Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

ZITTO azidi kuwaka, asisitiza Kagoda mali ya CCM

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, bado anasisitiza kuwa Kampuni ya Kagoda ni mali ya chama tawala CCM.
* Adai fedha ilizochotwa EPA zilitumika uchaguzi mkuu 2005

Na Kizitto Noya

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kukataa uhusiano wake na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited iliyochota zaidi ya Sh40 bilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

Zitto aliyekuwa anajibu mapigo ya CCM iliyomshutumu juzi kwa kuipaka matope kwa kuihusisha na Kagoda, alisisitiza kuwa CCM haiwezi kujivua gamba la Kagoda kwa kuwa ndiyo inayomiliki kampuni hiyo, ikiwa miongoni mwa kampuni 22 zilizochota jumla ya Sh133 bilioni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

"CCM ndiyo inayomiliki Kagoda na Kagoda ni ya CCM. Fedha za Kagoda ndizo zilizotumika kwenye kampeni za CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Huu ndio ukweli," alilisitiza Zitto.

Kwa mujibu wa Kabwe, endapo CCM inataka kutakata inatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu zake za mwaka 2004/2005 na ieleze wapi ilipata fedha za uchaguzi mkuu mwaka 2005 uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani.

....
........

Chiligati aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa chama hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na kampuni hiyo na kwamba hata kama kuna mwanachama anayehusika, ni suala lake binafsi na sio kwa mwavuli wa chama.

Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiihusisha CCM na Kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni kwenye akaunti hiyo na miongoni mwa watuhumiwa wa EPA waliokwishafikishwa mahakamani, yumo Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Shaaban Maranda

Juzi Chiligati ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM alitoa tamko la kukisafisha chama hicho na kashfa hiyo akisema haina uhusiano wowote na wala hawaitambui kampuni ya Kagoda.

"Vita dhidi ya ufisadi na rushwa nyingine ielekezwe kwa mtu mmoja mmoja na siyo CCM kwani haiwezekani wana-CCM wote wakaenda benki kuiba fedha hizo pamoja," alisema Chiligati na kuongeza: "kampuni ya Kagoda haina uhusiano wa aina yoyote na CCM na wala CCM hatuijui".

Alisema kwa muda mrefu viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakifanya juhudi za makusudi kutaka kuihusisha kampuni hiyo na CCM na kutoa mfano kwamba, hivi karibuni Kabwe alinukuliwa akisema kwamba kuisha kwa suala la EPA kwa kiwango kikubwa kunategemea Kagoda itakavyochukuliwa hatua za kisheria.

Alisema CCM ni chama chenye kuheshimika, makini na safi, hivyo vijana wadogo iliowalea kuanza kukipaka matope ni kutafuta laana na njama zao hazitafanikiwa.

Yaani huyu Chiligati anafanya watu wajinga ama? Anataka kusema kuwa kila mwanachama wa-CCM ni kiongozi? Aliyekamatwa na ngozi ni mwizi. Ni lazima CCM na viongozi wahujumu nchi wawajibishwe.

Ukaguzi wa CAG, kama independent, ni hatua ya kwanza.
 
Nahisi kama anafuata nyayo za Kingunge Ngombale Mwiru. Naye alianza hivyo hivyo, kwa hiyo tunaamini huyu Chiligati safari yake inakaribia ukingoni mwa siasa.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, bado anasisitiza kuwa Kampuni ya Kagoda ni mali ya chama tawala CCM.
* Adai fedha ilizochotwa EPA zilitumika uchaguzi mkuu 2005

Na Kizitto Noya

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kukataa uhusiano wake na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited iliyochota zaidi ya Sh40 bilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.

Zitto aliyekuwa anajibu mapigo ya CCM iliyomshutumu juzi kwa kuipaka matope kwa kuihusisha na Kagoda, alisisitiza kuwa CCM haiwezi kujivua gamba la Kagoda kwa kuwa ndiyo inayomiliki kampuni hiyo, ikiwa miongoni mwa kampuni 22 zilizochota jumla ya Sh133 bilioni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

"CCM ndiyo inayomiliki Kagoda na Kagoda ni ya CCM. Fedha za Kagoda ndizo zilizotumika kwenye kampeni za CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Huu ndio ukweli," alilisitiza Zitto.

