Kagoda: Ni Rostam

Kagoda: Ni Rostam

Hivi ule usemi wa anayeshikwa na ngozi... hauna maana kwa Feleshi?. Kama Feleshi anaogopa ajue kuwa "Justice denied is justice delayed" - reversed for Feleshi and his masters in CCM. Ipo siku wale wote waliohusika na Kagoda watafikishwa kwenye mkono wa sheria hata kama watakuwa makaburini, watashitakiwa na vitukuu vyao kufilisiwa kwa madhambi ya babu zao.

Ndiyo maana CCM hawataki wananchi wajichagulie serikali yao na kung'ang'ania wizi wa kura kwani wanajua kuwa wakitolewa tu uozo wao wote utafunuliwa na wengi kujikuta behind bars. Kama mimi ningekuwa ni miongoni mwa waamuzi wa CCM, huu sasa ungekuwa ni muda muafaka wa kuhakikisha nchi ina focus kwa maendeleo ya watu na kuboresha huduma za jamii, kukuza uchumi ili kupata ridhaa halali ya wananchi, kwani wizi wa kura kwa sasa unakaribia kikomo, nafikiri chaguzi si zaidi ya mbili zijazo tutashuhudia ama umwagikaji wa damu mkubwa baada ya wizi wa kura, ama kushindwa na kukubali yaishe (hii ni night mare kwa CCM).

"Hakuna adui mkubwa sana kwa usalama wa taifa kama wananchi kukata tamaa na serikali yao na kutokuona tena umuhimu wa maisha kwao" Ikifikia hali hii basi ni dhahiri usalama wa taifa letu utakuwa matatani zaidi ya "usalama wa CCM" ambao wao wanauita wa taifa. Nina hakika CCM ikiacha utamaduni wa kulindana na kutoa kafara vidagaa na kuwalisha ndoano mapapa kama RA, Chenge, Mkapa et al, Huo utakuwa ni uslama tosha wa Taifa letu na wao CCM wenyewe.
 
Nakubaliana na maneno mazito sana yaliyosemwa humu ndani ya JF.

Kama mna WIVU KWA WENZENU kuchota hela za EPA, MEREMETA, DEEPGREEN, Mwananchi Gold, etc, just GO AND HANG YOUR SELF.

Yes, WENYE WIVU MJINYONGE na TUISHILIE MBALI.......

"Mitanzania mingine ina/tuna wivu wa KIJINGA ...." By Benjamin William Mkapa.
 
Kuzungumzia maendeleo tu bila kuangalia vipingamizi ama vikwazo ni kuzorotesha juhudi za upatikanaji maendeleo ambapo rushwa ndio tatizo kubwa. Nadhani tuzungumze vipaumbele vya maendeleo kwa sasa ambapo rushwa ni kikwazo kikubwa. Kama 30% ya budget inapotelea mifukoni mwa watendaji wa serikali tutapaje huduma za maji safi,afya(hospitali bora zenye wafanyakazi na maabara za kutosha), shule zenye walimu wenye ujuzi sahihi, vitabu na nyumba za walimu na maabara, barabara za kuunganisha miji na vijiji ili kumnufaisha mwananchi kwa kuuza mazao kwa bei halali.Kwahiyo kutokuzungumzia rushwa ni kutokujua misingi halisi ya maendelea ya jamii.
 
Ninaomba mwenye namba ya Feleshi ya simu anipatie tafadhali, mtu huyu kanitia kichefu chefu kikuu.

Sijui sheria za jinai Tanzania zimebadilika au haziko sawa na za nchi nyingi au ni Feleshi ndie kilaza.

Bank Fraud, kwanza unamkamata anaye chukua fedha bank, yeye ndiye mtuhumiwa, mtu huyu anawajibu wa kumtaja aliyemtuma au yeye anabebeshwa dhambi nzima na kupewa maximum hukumu bila huruma, kwa makosa mengi sana mojawapo kuficha majambazi, kuiba, na kucheza na nyara za serikali.

Sasa kama DPP anajua nani alichukua fedha zetu halafu leo anasema hawezi mshitaki, sioni kwa nini DPP asiachie ngazi.
wakati umefika kumwomba DPP atoke madarakani au nasi tulete kitim tim kama kile cha Kadhi na misamaha ya kodi, tuandamane usiku nchi nzima hii ndio dawa, ukizingatia nchi yenyewe giza sauti zetu zitasikika kwa umbali unaotakiwa na tutafika tunapotaka.
 
Napata shida ya kuelewa kauli ya mwanasheria hodari na mwenye ujuzi kama feleshi.kama kazi imekuwa ngumu kwake ni wakati mzuri kwake kukubali kuachia ngazi.
 
Mambo mengine hata hayahitaji kuyajadili.

