Kagoda wamerudisha fedha, bado mnataka kuwajua?

Kagoda wamerudisha fedha, bado mnataka kuwajua?

Tumechoka na tume, tume ya ukweli na upatanisho iundwe na nani? ukweli na upatanisho pekee utakaoeleweka ni watu kuenda jela na fedha kurudishwa.

that is not option; unless mumfunge jela Rais wa CCM. That won't happen either. Somehow we have to bring these scandals to some sort of an ending. The legal system itahitimisha baadhi yake tu, lazima tufikirie njia nyingine.
 
If you say it is not an option you kill the possibility of that being an option, at least from your worldview.

If you entertain that it is possible it may very well turn out to be possible.

Gandhi hakuuangusha utawala wa muingereza kwa kusema "that is not an option" ali organize na kufanya kazi na wenzake.

Granted, the task is Herculean, but not necessarily Sysiphean.

We are about as organized as Gandhi (maybe a bit less) before 47 and Rostam and company are not as powerful as The British Empire (translate this picture to scale)

If Gandhi did it (without the internet nevertheless), we have no excuse.
 
that is not option; unless mumfunge jela Rais wa CCM. That won't happen either. Somehow we have to bring these scandals to some sort of an ending. The legal system itahitimisha baadhi yake tu, lazima tufikirie njia nyingine.

kama wamerudisha kweli, na kama mazito kiasi ambacho hata vyombo vikuu tunavyoviamini vinashindwa vianzie wapi, basi na tuyaache,hila tuakikishe japo baadhi ya wahusika hawarudi kwenye system! nguvu ya kura!kuwafunga hatuwawezi basi tusiwape kura zetu,kuamasisha amashisha mpaka kitaeleweka, kwenye familia yako ukipata watu watano tu watakao kuelewa na hao watano kila mtu akapata wa kwake mmoja mmoja, itakuwa haba na haba!
 
Kiini macho kingine ni kuambiwa kuwa fedha zinapelekwa kwenye kilimo. Huo ni uongo wa mchana kweupe, wanajua huko ndio sehemu pekee ambayo effect ya hiyo fedha hakuna atakayeiona.
Binafsi naona kitu cha muhimu si fedha kurudi, kwani ni vigumu kuthibitisha hilo, kwa sababu hawakwenda kuinvest bali walihonga wananchi ili wapate kura, kwa hiyo leo kusema wamerudisha, labda kama wametengeneza bomu sehemu nyingine. Kitu cha muhimu ni kuweka nidhamu na maadili ya uongozi katika nchi si kwa leo tu, bali hata mtoto mdogo akisikia historia ajue kuwa hakuna anayeweza kuiba and get away with it, hata kama yeye ni mkuu wa nchi. Ifike mahali kila mtz awe chini ya sheria, sio sheria zetu zinazobagua wakushughulikiwa. Nchi hii inaendelea kushuhudia kuwa anayeweza kushughulikiwa ni mtu masikini tu. Potelea mbali hizo fedha, tunataka wahusika waonje mkono wa sheria ili kuweka nidhamu katika nchi hii. Nadhani ni wakati mwafaka kwa JK mwenyewe kujitoa mhanga kwa faida ya muda mrefu ya nchi hii, hata kama anahusika aseme, ataenda jela miaka sio mingi sana, lakini atakuwa shujaa, afterall kuna wengine wapo gerezani wala hawakufanya kosa lolote!!
 
Mwanakijiji,

..WOW!! fedha za Kagoda zilitumika kuwahonga wakulima wakati wa uchaguzi. sasa hivi "wamerudisha" halafu zinapelekwa tena kusaidia kilimo/wakulima!! only in Tanzania!!
 