Alisema kauli ya chama hicho iliyotolewa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati kuikana kampuni ya Kagoda, ililenga kujisafisha lakini pamoja na jitihada hizo, ukweli utaendelea kubaki kuwa kampuni ya Kagoda ni mali ya CCM.

Kwa mujibu wa Kabwe, endapo CCM inataka kutakata inatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu zake za mwaka 2004/2005 na ieleze wapi ilipata fedha za uchaguzi mkuu mwaka 2005 uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani.

"Kama ni kujisafisha njia nzuri kwao si kutoa matamko, chama hicho kinatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu akikague na baadaye waseme fedha walizotumia katika uchaguzi mkuu mwaka 2005 zilizotoka wapi," alisema.

Alisema hakuna mantiki wala uhalali kuwaondoa mafisadi wa EPA katika uhusiano na CCM, kwani sehemu ya fedha iliyochotwa kwenye akaunti hiyo, zilitumiwa na CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2005.

"Mimi nasema hii ni spinning (kupindisha ukweli), kama mtu amechota Sh40 bilioni na sehemu ya fedha hizo zikatumika kwenye uchaguzi wa CCM utawezaje kukiondoa chama hicho kwenye ufisadi huo?" alihoji na kuendela:

"Kama CCM wataweza kuthibitisha kwa ushahidi kwamba hawahusiki na ufisadi huo na kwa ushahidi wa taarifa ya mkaguzi mkuu kuhusu chama hicho, niko tayari kuwajibika na maelezo yangu," alisema.

Katika hatua nyingine Zitto alisema Chadema inatarajia kutoa tamko kuhusu kauli ya Chiligati kwamba vijana wanatakiwa kuacha kuifuatafuata CCM kwa kuwa walizaliwa wakaikuta ikiwa imara na watakufa na kuiacha ikiwa imara.

Alisema kauli hiyo ni hatari kwa usalama wa vijana wa aina yake wanaotetea maslahi ya umma hivyo chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) lazima kitoe msimamo wake katika hilo.

"Labda nimalizie kwa kusema kwamba Chiligati anaposema sisi vijana tunaoifuata fuata CCM tutakufa na kuiacha CCM imara ni very serious. Kama chama (Chadema), leo (jana) tutaitolea tamko kauli hiyo kwani tunahisi wanataka kutuua," alisema.

Kabwe alitoa kauli hiyo siku moja baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoa tamko rasmi kuiruka kampuni ya Kagoda Agricultral Limited ikisema kuwa haina uhusiano nayo.

Chiligati aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa chama hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na kampuni hiyo na kwamba hata kama kuna mwanachama anayehusika, ni suala lake binafsi na sio kwa mwavuli wa chama.

Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiihusisha CCM na Kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni kwenye akaunti hiyo na miongoni mwa watuhumiwa wa EPA waliokwishafikishwa mahakamani, yumo Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Shaaban Maranda

Juzi Chiligati ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM alitoa tamko la kukisafisha chama hicho na kashfa hiyo akisema haina uhusiano wowote na wala hawaitambui kampuni ya Kagoda.

"Vita dhidi ya ufisadi na rushwa nyingine ielekezwe kwa mtu mmoja mmoja na siyo CCM kwani haiwezekani wana-CCM wote wakaenda benki kuiba fedha hizo pamoja," alisema Chiligati na kuongeza: "kampuni ya Kagoda haina uhusiano wa aina yoyote na CCM na wala CCM hatuijui".

Alisema kwa muda mrefu viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakifanya juhudi za makusudi kutaka kuihusisha kampuni hiyo na CCM na kutoa mfano kwamba, hivi karibuni Kabwe alinukuliwa akisema kwamba kuisha kwa suala la EPA kwa kiwango kikubwa kunategemea Kagoda itakavyochukuliwa hatua za kisheria.

Chiligati alisema Zitto pia alinukuliwa akisema kushindwa kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya Kagoda kuna maana moja tu na kwamba kampuni hiyo ndiyo inayoijengea CCM Kaburi.

Katibu mwenezi huyo alisema shutuma zinazotolewa na Zitto na wapinzani wengine ni siasa zenye takataka zinazolenga kuipaka matope CCM na kwamba ni za uzushi na uzandiki.

