Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Hapana, nadhani anaogopa kivuli cha bosiFeleshi anaogfopa kivuli chake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana, nadhani anaogopa kivuli cha bosiFeleshi anaogfopa kivuli chake
Wana JF,Mambo mengine!! Hapa huyu DPP hakuwa na cha kusema, akaamua kusema chochote! Maneno kama haya, ni afadhali asingeongea tu kwa sababu inazidisha suspicion ya umma kwa viongozi wakuu.
Watu wanajua Kagoda ni nani kwani yameshaandikwa sana. Sasa unaposema hashitakiki kwa kuwa alitumwa, unazidi kuwachongea tuu. Mi naona afadhali angekaa kimya tu kuliko kuongea hicho alichoongea.
Sijui kama haya yana msaidia yeye au mkuu wake au nani!!! We are still too poor on the art of talking!
Wana JF,
Kwanza naomba radhi kwa kupotea kwa siku kadhaa. Tangu nimeenda Biharamulo sikuwa hewani na sababu za msingi zinajulikana. Umeme Biharamulo unagawanywa kati ya Biharamulo na Chato, na ni muda mchache sana unapatikana, hivyo ilikuwa vigumu sana kuwa kwenye mtandao.
Pili, Kuhusu Kagoda, Feleshi aseme asiseme, KAGODA tutaendelea kuipigia kelele hadi kieleweke. FELESHI ajiandae tu huko tuendake. Nashukuru kuwa sasa amefikia hatua ya kukiri kuwa walioenda "kubeba" au "kuchukua" walitumwa. Hii ni hatua nzuri, tuendelee kupiga kelele. Siyo kuchukua tu, i) Brella ilisajili KAGODA 29 September, 205, lazima wawaambie Watanzania hao waliosajili ni kina nani na wana back ground gani katika Biashara. 2) Ardhi lazima watuambie Plot ya Kipawa ilipo ofisi hiyo ni ya nani? Je aliyeenda kuchukua fedha katika matawi 6 ya CRDB kwa siku mmoja ni huyo huyo aliyesajiliwa au ni nani? Dr. Kimei lazima atuambie huyo aliyechukua fedha hizo ni nani wakati Benki za nje ikiwemo Kenya Commercial Bank iliandikia BOT kuwa Kagoda haijulikani hivyo kuwakatalia kuchukua fedha hizo kupitia Benki yao.
Watanzania wavute subira, wawe wavumilivu lakini Uzi ni ule ule. Utadanganya umma kwa muda na hutaweza kuwadanganya muda wote, ndio usemi unavyoenda. Hivyo tukiendelea kudai, kushikamana katika kudai haki zetu tutafika. Kazi ya kudai si lelemama, lakini hatimaye tutafurahia matunda.
Wanasheria mnisaidie; fedha za EPA kupitia kagoda zimeibiwa Benki Kuu (BOT). Kisai cha Tsh. 40bil zimeibiwa kwa staili ya kuforgi nyaraka. DPP anasema walikuwa wanazichukua hizo fedha wanajulikana ila hawezi kuwashtaki eti walitumwa tu. Sasa anatafuta waliowatuma.
(a) amejuaje kwamba hao jamaa walitumwa?
(b) kama walitumwa si watakuwa wamewataja mabossi wao?
(c) fedha nyingi kiasi hicho si unaweza ku-trace kwa kuangalia bank transactions na kuzifuatilia akaunti husika?
(d) kama aliyewatuma ni Rais, au CCM, DPP atachukua hatua gani? atawaachia hao jamaa anaodai walitumwa?
Halafu bila aibu Kikwete anasema fisadi Rostam kasingiziwa!
Halafu bila aibu Kikwete anasema fisadi Rostam kasingiziwa!
Kwa wana JF,yeyote aliyena ukaribu na muungwana tafadhali ampelekee ujumbe huu;
Mpendwa Rais wangu Jakaya, nakuomba sana usitumie muda wako mwingi kumsikiliza Salva na wapambe wengine waliokuzunguka kukuhabarisha nini kinaendelea nchini mwako kwani wanakuzuga tuu na kukupotosha. Tafadhali jaribu kutumia saa moja tuu kila siku kutembelea Jamiiforums uhabarishwe yale ambayo hao wapambe hawakuambii kwa faida zao. Ninahakika utafumbuka macho na kuokoka kwa kuchukua hatua maana hujachelewa sana ila una muda mfupi vinginevyo utaondoka na fedheha kinyume na sifa uliyoingilia.
Yaani Kikwete anachezea akili zetu haswaaaaaaaaaa. Anatuona kama mabwege vile, halafu bado watu wanampigia kura, mimi siwaelewi kabisa. Na watu wa Igunga nao sijuwi kawalisha nini huyu jangili mpaka wamchague kuwa mbuge wao.
Akawaambia wananzega, "RA ni mtu safi, anawapenda, anawajali, lakini pia kaenea kila nyanja kama timu ya mpira" watu wakapiga makofi. Hivi kwa mwendo huu Kikwete kweli ana nia ya dhati ya kupambana na mafisadi? kweli anatufaa jamani?
18
COMPANY NAME: Meregesi Law Chambers
Shareholders and Directors: Johnson Lukaza and Maregesi
Related Company: Proin Properties/Kernel
Office Location: Plot 73 Kinondoni Road
Residence Address: ?
Hivi Johnson Lukaza ni mwanasheria?
Sheria asomee wapi?
Kabla ya bumu la EPA mshikaji alikuwa mfanyabiashara ndogo ndogo, alishawahi kuwa na internet cafee huko masaki na alikuwa anaagiza magari mawili matatu hivi toka dubai anauza.
Baada ya EPA kumwagia, mshikaji alikuja juu si kawaida, Advertizer yake ya kwanza ni kwenda na mshikaji wake wa karibu kucheki game ya ufunguzi world CUP ujerumani, Kuagiza Vogue kwa Ndege na kununua majumba kibao.
Halafu mkumbuke huu wizi ni mdogo SANA. Yani ni wizi wa kipindi cha 2005/2006, tukichokonoa zaidi yanaweza kuibuka makubwa zaidi. Huo ni mwaka mmoja tu...
Kuna tetesi na mwaka huu 2010 wamechota teka kutoka serikalini!