...hakuna seriousness yeyote kwenye leadership ya kikwete,yaani ni bla blah blah kila kitu na kila siku,hawana idea wanafanya nini hawa na sometimes unasema may be ni incompetency tuu lakini ukiangalia jinsi wanavyoshinda chaguzi unajua ni mafia watupu....eti pesa zimerudishwa na zitapelekwa kwenye kilimo na wengine eti umeme ukikatika tusilaumiane bila kusahau eti nina majina yenu na nitayapeleka kwa bosi wenu,yaani ni matapeli matupu mpaka yanatia hasira
 
that is not option; unless mumfunge jela Rais wa CCM. That won't happen either. Somehow we have to bring these scandals to some sort of an ending. The legal system itahitimisha baadhi yake tu, lazima tufikirie njia nyingine.

Tell me your just kidding......

Do you want us to believe that a bank robber is innocent simply by returning whatever money (& other properties) he has stolen from a bank?

This is nonsense. And I don't know the motive behind your post.......
 
Mwanakijiji utafanya watu waamini uko kwenye payroll fulani sasa.
 
Ni lazima tutafute njia ya kumaliza hii mijadala ya kashfa pamoja na kashfa zenyewe.

Baada ya Afrika Kusini kuingia kwenye utawala wa demokrasia ya kweli waliamua kuunda tume ya Ukweli na Maridhiano chini ya Askofu Mkuu D. Tutu. Ilikuwa ina lengo la kutafuta ukweli wa wote yaliyofanyika chini ya utawala wa kikaburu na kufunua yale ambayo yalikuwa yako kama tetesi. Tume ile ilikuwa na nguvu ya kutoa msamaha au kuagiza hatua zaidi kuchulikuwa. Matokeo yake tunayajua. Ni mwanzo wa uponyaji wa taifa la Afrika ya Kusini.

Rwanda baada ya mauaji ya 1994 wamekaa chini na kuanzisha mfumo wao wa haki za jadi (GACACA) ili kuweza kushughulikia kesi na madai mbalimbali lakini ndani yake ni nafasi ya kupata ukweli, kuomba msamaha, kukubali kuwajibika na hatua za kisheria.

Kenya baada ya mauaji yaliyofuatia uchaguzi wao wa mwaka mmoja tu hivi uliopita wamejikuta wakilazimika kuunda na wenyewe tume ya ukweli na mapatano. Mtindo ni huo huo hata sehemu mbalimbali nyingine duniani. Kumefanyika hizi tume za Ukweli na Maridhiano sehemu mbalimbali duniani kama jinsi ya kumaliza masuala muhimu ya kitaifa ambayo yana maumivu, uhalifu, hisia, na machungu mengi. Kuanzia Marekani, Canada, Chile, Liberia, Argentina, Sierra Leone n.k tume hizi zimekuwa na umuhimu mkubwa sana.

Kwanini Tanzania tusifikiri tume yetu ya Ukweli na Maridhiano iundwe?
 
Uta note kila sehemu unaanza kwa kusema "baada ya ..."

Sisi hatujafikia katika hiyo "baada" bado.

Ni kama vile unataka tume ya Ukweli na maridhiano in the middle of ubaguzi wa rangi South Africa, au kuanzisha community based justice kabla ya kumaliza genocide etc.Utaona kwamba nchi zote hizi zilimaliza tatizo la msingi kwanza kabla ya kurukia hizi tume, South Africa walimaliza apartheid, Mandela akawa rais ndiyo akaleta Tume ya Tutu. Huko Rwanda genocide iliisha, watu wakashitakiwa Arusha, ikaonekana kuna haja ya kuleta "justice by the grass"

Sasa kama hujakata mzizi wa fitina unakimbilia usuluhishi kuna watu wataona wameonewa (as a matter of fact hata ukimaliza issue kwa kukata mzizi wa fitina huwa kuna wengine wanaona si sawa, sembuse usipomaliza?) kwa hiyo unless unafunga watu jela au kupata "closure" inayokubalika na pande zote, utakuwa unapalilia matatizo tu.

Ndiyo maana utawala wa sasa hauna balls za kufanya lolote unabaki kupiga danadana tu, unajua kufunga watu hauwezi na kuwa absolve itakuwa too much.