Alisema CCM ni chama chenye kuheshimika, makini na safi, hivyo vijana wadogo iliowalea kuanza kukipaka matope ni kutafuta laana na njama zao hazitafanikiwa.

Source Mwananchi
 
Date::12/15/2008
Danadana zaendelea Kagoda

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

DANADANA za sakata la Kagoda Agriculture zinazidi kushika kasi, baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kusema kuwa, mwenye mamlaka ya kulizungumzia suala la kampuni hiyo kuhusishwa na wizi wa fedha nyingi kwenye Akaunti ya Malimbikizo ya Madeni ya Nje (EPA) si yeye.

Kampuni hiyo imekuwa kama zimwi kutokana na kila mtu kutotaka kuizungumzia kwa kina na hasa kuhusika kwake kwenye uchotaji wa fedha kwenye akaunti hiyo iliyo Benki Kuu (BoT) na wamiliki wake, huku wapinzani wakiitumia kama kete yao ya kisiasa dhidi ya chama tawala, CCM, wakidai kuwa chama hicho ndicho kilichotumia fedha zilizochotwa na Kagoda kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

Katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alitumia ziara yake wiki iliyopita kukanusha kuwa CCM haihusiki na kampuni hiyo inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni kati ya Sh133 bilioni zinazodaiwa kuchotwa na makampuni 22 kwenye akaunti hiyo, lakini presha bado ziko kwa watendaji wakuu wa serikali kuzungumzia mintaarafu ya Kagoda na mustakabali wake kwenye kashfa ya EPA.

DPP, Elieza Feleshi alisema mwishoni mwa wiki kuwa anayepaswa kuulizwa kuhusu suala la upelelezi wa baadhi ya majalada alioeleza awali kuwa unafanyika ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba.

Feleshi, ambaye siku za karibuni ameonekana kutotaka kuulizwa habari za mchakato wa EPA hasa suala la Kagoda, aliliambia gazeti hili kwamba wa kuulizwa kuhusu upelelezi si yeye.

"Nafikiri kwanza muulize DCI, kama ni upelelezi yeye ndiye anajua," alisema DPP.

Hata hivyo, alipoulizwa zaidi kwamba yeye ndiye alitangaza kuagiza upelelezi zaidi kwa baadhi ya majalada kwenye kashfa ya EPA, Feleshi alijibu kifupi: "Fanya nilivyokuelekeza."

Alipoelezwa kwamba DCI ameshasema kuwa mamlaka ya tuhuma au majalada ya kesi za EPA yako kwake (DPP) na kwamba, mwandishi angependa kujua zaidi suala la Kagoda, alijibu kwa kuuliza: "Hatuelewani."

Tayari Kamishna Manumba ameshasema kwamba mamlaka yote ya kuzungumzia mchakato wa tuhuma za EPA kwa sasa yako kwa DPP.

Kamishna Manumba alisema kiongozi wa mchakato mzima wa kufikisha watuhumiwa mahakamani na majalada yote ni DPP.

DPP anatoa kauli hiyo wakati Rais Jakaya Kikwete akiwa ameshaeleza kuwa jukumu la kuendesha kesi sasa liko kwa mkuu huyo wa mashitaka, kiasi cha kufanya watendaji wengine wa vyombo vya dola kutokuwa tayari kulizungumzia.

Hata hivyo, Feleshi, ambaye anasemekana kuwa anafanya kazi zake kwa makini, amekuwa akiyarudisha baadhi ya mafaili kwa watendaji wengine kila anapobaini kuwa ushahidi hautoshi kwa watuhumiwa kufikishwa mahakamani.

Alisharipotiwa kufanya hivyo kwa waziri wa zamani, Nazir Karamagi ambaye alikuwa akidaiwa kutosikiliza ushauri wa wataalamu kabla ya kusaini mkataba wa mgodi wa Buzwagi baada ya kuona ushahidi uliowasilishwa dhidi yake kutokidhi mahitaji.

Kampuni ya Kagoda imeibua mjadala mzito kutokana na kwamba ndiyo iliyochota fedha nyingi Sh40 bilioni kati ya makampuni yote 22 yanayotuhumiwa kuiba zaidi ya Sh133 bilioni kutoka akaunti hiyo.

