Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

'Ikulu ilichukua faili la Kagoda'





Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Serikali wa Usajili wa Kampuni (Blera) Esteriano Mahigila akifafanua jambo kuhusu kadoga habari kamili soma pembeni
Leon Bahati


WAKALA wa serikali wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) jana ulifafanua utata wa faili la usajili wa kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ukisema kuwa halikuwepo kwenye ofisi hizo kwa muda mrefu kutokana na maagizo ya rais.


Kampuni hiyo, ambayo umiliki wake umekuwa gumzo, inadaiwa kuchota Sh40 bilioni kutoka katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), lakini hadi sasa wamiliki wake hawajafikishwa mahakamani kama ilivyo kwa watu wengine 21 waliopandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kuiba jumla ya Sh133 bilioni kwenye akaunti hiyo.


Waandishi wa habari wamekuwa wakifuatilia mintaarafu ya kampuni hiyo kwenye ofisi za Brela bila ya mafanikio na hivi karibuni kuliibuka habari kuwa faili la kampuni hiyo limetoweka Brela, hali iliyozua wasiwasi kuwa huenda sakata la Kagoda litazimwa.


Lakini jana, msajili wa makampuni, Esteriano Mahingila aliwaambia waandishi wa habari akisema: "Nataka niwaambie kuwa nyaraka za Kagoda zipo. Kama kuna mtu anahitaji kuziona anaweza kuzipata, hata kama anataka kupiga 'photokopi' (kudurufu) faili zima, hakuna siri yoyote katika usajili wa kampuni."


Hata hivyo, Mahingila alisema kwa muda mrefu faili la Kagoda limekuwa halipo kwenye ofisi za Brela kwa sababu lilichukuliwa chini ya maagizo ya Rais Jakaya Kikwete tangu kampuni hiyo ilipohusishwa kwenye ufisadi wa EPA.


Alisema kuwa faili hilo pamoja na mengine ya kampuni zilizotajwa kwenye kashfa ya EPA, yalichukuliwa na kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa harakati za kushughulikia tuhuma za wizi wa EPA.


Mahingila pia alitangaza wamiliki wa kampuni hiyo akiwataja kuwa ni Francis William, ambaye alisema anamiliki asilimia 60 ya hisa na Johnson Kyomhando, ambaye anamiliki asilimia 40.


Majina ya watu hao yamekuwa yakiripotiwa na vyombo vya habari, lakini upatikanaji wa wamiliki hao umekuwa ni mgumu, kiasi cha kubashiriwa kuwa hakuna watu wanaotumia majina hayo.


Kwa mujibu wa taarifa kadhaa za uchunguzi zilizoripotiwa na vyombo vya habari, mawasiliano yaliyo kwenye nyaraka za usajili wa kampuni hiyo yanaonekana kuwa ni ya kampuni za wafanyabiashara maarufu.


Kuhusu taarifa za kupotea kwa faili la usajili wa Kagoda, Mahingila alisema kuwa kuwa mpangilio wa kuhifadhi kumbukumbu za kampuni katika ofisi ya Brela hufanywa kwa njia ambayo hata kama faili likipotea, taarifa zote zinaweza kupatikana kwenye daftari la msajili bila wasiwasi wowote.


"Nashangaa hawa watu walioandika hivi bila kuja kuniona. Taarifa za kampuni hatuziweki tu kwenye faili, bali zinaweza kupatikana pia kwenye daftari la registrar (msajili)," alifafanua Mahingila kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo).


Taarifa kuhusu kumbukumbu za Kagoda zimekuwa ni gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu hasa baada ya kutajwa kwenye orodha ya kampuni zilizochota mabilioni ya fedha za EPA.


Baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani mara kadhaa vimeitaja kampuni hiyo ya Kagoda kuwa ilitumiwa na CCM kuchota fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2005.


Hata hivyo, katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM- Itikadi na Uenezi,- John Chiligati alikanusha habari hizo, akisema kwamba chama chake hakihusiki na wala hakina uhusiano na kampuni hiyo.


Mahingila aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa anashangaa kusikia kuwa upatikanaji wa taarifa za Kagoda umekuwa ni mgumu, akisema hakuna mwandishi yeyote aliyewahi kumfuata ofisini na kumtaka aone faili ili kujua wahusika.