Hii scandal kwa Kikwete ni kama vita ya Iraq kwa Bush, hana njia ya kutokea na ikibidi anaweza kumuachia rais afuataye, au kwa sababu watanzania hawana ufuatiliaji (although this is changing nowadays) mpira huu utapigwa dana dana na alfu lela ulela mpaka tume ya uchunguzi itaundiwa tume ya uchunguzi, Mwakyembe aliyechunguza Dowans na kumtoa Lowassa naye ataundiwa tume ya kumchunguza na hao walio katika hiyo tume nao wataundiwa tume basi itakuwa kama an endless Russian doll, mpaka mwisho wa siku tutakuwa tunaunda tume bila kujua kiini ni nini.

ndiyo fate ya huu mchezo.
 
Uamuzi ni kama tuko tayari kuendelea kukesha kwenye hizi kashfa miaka nenda rudi au tufike mahali tuseme haya tuyamalize. Sasa tume tutakayoiunda ni lazime isiwe kama tume nyingine, itakuwa ni tume ya "Ukweli na Haki" (Truth and Justice). Itatungiwa sheria, iwe na nguvu ya kuadhibu, na kutoa msamaha, na vile vile kutoa kinga na kupendekeza hatua zaidi za kisheria kulingana na uzito wa makosa. Lengo lake ni kuhakikisha kuwa kesi zote kubwa za kifisadi zinafikia kikomo.
 
Hapa tunachohitaji ni regime change, kuunda tume itakayotoa haki kwenye hili ni sawa sawa na kutaka kuli uproot mansion kutoka ndani yake, bila vifaa.

Au kutaka ku uninstall MS Windows na ku format hard drive kutoka ukiwa logged on, bila kutumia CD au any auxilliary agent.

Huwezi kuwafanya kina Kikwete wajipe msamaha au kutoa haki, hawawezi kufanya neither with integrity.Labda kama unataka kufanya "kubali yaishe" which is basically saying "this issue is lagging too long, lets forget about it and move on".This is admitting that you have given up without solving the issue, and mafisadi wameshinda na watarudia game siku yoyote.Kwangu mimi ni bora kuwe na wingu la uncertainty itakayowafanya mafisadi waogope kuiba tena kuliko kuwa na closure itakayowapa vichwa.

Unahitaji kuwatoa kwanza, uweke mtu mwenye integrity, halafu ndio tutaendelea na mengine.
 
Ni lazima tutafute njia ya kumaliza hii mijadala ya kashfa pamoja na kashfa zenyewe.

Baada ya Afrika Kusini kuingia kwenye utawala wa demokrasia ya kweli waliamua kuunda tume ya Ukweli na Maridhiano chini ya Askofu Mkuu D. Tutu. Ilikuwa ina lengo la kutafuta ukweli wa wote yaliyofanyika chini ya utawala wa kikaburu na kufunua yale ambayo yalikuwa yako kama tetesi. Tume ile ilikuwa na nguvu ya kutoa msamaha au kuagiza hatua zaidi kuchulikuwa. Matokeo yake tunayajua. Ni mwanzo wa uponyaji wa taifa la Afrika ya Kusini.

Rwanda baada ya mauaji ya 1994 wamekaa chini na kuanzisha mfumo wao wa haki za jadi (GACACA) ili kuweza kushughulikia kesi na madai mbalimbali lakini ndani yake ni nafasi ya kupata ukweli, kuomba msamaha, kukubali kuwajibika na hatua za kisheria.

Kenya baada ya mauaji yaliyofuatia uchaguzi wao wa mwaka mmoja tu hivi uliopita wamejikuta wakilazimika kuunda na wenyewe tume ya ukweli na mapatano. Mtindo ni huo huo hata sehemu mbalimbali nyingine duniani. Kumefanyika hizi tume za Ukweli na Maridhiano sehemu mbalimbali duniani kama jinsi ya kumaliza masuala muhimu ya kitaifa ambayo yana maumivu, uhalifu, hisia, na machungu mengi. Kuanzia Marekani, Canada, Chile, Liberia, Argentina, Sierra Leone n.k tume hizi zimekuwa na umuhimu mkubwa sana.