Mbali ya Kagoda kuwa kete ya kisiasa, lakini pia kampuni hiyo ambayo iliiba fedha kwa mgongo wa Idara ya Usalama wa Taifa, imeibua mjadala miongoni mwa watu wa kada tofauti.

Hatua ya wamiliki wa Kagoda kutofikishwa mahakamani, inazidi kuacha maswali mengi kwamba huenda kuna mkono wa vigogo.
 
Shindilia hapo hapo Mh. Zitto, hakina kwaachia wapumue hadi kielweke!

Yaani ni aibu gani mtu mzima eti walio iba ni wanachama wa CCM si CCM, kwani CCM ni ninini? si mkusanyiko wa wanachama hao hao ambao waliiba tena kwa manufaa ya chama hicho hicho??

Za mwizi zenu zimetimia.. Chiligati et al...kaa tayari
 
Hesima mbele mkuu.
Naomba tupanue kidogo huu mjadala kuhuisiana na hizi fedha zinazodaiwa kupelekwa CCM kwa ajili ya kampeni.
Kwa mtazamo wangu, hata kama aliyepeleka alikuwa individual, alifanya hivyo kwa lengo la kusaidia kitu fulani-na kitu hicho (kulingana na wakati) ilikuwa ni uchaguzi. Tunajua kuwa ili mtu achaguliwe, anahitaji kuwa nomibnated na chama. nadhani hapo ndipo CCM inapounganika na fedha hizo kwa sababu zililetwa na individual kwa ajili ya mgombea/wagombea wa CCM.
Au, unataka kutueleza kuwa fedha hizo zilizoingizwa na individual zilitumika individually? yaani zilipelekwa ofisi za Mindu badala ya Lumumba?

- Mkuu Mpitanjia,

Heshima mbele sana, kwani sheria inasema nini kuhusu individuals kutoa misaada mbali mbali kwa vyama vyetu vya siasa? Maana kama ipo, basi inatakwia kuwabana pande zote mbili yaani CCM na Upinzani,

- Kwa vyama vyetu vya siasa, kupokea misaada ya wazawa, au ya kutoka foundation ya Tony Blair sidhani kama kuna sheria imevunjwa, au?
 
Si kweli.

Chama kinatakiwa kimpelekee Msajiri ripoti ya akaunti zake ambazo zimeshafanyiwa ukaguzi na chama chenyewe tayari. Na hapo ndio kuna tatizo.

- Sasa usalama wa taifa unafanya nini hapa?
 
Mkuu sijakuelewa hata chembe.
Fedha inayoongezwa individually kusaidia chama haimo kwenye hesabu ya fedha ya chama. Je hii ina maana kwamba CCM ikiongezewa fedha individually, let say 40,000,000,000.00 kutoka kampuni ya Kakiti Agricultural Co, fedha hiyo has nothing to do with CCM??!!!??!!??

Una maana fedha zinazofanyiwa auditing ni zile zitolewazo toka serikalini tu?au namna gani!!?

If that has nothing to do with with CCM as a party, tutajua vipi chama kinapewa fedha na KGB ,Maharamia wa Somalia, au kinanunuliwa kwa bei chee na wanachama wake ambao ni wahusika wakuu wa wizi wa aina zote serikalini?
Je mtu binafsi akikipa Chama fedha, fedha hiyo haihesabiwi kama source moja ya income ya chama?

Ni katika kutaja kujua tu mkuu, maana kuuliza si ujinga ila kubwatuka ndiyo.

- Kwani sheria inasema nini mkuu kuhusu misaada ya individuals kwa vyama vyetu vya siasa? I understand the anger lakini kama kweli hizi hela zote ziliibiwa na CCM na kutumika kumchagua rais, sasa anatoa wapi ubavu wa kuwafikisha kwenye sheria huku akijua kwua watamtaja na yeye kuhusika?

I mean hoja zingine mbona hata common sense inakataa kukubali?
 
Kagoda ni mali ya Rostam, nafirki Zitto anachotaka ksuema ni kesi iende kwenye sheria maana itaibua mengi sana, lakini sio siri kwamba Kagoda ni ya Rostam.

