Kagoda wamerudisha fedha, bado mnataka kuwajua?

Kagoda wamerudisha fedha, bado mnataka kuwajua?

- Uamuzi wa kurudisha pesa zilizoibiwa uliamuliwa na wanasiasa wetu kutokana na kuelewa mazingara magumu ya kupatikana haki kwenye mahakama zetu, kwa kuzingatia kwamba walioiba walikuwa na pesa nyingi sana za kuweza kuhonga ili kuachiwa na sheria, ingebidi serikali iwakamate wote kwa mara moja na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, wangehonga na wote kuachiwa huru,

- Kuepuka hili ikaamuliwa wapewe muda wa kurudisha, hiki sio kitu cha kujivunia kwa serikali na binafsi nina tatizo na this idea kwa sababu ni kui-encourage wezi kuendelea kuiba, lakini pia ninajaribu ku-struggle na the whole idea ambayo ni samba samba na mazingara yetu. Kunahela zilizorudishwa kwa taifa regardless of what is being said here kwa sababu sometimes ndio political correctness na kukubalika hapa JF yaani kukataa tu ukweli.

- Is this all what our government ingeweza kufanya, no! Je rais aache shuguli za kuendesha taifa na kushinda mahakamani kuhakikisha sheria inafuatwa, hapana! sasa what do we do na ishus kama hizi, I do not know!, lakini as much as viongozi wetu wana matatizo, na sisi wananchi huenda tunachangia sana haya matatizo kwa sababu rais wa jamhuri hawezi kwenda kwenye mahakama zetu kusimamia sheria, wala kufanya uchunguzi wa crimes against taifa letu, wakuu wa sheria na dola wamebadilishwa wee lakini wapi hakuna hope,

- Ssasa wa kulaumu hapa ni nani hasa viongozi wetu tu? sisi wananchi tu? Au wote yaani viongozi wetu na sisi wananchi pia?


- Kama kawaida yetu huwa tunatoa alternative ideas, au mawazo mbadala katika kujaribu kutafuta jawabu ya matatizo ya taifa letu, ingawa sio popular political stand lakini somebody has to do it na sio siri kwamba most of the times it has to be me, WHY ME? Kwa sababu hatupendi majibu rahisi rahisi on serious ishus, hasa tukizingatia mazingara yetu ya kisiasa na kisheria Tanzania.

Mungu Aibariki Tanzania.

Wazee wa sauti ya umeme FMES!
 
Kusema haiwezekani kuiondoa CCM ni defeatist attitude, sababu pekee ya kutufanya tusiweze kuwaondoa CCM ni kwa vile hatujajiandaa vilivyo, sio kwa sababu CCM is all that invincible.

Sasa tujiandae vipi? nani atatuongoza? tunahitaji kiongozi au kila mmoja ajifanyie mambo yake kivyake vyake, je tuendelee kuandika na kujenga hoja na kuzungumza kama kawaida yetu. What are the concrete steps we need to take. I'm willing to be part of whatever need to be done. Kiranga, tukufuate utuongoze kuelekea haya mabadiliko?
 
-


- Kama kawaida yetu huwa tunatoa alternative ideas, au mawazo mbadala katika kujaribu kutafuta jawabu ya matatizo ya taifa letu, ingawa sio popular political stand lakini somebody has to do it na sio siri kwamba most of the times it has to be me, WHY ME? Kwa sababu hatupendi majibu rahisi rahisi on serious ishus, hasa tukizingatia mazingara yetu ya kisiasa na kisheria Tanzania.

Ungonjwa wako ni mkubwa sana sidhani kama madaktari wa kawaida wataweza kukutibu njia iliyobaki ni maombi tu.

Wengi humu tunakujua kuwa huna mawazo mbadala yoyote kwani you are the most partisan person kwenye hii forum na unakipenda chama chako kuliko hata mama yako.

Pia tunajua kuwa ni mtu unayependa sifa, kuoneka kuwa wewe ndiyo mwenyewe na mara kwa mara umejisahau humu na kujiexpose vibaya hiyo tabia yako siku nikipata muda nitapitia thread na kuweka masifa yako peupe nikikunukuu kwa mfano eti "mimi najuana na viongozi wengi Tanzania", "nilikuwa nyumabani kwa mama Migiro sijui kafanya nini!" yote hiyo ni misifa tu

Na leo unaendelea kujisifia sijui una matatizo gani wewe

By the way je una uhusiano na huyo dingi mwanachama mpya anayejiita siju W Malecela naona mna fit sana ideas?
 
Mbona kwenye kilimo wanasema haijaingia hata senti tano zimekwenda wapi?
 