Kwanini Tanzania tusifikiri tume yetu ya Ukweli na Maridhiano iundwe?

Mkuu,

Tanzania tunaunda tume ya nini? Kuridhiana nini? Mimi ninavyojua tume inaundwa kuleta maridhiano kwenye jamii. Sasa hapa kwetu tuna ugomvi na watawala na si kati ya wananchi wenyewe. Watawala na wabia wao wameshirikiana kutuibia na mbaya zaidi wamekomba hadi mboga. Kwa hiyo hapa hakuna uhalali wa kuunda tume unayoshauri. Kama tungekuwa tunachapana, ama kwa makabila yetu au kwa rangi za bendera zetu basi watu wenye akili na busara tungependekeza tume ya ukweli na maridhiano ili ugomvi katika jamii uishe.

Halafu kati ya mifano uliyoitoa sikuona mahali ambapo iliundwa tume ya maridhiano kutatua matatizo kati ya watalawa na watawaliwa. Hapa dawa yake ni moja. Wenye madaraka yao kuyachukua na kuwapa watu wengine ambao wanaweza kuyatumia kwa manufaa yao. Hilo ndilo tatizo kubwa hapa kwetu Bongo. Watu tumeibiwa na kila kitu kiko wazi, lakini tunaendelea kuficha mkia matakoni kama mbwa koko. Siku tukimalizana na hilo tatizo ndio tume yetu itakuwa imeanza kazi. Na hakika hakuna atakayepona baada ya wajinga kuamka. Kwa hiyo suluhu ya hizi kashfa zote ni kusubiri wananchi waamke ili watoe hukumu isiyokatiwa rufaa hata mbinguni. Wataamka lini na wataamshwa na nani ndiyo kazi tunayotakiwa kuongelea.
 
Hapa tunachohitaji ni regime change, kuunda tume itakayotoa haki kwenye hili ni sawa sawa na kutaka kuli uproot mansion kutoka ndani yake, bila vifaa.

Regime change ni njozi nzuri, haitimiliki sasa. Kuna vitu ambavyo tunaviweza sasa na hili naamini linawezekana sasa. Ideally, nakubaliana na wewe kabisa lakini realistically we have to do something now kuliko kuombea mvua jangwani.

Huwezi kuwafanya kina Kikwete wajipe msamaha au kutoa haki, hawawezi kufanya neither.

Sijasema composition ya hiyo tume iweje. Sidhani kama Kikwete akisikia the full proposal ataipenda tume pia.

Unahitaji kuwatoa kwanza, uweke mtu mwenye integrity, halafu ndio tutaendelea na mengine.

utawatoa vipi na utamweka vipi na kutoka wapi huyu mtu 'mwenye intergrity'?
 
Na hakika hakuna atakayepona baada ya wajinga kuamka. Kwa hiyo suluhu ya hizi kashfa zote ni kusubiri wananchi waamke ili watoe hukumu isiyokatiwa rufaa hata mbinguni. Wataamka lini na wataamshwa na nani ndiyo kazi tunayotakiwa kuongelea.

Unaona dalili zozote za kuamka? na Watanzania wana muda gani wa kusubiri waamshwe!?
 
Unaona dalili zozote za kuamka? na Watanzania wana muda gani wa kusubiri waamshwe!?