"Mtu yeote anaweza kuona kumbukumbu zote za mafaili kwa kulipia Sh1,500 tu na kwa waandishi wa habari, hii ni bure, hawatahitaji kulipa chochote," alibainisha Mahingila.


Alisema Kyomuhendo na William walijitambulisha kwenye kumbukumbu za usajili kuwa wanapatikana katika kitalu namba 87, eneo la viwanda Kipawa, wilayani Temeke.


Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaonyesha kuwa Kagoda ilisajiliwa Septemba 29, 2005, siku moja baada ya kuomba usajili na baada ya mwezi mmoja, BoT ikaanza kuidhinisha sehemu ya malipo yaliyochotwa EPA.

KUMBE NA RAISI ANAHUSIKA LOOH!!!
 
LOH kikwete huna hata haya rais wetu watu wanapiga kelele kwenye magazeti websites kumbe msaafu wote unao weye haya tunakusubiri ahsante mr breila
 
Mungu wanugu, sasa kwenye hiyo taarifa Rais anahusika je? Kama mumeambiwa record zote zipo... then Rais anahusika je? Tena kwenye hiyo hiyo taarifa kina hiki hapa

Alisema kuwa faili hilo pamoja na mengine ya kampuni zilizotajwa kwenye kashfa ya EPA, yalichukuliwa na kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa harakati za kushughulikia tuhuma za wizi wa EPA.
 
CCM ni Safi kwa hili..

Leo nimefikiria sana kuhusus chama changu,Ninaona Kama vipi Tulio wasafi tujitenge na Mafisadi..Tuwafukuze katika Kamati kuu na wawe na chama chao..
 
CCM ni Safi kwa hili..

Leo nimefikiria sana kuhusus chama changu,Ninaona Kama vipi Tulio wasafi tujitenge na Mafisadi..Tuwafukuze katika Kamati kuu na wawe na chama chao..

Au ninyi wasafi mjitoe muanzishe chama chenu
 
Wewe ninaamini ni msomi,sasa unakubalije kudanganyika kiurahisi hivyo?

Wakulu heshima Mbele,
Watu kila siku tumekuwa tukipiga kelele sana hapa Jamvini tukitaka kuwajua wamiliki wa kagoda.Tumekuwa tukiwahusisha watu na CHama cha Mapinduzi kwa hili na wengi tukihisi mambo mengi sana.

Jana Msajili wa Kampuni wa BRELA kaweka wazi wamiliki ni Bwna aJohn na Francis.Na Dr. Slaa alisema wamiliki wa Kagoda ni viongozi Flani wa CCM,zitto anasema zilitumika katika kampeni za CCM mwaka 2005.Sasa nani anatudanganya hapa?

Kuna mtu ana wasifu wa watu hawa,

Je ni kina nani na wanafanya shughuli zipi?
Je ni wanachama wa chama chochote?
Je wana undugu na Kiongozi yeyote?
Je wana historia ya Ufisadi?
Je wako hai?
Je wanaweza kutishia usalama wa Nchi?
Je wana nguvu gani mpaka wasikamatwe mpaka sasa?
Je hawa ni wadhamini wa Kampeni za CCM?

Hao ndiyo wamiliki walioko BRELA,Hivyo Kagoda siyo mali ya CCM na CCM haihusiki?Kwa sasa naamini hivyo mpaka pale nitakapoambiwa wasifu wa hawa watu
 
Wewe ninaamini ni msomi na una akili,sasa unakubalije kudanganywa kiurahisi hivyo?Hayo ni mapandikizi tuu.

Wakulu heshima Mbele,
Watu kila siku tumekuwa tukipiga kelele sana hapa Jamvini tukitaka kuwajua wamiliki wa kagoda.Tumekuwa tukiwahusisha watu na CHama cha Mapinduzi kwa hili na wengi tukihisi mambo mengi sana.

Jana Msajili wa Kampuni wa BRELA kaweka wazi wamiliki ni Bwna aJohn na Francis.Na Dr. Slaa alisema wamiliki wa Kagoda ni viongozi Flani wa CCM,zitto anasema zilitumika katika kampeni za CCM mwaka 2005.Sasa nani anatudanganya hapa?

Kuna mtu ana wasifu wa watu hawa,

Je ni kina nani na wanafanya shughuli zipi?
Je ni wanachama wa chama chochote?
Je wana undugu na Kiongozi yeyote?
Je wana historia ya Ufisadi?
Je wako hai?
Je wanaweza kutishia usalama wa Nchi?
Je wana nguvu gani mpaka wasikamatwe mpaka sasa?
Je hawa ni wadhamini wa Kampeni za CCM?