Mkuu MKJJ,

Kagoda ni brainchild ya CCM. Ilikua ni plan hatched ndani ya CCM, executed by CCM kwa lengo la ku-further interests za CCM na SABABU PEKEE wananchi tumekuja kujua about Kagoda ni kwasababu source ndani ya CCM ndo ime-leak hizi juicy details. Hii inaashiria kwamba kuna discontent ndani ya CCM na consequently kuibuka kwa makundi/mpasuko. Inaelekea proceeds za hizi scams hazinufaishi wanachama wote. Hii (makundi/mpasuko) uliizungumzia vizuri sana kwenye makala yako ya Tz Daima. Latest indicator ya huu mpasuko ni malumbano kati ya Mwakyembe na Rostam.

Despite the theatrics za kujifanya wanachukuliana hatua, at this rate wao wenyewe CCM ndo watatuambia Kagoda ni nani na mbinu walizotumia. Already wametajana "indirectly" na watu wana pretty good idea who Kagoda is lakini no one has come forward to convincingly deny the accusations. CCM ndo wameanzisha huu mjadala wa Kagoda na ni wao ndo watakao umaliza. Wengi wetu wananchi ni washabiki tu, kazi kudakia na kushadadia. Lets wait and see/hear. Anytime now.

Downfall.
Nakubaliana nawe kwamba CCM hawawezi kuondolewa madarakani just because most people wish them to go. Ila tena nnachoona ni wao wenyewe watajiondoa madarakani by self destructing. Cases in point ni KANU ya Kenya na ANC ya Africa Kusini. Itafika mahali baadhi ya vinara wa CCM wataunda chama kingine. What is lacking kwa sasa ni strong political cause (eg ukabila, udini, ulalahoi....etc) to rally the ignorant masses around. I hasten to add kwamba kuondoka CCM won't be the end of our problems. Ni ruling elite ileile watabadilisha costumes tu. If anything, the new characters may be worse. Waulize Wakenya.

Ufisadi.
Mimi naona kumaliza hili, kwanza inabidi a concise definition of the term ipatikane. Waweza kuta 98% of our population fall in this category. Pili uhalalishwe (informally). Watanzania wote tukiwa mafisadi it will be a normal thing and thus cease being a problem.
 
By The Way Kuna huu Ugomvi kati ya Rostam na Mwakyembe, Kwa nini Wapinzani Wasicapitalize hapo, nina maana that can be a good Divide ana Conquerkwa Sababu siyo Siri hawawezi kuja open kumsurpot either of the two kwa Sababu:

Mwakyembe hawezi kutoswa sababu ya Suport yake kwa Wananchi CCM wataogopa, vile vile Rostma hawezi kutoswa sababu ya Mambo anayoyajua kuhusiana na CCM.
 
By The Way Kuna huu Ugomvi kati ya Rostam na Mwakyembe, Kwa nini Wapinzani Wasicapitalize hapo, nina maana that can be a good Divide ana Conquerkwa Sababu siyo Siri hawawezi kuja open kumsurpot either of the two kwa Sababu:

Mwakyembe hawezi kutoswa sababu ya Suport yake kwa Wananchi CCM wataogopa, vile vile Rostma hawezi kutoswa sababu ya Mambo anayoyajua kuhusiana na CCM.

Hapana kuna kundi la wabunge kama 16 wa CCM ambao wanaweza kutoswa na CCM isitetereke. Itaonekana kupewa sifa na pongezi. Kundi hilo linaongozwa na vinara saba. Hawa wanapigiwa mahesabu ya jinsi gani watatolewa CCM.

Kundi la wabunge wengine karibu 100 lina nguvu ya fedha, ushawishi, na mizizi katika chama na serikali. Hili haliwezi kuondoka wala kutimuliwa kwani hatima ya CCM inasimama au inaanguka na kundi hili.

Tatizo ninaloliona ni kuwa kundi la wale 16 likimeguka au kutimuliwa litasikitikiwa na wananchi, lakini sioni sababu ya wananchi kuona matumaini kwenye kundi hilo kwani kampeni ya kufumua uchafu wao itakuwa kubwa kuliko ile ya Mrema kuitwa Kichaa na mgonjwa wa akili!
 
mkuu mkjj - nimekusoma lkn naomba nikuulize ww, je, unataka kuniambia JK alivyoruhusu uchunguzi hakujua kama hili halitamgusa??...
 
mkuu mkjj - nimekusoma lkn naomba nikuulize ww, je, unataka kuniambia JK alivyoruhusu uchunguzi hakujua kama hili halitamgusa??...

ukisoma mandate ya ule uchunguzi kwa hakika alihakikisha haurudi kumgeuka.
 