Mkuu hapo ndiyo kwenye utamu. Kwa sababu kama hawataamka hata hiyo tume haitasaidia kitu. Tutamaliza EPA, watachukua mamilioni toka mfuko wa barabara n.k. Kwa hiyo kazi yetu itakuwa ni kuunda tume kati yetu na watu tuliowakabidhi mali zetu watulindie kwa ujira. Mimi naona mjandala sasa ungehamia kwenye hilo la kuwaamsha wenye nchi. Mfano mzuri ni hiyo model uliyotumia ya Cheche za fikira pia hata hii JF. Kwa hiyo tuanze kuangalia ni jinsi gani tunaweza kuwafikia wale waliko Kakonko, Mnyuzi, Tewe, Ishozi, Pwaga, Mbaba Bay n.k
 
Regime change ni njozi nzuri, haitimiliki sasa. Kuna vitu ambavyo tunaviweza sasa na hili naamini linawezekana sasa. Ideally, nakubaliana na wewe kabisa lakini realistically we have to do something now kuliko kuombea mvua jangwani.

Sijasema composition ya hiyo tume iweje. Sidhani kama Kikwete akisikia the full proposal ataipenda tume pia.

utawatoa vipi na utamweka vipi na kutoka wapi huyu mtu 'mwenye intergrity'?

MKJJ nadhani kama unavyodhani kuwa ni vigumu kwa regime change ndivyo basi itakavyokuwa ngumu zaidi kuwa na tume ya maridhiano. Hayo maridhiano unayosema muuondo wake ndio huo umekuwa ukizuia mabadiliko ya kweli Tanzania. Mimi ninachokiona ni kuwa Tanzania hatujapata viongozi wa kuendesha harakati za kubadilisha hali ya mambo. Tunahitaji sasa kama taifa kuanza mbio za kuishinikiza serikali ichukue hatua na kuwawajibisha wote, hata kwa kulala barabarani nk. Hatuwezi kuwa tunaelewa na taarifa zote ziko wazi lakini hatuchukui hatua, haya ni makosa makubwa, taarifa zote za wote wanaohusika zipo, lakini hakuna anae jali, hiyo tume itakuwa ya nini kama hakuna anaeona yote haya? Sioni kabisa hiyo tume itakuwa ya kumsuluhisha nani.
Tume zimeundwa nyingi, ikiwepo hata ya ccm na cuf ambazo baadae hazikuleta matunda yoyote, mimi naona watu waendelee tu kama ilivyo kupigana hivi hivi na chuki ya wananchi itakapokuwa basi watakuwa na haja ya kudai nao watawala wataona, lakini watakuwa wamechelewa!

Mimi wakati mwingine nafikiri kuwa watanzania walinyimwa elimu ii waweze kutawaliwa, ndio! sasa tuseme je? wote si ndio waliojimilikisha rasilimali zote za nchi?
 
Regime change ni njozi nzuri, haitimiliki sasa. Kuna vitu ambavyo tunaviweza sasa na hili naamini linawezekana sasa. Ideally, nakubaliana na wewe kabisa lakini realistically we have to do something now kuliko kuombea mvua jangwani.

Tatizo siyo kwamba ndoto haitimiliki, watu wamepeleka mtu mwezini itakuwa kuiondoa CCM katika nchi yenye umasikini kama Tanzania? Tatizo strategy hamna, hamna upinzani, watu hawajaelimika, umasikini umetawala mpaka inatisha, hata alternative ya kuchukua nchi hamna, haya ndiyo matatizo.kwa hiyo lets focus kujenga a strong opposition CCM inatusaidia yenyewe kujiengua, otherwise tunacheza kama unavyosema.Lakini I would rather advance slowly than give up.

utawatoa vipi na utamweka vipi na kutoka wapi huyu mtu 'mwenye intergrity'?