Hao ndiyo wamiliki walioko BRELA,Hivyo Kagoda siyo mali ya CCM na CCM haihusiki?Kwa sasa naamini hivyo mpaka pale nitakapoambiwa wasifu wa hawa watu
 
Mungu wanugu, sasa kwenye hiyo taarifa Rais anahusika je? Kama mumeambiwa record zote zipo... then Rais anahusika je? Tena kwenye hiyo hiyo taarifa kina hiki hapa

eheeheeeee da atakuwepo tu mbona tunawalalamikia hawakanushi wajameni, hivi ile issue ya Mzindakaya na BOT iliishia wapi? siku za hivi karibuni nilimuona TIB sijui anachota nyingine
 
Tikerra,

Sasa kama tunalazimishwa kuamini tusichokubali unategemea tufanye nini?Tumekuwa tukikubali kuzugwa kwa muda mrefu sasa..Mie kuna kipindi nilihisi kukata tamaa.

Kuna mawili,kuamua kujiunga nao au kuamua kujitoa .Na kujitoa nidyo wazo zuri sababu hawa wakiguswa tu nchi itashindwa kukalika..hivyo ni kukimbia uchafu tu kuliko kukaa nao.

Mie ni msafi kwanini nikae karibu na shimo la takataka hata kama wana nguvu.Ila najiuliza nikimbiliea wapi kusiko na uchafu?Nahisi natakiwa kukimbilia kule ambako kuna tumaini la maisha ya mtanzania..
 
kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima la leo, Bw. Francis Willium alifariki kabla ya kusajili hiyo kampuni yaani hakuwepo wakati Kagoda inasajiliwa. Sasa huenda hata hili jina la John kyomuhendo limetungwa au marehemu fulani hivi.

zaidi ya hilo. Mwanahalisi la wiki hii linaripoti kwamba, afisa wa NBC aliyekuwa anapokea maagizo/maelekezo na Balali ya kuwalipa Deep green, Meremeta na Tangold, pia alishafariki sanjari na kifo cha Balali.
 
Jamani sio rahisi kama watanzania wengi tunavyofikiri kuwa itatokea siku Mhishimiwa RA atapelekwa mahakani, kwa sababu zifuatazo
  1. Yeye ndiye mfadhiri mkubwa wa CCM na anawafadhiri kwa pesa ya watanzania.
  2. Ikibainika kuwa serikali iliyopo madarakani ilitunia pesa za wizi kuingia madarakani itabidi ijiudhuru na kutoa nafasi ya uchaguzi mpya ndio maana hakuna cha Deep Green finance wala Kagoda Ltd itakayoongelewa hapa
  3. Rahisi na yeye anaweza kuhusishwa na EPA ambapo ndio itakuwa mwisho wake wa kisiasa

Katika situation kama hizi sioni ni jinsi gani hata hao waliopelekwa mahakamani watafungwa zaidi ya kutuzuga na kutudanganya watanzania kuwa serikali hiko serious wakati hakuna lolote.

Hawa wanatengenezewa mabilioni mengine kama fidia ya kuwashitaki bila makosa na kuwadhalilisha mbele ya jamii, wait and see watalipwa mabilioni mengine muda si mrefu hakuna hata mmoja atayefungwa.

Tanzania ni shamba la bibi kila mtu anachuma na kula anachokiweza ndio maana ni vizuri wale watoto wa mlimani waendelee kugoma ili nao wapewe share yao ya keki badala ya kuwadanganya na kuwapa 40%, sasa kasheshe ni wagonjwa wagome namna gani sijui ili na wao wapewe share yao maana kikwete na kundi lake wanatafuna tu na hakuna kinachoendelea.
 
CCM ni Safi kwa hili..

Leo nimefikiria sana kuhusus chama changu,Ninaona Kama vipi Tulio wasafi tujitenge na Mafisadi..Tuwafukuze katika Kamati kuu na wawe na chama chao..