Hizo fedha ndizo zimetumika ktk kampeni zao na nyingi wamekula hao waliompa huyu jamaa kazi,sasa mnataka ampeleke nani mahakamani?
 
jamani feleshi kwa kiswahili rahisi ni kwamba hawezi kumkamata mtu aliyemteua yeye kushika hicho cheyo

anaweza kumkamata aiyetumwa lakini aliyemtuma hawezi
aliyemtuma ndiye aliyemuajiri feleshi
 
Kuna haja ya kuhoji a hata kupunguza madaraka ya rais ambaye ni mwenyekiti wa Chama kilichoko madarakani .Pesa yetu na haki zetu kweli majibu ni haya tunapewa ? Uwiiii CCM ifie mbali kabisa .Hivi hili si kosa kama DPP hawezi kuamua jambo hili kesho Chama kingine kikiingia madarakani Feleshi hawezi kushitakiwa kwa kushiriki kuhujumu uchumi wa Nchi ?
 
Hivi kazi ya DPP ni kuamua kesi? Maana hapo katoa hukumu ya siri tayari kwamba watajwa hawana hatia. Kumbe hatuna haja ya mahakama Tanzania!

Hivi DPP anajua process nzima ya ku-register kampuni? halafu ya kufungua akaunti ya kampuni benki? kupata leseni ya kuweza kuanza kufanya "transactions" kubwa namna hiyo? Nadhani kama nchi ingelikuwa na DPP wa kweli amabaye anakajichembe kadogo tu ka uwajibikaji alistahili kuwa anakabidhi mafaili leo hii! KAma kweli ni msomi aliyeelimika, basi baada ya maelezo hayo alistahili kuachia ngazi.
 
Ninaomba mwenye namba ya Feleshi ya simu anipatie tafadhali, mtu huyu kanitia kichefu chefu kikuu.

Sijui sheria za jinai Tanzania zimebadilika au haziko sawa na za nchi nyingi au ni Feleshi ndie kilaza.

Bank Fraud, kwanza unamkamata anaye chukua fedha bank, yeye ndiye mtuhumiwa, mtu huyu anawajibu wa kumtaja aliyemtuma au yeye anabebeshwa dhambi nzima na kupewa maximum hukumu bila huruma, kwa makosa mengi sana mojawapo kuficha majambazi, kuiba, na kucheza na nyara za serikali.

Sasa kama DPP anajua nani alichukua fedha zetu halafu leo anasema hawezi mshitaki, sioni kwa nini DPP asiachie ngazi.
wakati umefika kumwomba DPP atoke madarakani au nasi tulete kitim tim kama kile cha Kadhi na misamaha ya kodi, tuandamane usiku nchi nzima hii ndio dawa, ukizingatia nchi yenyewe giza sauti zetu zitasikika kwa umbali unaotakiwa na tutafika tunapotaka.

Namba ya mkubwa huyu ni

0713 317807
Kazi kwako utupe majibu kama kabadili sema nimzamie tena nipate nyingine .
 
JK is very trick!
kuna vyombo viwili amevishika sawasawa:
-idara hiyo ya mashitaka ya jinai
-usalama wa taifa

yaani hawa kazi yao ni kufanya MAZINGAOMBWE,kuwadhalilisha viongozi waliopita kwa kashfa za ufisadi,na kumsafisha huyu bwana mkubwa aonekane msafi
 
Documents zilikuwa forged, hata kama walitumwa hawakuambiwa wa-forge documents. Wizi ni wizi tu hata kama walitumwa kuchukuwa bila kufuata utaratibu STILL HUO BADO NI WIZI.
 
Wanasheria mnisaidie; fedha za EPA kupitia kagoda zimeibiwa Benki Kuu (BOT). Kisai cha Tsh. 40bil zimeibiwa kwa staili ya kuforgi nyaraka. DPP anasema walikuwa wanazichukua hizo fedha wanajulikana ila hawezi kuwashtaki eti walitumwa tu. Sasa anatafuta waliowatuma.
(a) amejuaje kwamba hao jamaa walitumwa?
(b) kama walitumwa si watakuwa wamewataja mabossi wao?
(c) fedha nyingi kiasi hicho si unaweza ku-trace kwa kuangalia bank transactions na kuzifuatilia akaunti husika?
(d) kama aliyewatuma ni Rais, au CCM, DPP atachukua hatua gani? atawaachia hao jamaa anaodai walitumwa?

Ukiona mtu mzima kama mwanasheria Mkuu ANALIA ujue kuna jambo!!! Hayo majibu ni kwamba amechanganyikiwa!!
 
Mambo mengine hata hayahitaji kuyajadili.