Kikwete anatolewa na ethical propaganda zitakazowafungua watu macho.Wapinzani wana mpango gani wa kuanzisha vituo vya televisheni vya kanda na kuonyesha TV bure kwenye public places? Vipi kuhusu vijarida? Vipi kuhusu kufanya a permanent campaign ambayo ina lengo la kuzidisha wanachama na wapiganaji wake vijijini? Vipi kuhusu kuwa na uongozi unao inspire watu? Vipi kuhusu kusambaza kanda za hotuba? Wapinzani wetu wanafanya yote wanayotakiwa? Vipi move ya kubadili katiba na kuwa na tume huru ya uchaguzi, sisikii kitu.Kuna mengi sana ya kuvalia njuga ambayo hayajafanywa kiasi siamini mtu akisema "regime change is out of the question" tatizo letu tuko softies, hatujui guerilla warfare, tumepewa uhuru on a silver platter, kutoka hapo tumekuwa bulldozed literally na Nyerere na hatukusema kitu.Too weak to act, too docile to protest, too quick to proclaim we can't.

Watu wenye integrity wapo kibao Tanzania, wameshikwa na the Socratic curse, those who are able and of the right integrity to run this country, seeing the political machinations required to engage in this reality TV show like drama, choose not to, those who choose to dive in it lack the necessary integrity and competence.Lakini wako no names kibao middle level bureaucrats wana toil kila siku, huwasikii hata kupewa credit.

Ndiyo maana Eda Sanga alipomuuliza Nyerere (paraphrasing) "Mwalimu, mbona sifa ulizozitaja mtu huyo Tanzania kama hayupo" Nyerere alimwambia katika nchi ya watu almost milioni 40 kusema mtu huyu hayupo ni matusi.Nyerere angeweza kusema "katika NEC...." AU "Katika uongozi wa CCM...." lakini hakusema hivyo, alisema "katika nchi ya almost 40 million people..."
 
MKJJ nadhani kama unavyodhani kuwa ni vigumu kwa regime change ndivyo basi itakavyokuwa ngumu zaidi kuwa na tume ya maridhiano. Hayo maridhiano unayosema muuondo wake ndio huo umekuwa ukizuia mabadiliko ya kweli Tanzania. Mimi ninachokiona ni kuwa Tanzania hatujapata viongozi wa kuendesha harakati za kubadilisha hali ya mambo. Tunahitaji sasa kama taifa kuanza mbio za kuishinikiza serikali ichukue hatua na kuwawajibisha wote, hata kwa kulala barabarani nk. Hatuwezi kuwa tunaelewa na taarifa zote ziko wazi lakini hatuchukui hatua, haya ni makosa makubwa, taarifa zote za wote wanaohusika zipo, lakini hakuna anae jali, hiyo tume itakuwa ya nini kama hakuna anaeona yote haya? Sioni kabisa hiyo tume itakuwa ya kumsuluhisha nani.
Tume zimeundwa nyingi, ikiwepo hata ya ccm na cuf ambazo baadae hazikuleta matunda yoyote, mimi naona watu waendelee tu kama ilivyo kupigana hivi hivi na chuki ya wananchi itakapokuwa basi watakuwa na haja ya kudai nao watawala wataona, lakini watakuwa wamechelewa!

Mimi wakati mwingine nafikiri kuwa watanzania walinyimwa elimu ii waweze kutawaliwa, ndio! sasa tuseme je? wote si ndio waliojimilikisha rasilimali zote za nchi?

Mkuu hakuna kupigana kwa aina yoyote hapa. Sana sana utasikia wanaopigana ni wakulima na wafugaji au huko Tarime. Na ukifuatilia utakuta mapigano hayo yanasababishwa na huo ufisadi. Hapa bwana inabidi kupigana hasa! Na kama ingekuwa hivyo hawa akina RA wasingekuwa wanatamba mitaani. Ila naamini ipo siku. Kwa mtu anayefuatilia vizuri ataona kwamba kuna mabadiliko makubwa sana ya kifikra na mtazamo wa baadhi ya watu yaliyotokea kati ya mwaka 1992 tulipoanza mfumo feki wa vyama vingi na sasa. Kazi iliyobaki naamini haitachukua miaka mingikiasi hicho. Pamoja na shida na njaa vinavyosabibishwa na hii serikali ya kifisadi, muda utafika watakiona cha mtema kuni.
 
Back
Top Bottom