Subutu!!!! CCM hii ya akina JMK, RA, EL, Makamba, Msekwa, Mramba, Yona, Chenge, Maranda,n.k,
Labda muunde chama kipya cha mapinduzi, lakini hiki tunachokifahamum kinachotutafuna wadanganyika hakiwezi kuwa safi hata mkioshe na sabuni gani hata kikiogeshwa na maji ya katikati ya bahari hakiwezi kuwa safi.
Halafu mkubwa kama sio mapenzi binafsi kwa chama chako ungeweza kufanya tafakuri kidogo tu ungegundua kuwa hao wamiliki wa kagoda waliotajwa na msajili wa brela ni wa kutengenezwa.Kama ungekuwa makini kuisoma post ya Invisible kagoda ni RA, ungezingatia ushahidi uliotolewa ndipo ungejua kwanini watanzania tulio thabiti bila kuweka ushabiki wa itikadi za vyama vya siasa tunaamini kuwa hawa unaotaka tuwajadili sio wamiliki halali wa kagoda, tuaamini kuwa RA ndiye mla nyama hawa wawili wameshikishwa ngozi tu.
 
Ze Komedi, hatimaye wamekubaliana kuwapeleka mbuzi wa kafara mahakamani na wakina Rostam na Apson Mwang'onda kutamba uraiani. Ama kweli Mkapa bado ana ubavu, Kikwete ameshindwa kujitoa kafara! Sasa jitihada za kuwataja zinakuwa kubwa kweli zikifuatiwa na kelele za mahakamani. Chami na Chikawe walitumwa kupima maji na ku-divert attention, BRELA wamesawazisha. Sasa tatu, tatu!

PM

Hawa mbona ni wamoja!, yaani wote hao ni Ze Komedi. upande mmoja wasoma habari upande mungine ni wafanya matukio
 
East African Business week iliwahi kutoa ripoti ifuatayo :-

Dar es Salaam — Controversy over the ownership of one of the major companies which is accused of looting a big chunk in the $131million EPA account of the Bank of Tanzania, Kagoda Agriculture Limited has raised concerns following reports that the "owner" of the company is dead.

Reports have it that, although both Kyomuhendo and William appear in the documents of the company, these were really not the owners, but names used to formalise legal requirements for the registration of the company.

An official from the Bank of Tanzania (BoT) told East African Business Week last week that, all the cheques were collected by a Tanzanian of Asian origin who later took them to a local bank. It's from there where he was paid the said $30.8 million.

"We have the records. The cheques and the money were neither taken by Kyomuhendo nor William, but only by a CCM bigwig of Asian origin," the official said adding that the businessman was the one who was frequenting the BoT headquarters to demand for payment.

Huyu Official wa BoT bado yupo hai au naye ni moja kati ya waliofikishwa Kisutu ?
 
East African Business week iliwahi kutoa ripoti ifuatayo :-

An official from the Bank of Tanzania (BoT) told East African Business Week last week that, all the cheques were collected by a Tanzanian of Asian origin who later took them to a local bank. It's from there where he was paid the said $30.8 million.

"We have the records. The cheques and the money were neither taken by Kyomuhendo nor William, but only by a CCM bigwig of Asian origin," the official said adding that the businessman was the one who was frequenting the BoT headquarters to demand for payment.

You do not need to use too much effort... That's Roast-em!
 
You do not need to use too much effort... That's Roast-em!

hivi bongo hatuna snippers?? tuchangeni jamani wapo wa kirusi walio kuwa kwenye jeshi lao zamani wanacharge 100,000$ per head.jf hatuwezi kuchanga?? vita dhidi ya ufisadi ni kazi ya siku moja tuu hiii
 
Wakati huo Rostam alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Kama aliweka mkono ilikuwa ni kwa niaba wa CCM. CCM ni mkusanyiko wa wezi - iwe kura ama kula.

Sawa Zitto na wengineo wanajua sana kuwa Kagoda ni ya nani na fedha zilikwenda wapi.Kujua sio tataizo.Sawa mmeshajua, sasa je?
Acha kudaganya.Wote mnaolijua hili suala hakuna miogoni mwenu ambaye anaweza kufanya kitu.Kama RA ndiye mmiliki au aliyekuwa anachukua hizo hela kwa nini hakamatwi?Kwani TZ hii ni yenu.Wenye nchi waacha wale na wataendelea kula.Kama mnaandika kwa ajili ya furahisha genge la JF hongereni.
 
LOL Nyie ni watu wa ajabu sana.

Mnataka kumkamata "RAIS"? ahahahaaaaaa LOL

Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.

Alamsik

FP
 
Back
Top Bottom