Hii ilikuwa dili ya wizi, iliandaliwa ikawa inasuburi muda wa kuipitisha bila watu kushtuka; hebu fikiria siku 3 kabla ya uchaguzi na viongozi wengi serikalini wakati ule hawakuwa na uhakika wa kushinda majimbo yao!Kama ni kweli hizo pesa CCM walipanga kuiba kwa ajili ya uchaguzi, kweli wangechukua siku tatu kabla ya uchaguzi wenyewe? Siku tatu zingesaidia nini? Walizigawa lini kwenye majimbo husika?
Labda waliiba ili kulipa madeni. Vinginevyo timeline ni kama hai make sense.
Hivi uchaguzi uliahirishwa tarehe ngapi? Kama walichota baada ya uchaguzi kuahirishwa, hapo ina make sense.
Huenda wajanja wachache walitumia vurugu za kwenye uchaguzi ili kutuibia.
Kama ni kweli hizo pesa CCM walipanga kuiba kwa ajili ya uchaguzi, kweli wangechukua siku tatu kabla ya uchaguzi wenyewe? Siku tatu zingesaidia nini? Walizigawa lini kwenye majimbo husika?
Labda waliiba ili kulipa madeni. Vinginevyo timeline ni kama hai make sense.
Hivi uchaguzi uliahirishwa tarehe ngapi? Kama walichota baada ya uchaguzi kuahirishwa, hapo ina make sense.
Huenda wajanja wachache walitumia vurugu za kwenye uchaguzi ili kutuibia.
Kama DPP na waziri Chikawe hawawezi kuwashitaki wahusika wa Kagoda kisa hawana ushahidi. Je mtu/watu binafsi si wanaruhuiswa kufungua mashtaka? Kama ndivyo basi nashauri ili kuonesha ujasiri na kujiamini kwa wale walio na ushahidi wa kutosha wafungue hizo kesi wao binafsi. Ninaamini kama kweli na ikagundulika kwamba hao jamaa waliiba na wakanyweshwa mvua kwenda Segerea, heshima ya aliye/watakaofungua hiyo kesi itakuwa kubwa sana. Na kama ni chama basi kuna uwezekano mkubwa wa chama hicho kushika hatamu za uongozi wa nchi hii kuliko hawa wajulikanao kama mafisadi!
Duh, maskini sisi watanzania- bao waziwazi!
Kama haiwezekani, angalau wawafunge walioshiriki kupoteza nyaraka brela na benki, kwa kutumia vibaya ofisi zao au kitu kama hicho.
Outlier, sidhani kama atafungwa mtu maana watuhumiwa wote wana siri nzito dhidi ya watawala wetu wa juu nasikia hata wale wa EPA na mawaziri waliofikishwa kizimbani hivi karbuni wameanza kuziweka dhidi hizo vizuri ili walale mbele na watawala.
Labda ndiyo maana Pinda, Mwanasheria Mkuu Mwanyika na Mkuu wa polisi wakatwambia Watanzania mafisadi ni 'matajiri' wakubwa wakifikishwa mahakamani basi 'nchi itawaka moto' na kushindwa 'kutawalika'
Kila ofisi nyeti Tanzania imeshikwa na mafisadi hivyo wanapoamua documents muhimu katika ushahidi dhidi yao zipotee, basi zinapotea bila matatizo yoyote. Mungi inusuru Tanzania toka mikononi mwa mafisadi.
Mafisadi wajue maisha ya DUNIA ni maisha ya kupita...kwanza watenge muda kujiuliza kwanini watu wanakufa....?
Wajiulize wapo wapi watawala waliokuwa na Nguvu, Mali na sasa hawapo tena?
Yupo wapi..Nyerere, Yupo wapi kwame Nkrumah, Yupo wapi Mobutu?, Yupo wapi Gamal AbdulNasir? Yupo wapi Catro(Yu Hoi kitandani...)..Yupo wapi Sharooun( kufa hafi na mateso ya DUNIA anayapata...)..Yupo wapi Hitler?...nimetaja mifano mbalimbali kuonesha kuwa Uongozi una mwisho...na MJUE DHULMA HAIDUMU...!!!
Watanzania ambao leo hii mnawaibia ipo siku watasema basi kudhulumiwa!!!