Hata Zitto, anajua kuwa kuna mkataba wa Kagoda na BOT, uliosainiwa na Rostam kwa niaba ya Kagoda, na Mgonja kwa niaba ya Serikali.

Hata mimi ninayo copy!
 
Mkuu FMES

Hizi ni news kwangu...mbona ilisemekana kuwa hakuna mkono (signature) wa Rostam popote kwenye hii kitu inaitwa Kagoda..kumbe kuna "mkataba" aliwahi kuweka mkono wake..??!!
 
Shindilia hapo hapo Mh. Zitto, hakina kwaachia wapumue hadi kielweke!

Yaani ni aibu gani mtu mzima eti walio iba ni wanachama wa CCM si CCM, kwani CCM ni ninini? si mkusanyiko wa wanachama hao hao ambao waliiba tena kwa manufaa ya chama hicho hicho??

Za mwizi zenu zimetimia.. Chiligati et al...kaa tayari

Rwagubiri

Una maana unapingana na ukweli kuwa CCM ni Independent entity?
 
Kagoda ni mali ya Rostam, nafirki Zitto anachotaka ksuema ni kesi iende kwenye sheria maana itaibua mengi sana, lakini sio siri kwamba Kagoda ni ya Rostam.

Hata Zitto, anajua kuwa kuna mkataba wa Kagoda na BOT, uliosainiwa na Rostam kwa niaba ya Kagoda, na Mgonja kwa niaba ya Serikali.

Hata mimi ninayo copy!

Zito yupo sawa kabisa kagoda ni ccm na ccm ni kagoda.
Rostam ni mwizi aliyebarikiwa na CCM kufanikisha wizi wa mali ya umma. Zito anachofanya analiweka swala zima la kagoda hadharani na nia ya kagoda kuanzia CCm, Rostam, BOT na mgonja.
Mhesmiwa field usitishike na nani alisaini au jina la nani lilifika bank kumbuka CCM ni mkusanyiko wa watu na Rostam ni mmojawapo.
 
Wakati huo Rostam alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Kama aliweka mkono ilikuwa ni kwa niaba wa CCM. CCM ni mkusanyiko wa wezi - iwe kura ama kula.
 
Sasa yule alipelekwa leo mahakamani itakuwaje ! kama alihusika huku na anasiri nyingi sidhani kama anaweza kutoswa namna hii siataibua haya.Mhhhhhhhhhhh hapa panasomeka kichina hizi safari za mahakamani ni kujitoa one for the team hakuna lolote.
 
I kind of like the pressure from the opposition parties politicians. I wish wananchi tungeweza kuandamana kuonyesha hasira zetu juu ya mafisadi. The likes of Zitto, Slaa and Lipumba should oragnize a public rally ili wananchi tutuoe hasira zetu. Yaani kama Ugiriki vile! But hey! We are getting there. Aint we?
 
CCM wameibiwa na Mafisadi wao ndio maana wamekasirika. Sasa watawakomesha hao mafisadi walio Ifisadi CCM. Tunawaita Mafisadi Viwembe. CCM itatumia Upanga wa Kodi kupata hizo hela zilizofisadiwa. Fisadi anazaa mafisadi nao wanazaa Lifisadi nalo linazaa,kafisadi nako kanazaa Vijifisadi navyo vinazaa,Tufisadi.
 
Sasa yule alipelekwa leo mahakamani itakuwaje ! kama alihusika huku na anasiri nyingi sidhani kama anaweza kutoswa namna hii siataibua haya.Mhhhhhhhhhhh hapa panasomeka kichina hizi safari za mahakamani ni kujitoa one for the team hakuna lolote.

You are damn right.
kikwete lazima aje na mbinu nyingine ili kuweza kumwamini, haya yote yanayotokea ni drama big time. ukijaribu angalia jinsi hawa waheshimiwa wanavyofika mahakamani unaona bonge ya usanii.
Sina imani na kikwete na serikali yake wote ni genge la majambazi wamesha iiba sasa wanatuchezea cheusi chekundu.
Kampeni ya 2010 na kampeni ya yeye kuendelea kupata misaada kutoka kwa wafadhili ndio inayochezwa.
Lets watch and see......
 
Back
Top Bottom