- Uamuzi wa kurudisha pesa zilizoibiwa uliamuliwa na wanasiasa wetu kutokana na kuelewa mazingara magumu ya kupatikana haki kwenye mahakama zetu, kwa kuzingatia kwamba walioiba walikuwa na pesa nyingi sana za kuweza kuhonga ili kuachiwa na sheria, ingebidi serikali iwakamate wote kwa mara moja na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, wangehonga na wote kuachiwa huru,

FMES,

Kusema kwako hivyo kunatoa maana kuwa hakuna mfumo wa haki Tanzania na wote wanaofikishwa hatiani kwa kuiba kuku na tairi la gari, hawana haki yeyote na hawana thamani. Huku ni ukiukaji wa haki za binaadamu na uvunjaji sheria.

Hatuwezi kujenga Taifa lenye kujenga matabaka ya watakaofuata Sheria na watakaopewa upendeleo maalum. Baya zaidi ni ulilosema, Wanasiasa kuelewa mazingira magumu, sasa haya mazingira ni magumu yaliyotokana na udhaifu wa ufuatiliaji wa sheria. sasa Wananchi waendlee kujikanza mikanda na kunyon'gonyea mpaka lini ikiwa wanasiasa wanafanya maamuzi mabovu ambayo yanalitia hasara Taifa letu?

Leo hii tunalazimishana tuwaelewe wanasiasa kwa ugumu wa kazi zao kufunika maovu, je Wananchi wanaohangaika kila siku kutokana na ukosefu wa chakula, madawa, maji safi, matibabu, elimu, ajira na hata bein nzuri za mazao ni nani atakayewatetea ikiwa waliopewa dhamana ya kulinda Katiba na umma wa Watanzania wanachagua na kubagua ni nani wa kuwapa ushirikiano au kuwalinda?

- Kuepuka hili ikaamuliwa wapewe muda wa kurudisha, hiki sio kitu cha kujivunia kwa serikali na binafsi nina tatizo na this idea kwa sababu ni kui-encourage wezi kuendelea kuiba, lakini pia ninajaribu ku-struggle na the whole idea ambayo ni samba samba na mazingara yetu. Kunahela zilizorudishwa kwa taifa regardless of what is being said here kwa sababu sometimes ndio political correctness na kukubalika hapa JF yaani kukataa tu ukweli.

Tunalalamikia kuhusu Tanzania kuwa ubovu katika Utawala bora na Sheria. Chaguzi zetu zinaendeshwa kwa matakwa ya Chama au wanasiasa fulani an si umma wa Watanzania, sasa tutasema ili kuepuka na A, basi wanasiasa wanaamua kupinda sheria na kufanya mambo alimradi B la kisiasa litimie, hatuoni kuwa tunajenga utamaduni mbovu wa wachache wenye kujiamulia mambo kwa manufaa yao na kwa mtazamo wao binafsi na si mtazamo wa jumla wa Taifa?

Ikiwa leo tunamlaani Nyerere kwa vijiji vya ujamaa na siasa mbovu ya ujamaa na hata kumshutumu kwamfumo mbovu wa uongozi na viongoi, iweje tufumbie macho ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Katiba unaofanywa na Wanasiasa kwa kisingizio cha "Political Correctness"?

Karamagi alikwenda London na kubadilisha mkataba kwa ajili ya "Political Correctness", Lowassa alikubali mkataba wa Richmond kwa "Political Correctness", tumenunua Ndege, Rada na kuingia mkataba wa IPTL kwa ajili ya "Political Correctness", mapato yetu ya uwekezaji ni finyu kuliko faidda anayopata mwekezajim kama vile dhahabu, tumeambiwa Dhahabu iliyovunwa mpaka mwka 2007 ilikuwa ya thamani ya US $ 3 billion, Tanzania tulichokipata kama mapato ya kosi n US $1 million ambayo ni 3.3% yote hii ni kutokana na "Political Correctness" je huoni kuwa kuna walakini katika hii mandate ya bure ya "political Correctess" tuliyo waachia Wanasiasa?

