Kampuni ya Kagoda haijaguswa.

"Serikali hatuwezi kufanya kazi kwa shinikizo la kisiasa, tunampeleka mtu au kampuni mahakamani kwa mujibu wa taaluma ya sheria na pia sisi si wapelelezi" alikaririwa Chikawe.

Wakati serikali ikibaninisha msimamo huo wa kutokuwa na ushahidi wa kuishtaki kampuni ya Kagoda, baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamesema uamuzi huo una lengo la kulinda ufisadi uliofanywa na viongozi waliopo madarakani na waliomaliza uongozi, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya taifa.

Miongoni mwa viongozi hao ni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), alisema vielelezo alivyonavyo vinaonyesha jinsi CCM ilivyochota fedha hizo na kuzitumia katika kampeni za uchaguzi wa 2005, ndiyo maana serikali imepata kigugumizi kuifikisha mahakamani Kampuni ya Kagoda.

Kampuni ya Kagoda Agriculture, inayotuhumiwa kuchota sh bilioni 40 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Benki Kuu ya Tanzania, wizi huo ulimfanya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, marehemu Daudi Balali.

Kutengua uteuzi huo kulikuja baada ya ukaguzi uliofanywa na Kampuni ya Ernst&Young na kubaini wizi wa sh bilioni 133 katika akaunti hiyo.

Hadi sasa jumla ya watuhumiwa 20 tayari wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu tuhuma za wizi huo huku kati yao 19 wakipata dhamana na mmoja kuendelea kusota rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti.
 
Kama DPP na waziri Chikawe hawawezi kuwashitaki wahusika wa Kagoda kisa hawana ushahidi. Je mtu/watu binafsi si wanaruhuiswa kufungua mashtaka? Kama ndivyo basi nashauri ili kuonesha ujasiri na kujiamini kwa wale walio na ushahidi wa kutosha wafungue hizo kesi wao binafsi. Ninaamini kama kweli na ikagundulika kwamba hao jamaa waliiba na wakanyweshwa mvua kwenda Segerea, heshima ya aliye/watakaofungua hiyo kesi itakuwa kubwa sana. Na kama ni chama basi kuna uwezekano mkubwa wa chama hicho kushika hatamu za uongozi wa nchi hii kuliko hawa wajulikanao kama mafisadi!
 
Mkuu mtu binasi anaweza kufungua mashtaka dhidi ya serikali, chama au shirika ili mradi unaushahidi wa kutosha, hivyo unaonaje wewe mwenyewe binafsi uchukue jukumu hilo la kushtaki badala ya kusubiri mtu ajitokeze
 
Duh, maskini sisi watanzania- bao waziwazi!
Kama haiwezekani, angalau wawafunge walioshiriki kupoteza nyaraka brela na benki, kwa kutumia vibaya ofisi zao au kitu kama hicho.
 
Duh, maskini sisi watanzania- bao waziwazi!
Kama haiwezekani, angalau wawafunge walioshiriki kupoteza nyaraka brela na benki, kwa kutumia vibaya ofisi zao au kitu kama hicho.

Outlier, sidhani kama atafungwa mtu maana watuhumiwa wote wana siri nzito dhidi ya watawala wetu wa juu nasikia hata wale wa EPA na mawaziri waliofikishwa kizimbani hivi karbuni wameanza kuziweka dhidi hizo vizuri ili walale mbele na watawala.

Labda ndiyo maana Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi wakatwambia Watanzania mafisadi ni 'matajiri' wakubwa wakifikishwa mahakamani basi 'nchi itawaka moto' na kushindwa 'kutawalika'

Kila ofisi nyeti Tanzania imeshikwa na mafisadi hivyo wanapoamua documents muhimu katika ushahidi dhidi yao zipotee, basi zinapotea bila matatizo yoyote. Mungi inusuru Tanzania toka mikononi mwa mafisadi.
 
Ndiyo maana Mwanyika, Hosea na Mwema wakapewa muda wote huo kufanya upelelezi - upelelezi ? I bet walitumia muda huo kufuta nyayo za wezi. Wezi wanafahamika ila walikopitia.
 
Last edited:
Mafisadi wajue maisha ya DUNIA ni maisha ya kupita...kwanza watenge muda kujiuliza kwanini watu wanakufa....?

Wajiulize wapo wapi watawala waliokuwa na Nguvu, Mali na sasa hawapo tena?
Yupo wapi..Nyerere, Yupo wapi kwame Nkrumah, Yupo wapi Mobutu?, Yupo wapi Gamal AbdulNasir? Yupo wapi Catro(Yu Hoi kitandani...)..Yupo wapi Sharooun( kufa hafi na mateso ya DUNIA anayapata...)..Yupo wapi Hitler?...nimetaja mifano mbalimbali kuonesha kuwa Uongozi una mwisho...na MJUE DHULMA HAIDUMU...!!!

Watanzania ambao leo hii mnawaibia ipo siku watasema basi kudhulumiwa!!!
 
Mkuu nipo pamoja nawe kuwa kwa hawa mola ndiye muhukumu lakini hii isitufanye kukata tamaa katika kuwaandama MAFISADI kwani wao hawamjui mungu katika kufanya dhuluma.
 
Serikali isipokuwa makini hata hao ambao wamefunguliwa kesi, watatumia fedha zao kushida kesi halafu watafungua wao kesi za madai dhidi ya Serikali kwa kudhalilishwa na wataondoka na kitita chengine ambacho kitakuwa cha 'halali'.
 
- Dawa ni kuwaomba wabunge wasimame kidete ili apewe Mwakyembe hii kitu, si hawa hawa serikali na Hosea walituambia kuwa hakuna usahidi kwenye Richimonduli, I mean hili la Kagoda halijaisha bado ila wana-delay to kama kawaida yao, na they know that!.
 
Back
Top Bottom