Hizo fedha ndizo zimetumika ktk kampeni zao na nyingi wamekula hao waliompa huyu jamaa kazi,sasa mnataka ampeleke nani mahakamani?
Well said, Feleshi anatakiwa awe mzalendo kwa nchi yake aseme ukweli hela zililiwa na CCM full stop!!! siyo anajali tumbo lake tu (Kazi yake), lini tutapata jasiri kutoka kwa viongozi (maofisa) wa serikali kuacha kutumikia wanasiasa badala yake watumikie wananchi??? when?
 
MKURUGENZI wa Mashtaka (DDP), Eliezer Feleshi amesema ni vigumu kuwaburuza mahakamani watuhumiwa wanaohusika na kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, akisema kufanya hivyo kunaweza kuiweka serikali mahali pagumu kwani serikali inaweza kuwakamata waliotumwa kuchukua fedha, lakini ikashindwa kuwanasa waliowatuma.

Ama kweli matukio mengi nchini huitwa - ONLY in Tanzania.
Hivi kweli umewahi kusikia askari akishindwa kumkamata mwizi kwa sababu mwizi huyo katumwa..
Wezi wengi Ulaya hata ktk Benk hutumwa, master planner hubakia kutazama mchezo unavyokwenda...Wauza unga toka Columbia hutumwa lakini wote hawa hukamatwa na wakafungwa pamoja na kwamba wametumwa. Leo Tanzania mtu alotumwa kuiba sii mwizi..Basi kama kweli ipo sheria hiyo tutaibiwa sana..Na hakika ya maneno haya itafungua ukurasa mpya wa sheria kiasi kwamba kesho mahakamani wezi watashinda kesi zao, kwa sababu WAMETUMWA.
 
Mheshimiwa Feleshi mi nafahamu sana diligence yako katika utumishi maana nimefanya kazi na wewe. Natambua umesema hayo kwa kuwa tu umebanwa pande zote mbili za shilingi; kwanza unajua kabisa wezi wa hizo pesa ni kina nani na ndo maana unasema kuwashitaki ni kutoitakia mema serikali, pili ungependa kuona at least hatua fulani zinachukuliwa ndo maana unasema bado mnalifanyia kazi.
Lakini, kwa hili mi naamini umechemsha. Kama mnawajua waliochota hizo pesa, kwa nini msiwakamate hao na kuwashitaki na iwe juu yao kuwataja waliowatuma na kuthibitisha kuwa kweli walitumwa? Mi siyo mwanasheria, lakini kwa common sense hilo haliingii akilini! Hivi kweli ukinituma kwenda kuiba mahindi shambani kwa jirani nikakamatwa na mahakamani nikathibitisha kuwa kewli ulinituma, mshitaki si atakuwa ameua ndege wawili kwa jiwe moja? Nikishindwa kuthibitisha kuwa ulinituma si msalaba unakuwa wangu peke yangu? Wakati mwingine nyie viongozi huwa mnatoa hoja za kitoto sana zinazowashushia hadhi.
 
Ama kweli matukio mengi nchini huitwa - ONLY in Tanzania.
Hivi kweli umewahi kusikia askari akishindwa kumkamata mwizi kwa sababu mwizi huyo katumwa..
Wezi wengi Ulaya hata ktk Benk hutumwa, master planner hubakia kutazama mchezo unavyokwenda...Wauza unga toka Columbia hutumwa lakini wote hawa hukamatwa na wakafungwa pamoja na kwamba wametumwa. Leo Tanzania mtu alotumwa kuiba sii mwizi..Basi kama kweli ipo sheria hiyo tutaibiwa sana..Na hakika ya maneno haya itafungua ukurasa mpya wa sheria kiasi kwamba kesho mahakamani wezi watashinda kesi zao, kwa sababu WAMETUMWA.

yaah! nchi ya kusadikika, tunawahitaji akina Karama, watu wanaodiriki kuziba mapengo ya utawala uliopo. Mpaka lini tutadanganywa kama watoto? Yaani hili hata ukimwambia layman kule bush kabisa hawezi kukubali. aibu tupu nchi hii.
 
ha ha ha .kama tanzania sio nchi ya kwanza duniani kuwa na viongozi wapumbavu kwenye serikali basi naomba nitajiwe nchi ya kwanza ni hipi?
 
MNT - Nyani Ngabu (JF Member).
Hate it or love it.
 
Ndio maana hutakiwi kushindwa kushangaa hawa wasomi ma dk, prof opamoja na vyeo na mdaraka wanayopewa bado wanaendeshwa endeshwa na wanasiasa. Na usomi wao wanatumiwa kama ruber stamp na wajanja wachache . Sasa sijui kwa kauli kama hizi za feleshi si ajabu tuna vihiyo wengi.
 
Back
Top Bottom