- Is this all what our government ingeweza kufanya, no! Je rais aache shuguli za kuendesha taifa na kushinda mahakamani kuhakikisha sheria inafuatwa, hapana! sasa what do we do na ishus kama hizi, I do not know!, lakini as much as viongozi wetu wana matatizo, na sisi wananchi huenda tunachangia sana haya matatizo kwa sababu rais wa jamhuri hawezi kwenda kwenye mahakama zetu kusimamia sheria, wala kufanya uchunguzi wa crimes against taifa letu, wakuu wa sheria na dola wamebadilishwa wee lakini wapi hakuna hope,

Tulipoambiwa Benki Kuu na Richmond kuna hujuma, kwa nini Polisi na Usalama (Dola) havikuachiwa vifanye kazi zao bila kuomba ruhusa Ikulu? Je utakubali kuwa madaraka ya Rais ni makubwa mno na mfumo wa kiutawala na kiutendaji(ambao chama chako cha CCM kinadai hauna matatizo alimradi una manufaa kwa CCM) ni mbovu?

Kwa nini basi wakati Polisi walipovunja Sheria kule Pemba au Mwembechai, ilibidi kibali kitoke Ikulu kwanza ndipo waliohusika wafikishwe kwenye sheria? Je hili la Yona, Mramba na Mgonja, kwa nini ilitakikana idhini ya Rais kuwapeleka mahakamani kama si udhaifu wa mfumo wa utendaji ambao umesababisha Rais awe mwamuzi wa kila kitu?

Kama kweli mfumo huu ambao CCM inauona ni bora kwa manufaa yao leo utatuambia haufai, kwa nini basi CCM iendelee kung'ang'ania kuwa inaridhia mfumo kama huu ambao bni butu na unakidhi maslahi ya Watu Milioni 5 kati ya Milioni 40?

- Ssasa wa kulaumu hapa ni nani hasa viongozi wetu tu? sisi wananchi tu? Au wote yaani viongozi wetu na sisi wananchi pia?

Katika mada ya kusema CCM ni mbovu, umeitetea kwa nguvu sana na kudai ni viongozi na wanachama wachache tuu, ndio wanaoharibu mambo. Naomba nikuulize, kama CCM ina wanachama Milioni 5, halafu kuna wanachama elfu kumi (10000) ambao ndio mafisadi, wahujumu, wavunja sheria na kadhalika ambayo inaashiria ndio wanaoharibu chama na kufanya mambo mrama, je wale wanachama 4,990,000 wako wapi na kwa nini wanakaa mguu pande wasiwaondoe hawa wachache wenye kuharibu jina na sifa ya Chama?
 
1.
Rev. Kishoka;412470]FMES,

Kusema kwako hivyo kunatoa maana kuwa hakuna mfumo wa haki Tanzania na wote wanaofikishwa hatiani kwa kuiba kuku na tairi la gari, hawana haki yeyote na hawana thamani. Huku ni ukiukaji wa haki za binaadamu na uvunjaji sheria. Hatuwezi kujenga Taifa lenye kujenga matabaka ya watakaofuata Sheria na watakaopewa upendeleo maalum. Baya zaidi ni ulilosema, Wanasiasa kuelewa mazingira magumu, sasa haya mazingira ni magumu yaliyotokana na udhaifu wa ufuatiliaji wa sheria. sasa Wananchi waendlee kujikanza mikanda na kunyon'gonyea mpaka lini ikiwa wanasiasa wanafanya maamuzi mabovu ambayo yanalitia hasara Taifa letu? Leo hii tunalazimishana tuwaelewe wanasiasa kwa ugumu wa kazi zao kufunika maovu,

- Kupatikana kwa haki hasa tajiri anapokuwa kwenye upande wa pili wa sheria, siku zote historia ya dunia na sheria inaonyesha kua sio kazi rahisi, unless labda ni China, unapoliona taifa lolote lina matatizo ya kuheshimu sheria kama letu, basi nenda kwenye foundations zake utakuta jawabu. Tatizo la kutokuheshimu sheria hili linatuhusu wananchi wote wa Tanzania na viongozi wote, hatujui sheria na hatuheshimu sheria, matokeo ndio haya unayoyasema maana kuanzia nchini mpaka juu hatuheshimu sheria.

2.
je Wananchi wanaohangaika kila siku kutokana na ukosefu wa chakula, madawa, maji safi, matibabu, elimu, ajira na hata bein nzuri za mazao ni nani atakayewatetea ikiwa waliopewa dhamana ya kulinda Katiba na umma wa Watanzania wanachagua na kubagua ni nani wa kuwapa ushirikiano au kuwalinda?

- Again hili ni tatizo la society, unless tunataka majibu mepesi mepesi ambayo siku zote huishia kua temporary solution, lakini kama tunataka kutafuta permanent ones, then tuanzie na chini kwenye society, kwa sababu hawa viongozi hawakujifunza kuvunja sheria wakiwa uongozini tu, na hawawezi kuvunja sheria kirahisi mbele ya wananchi wanao heshimu sheria, unakumbuka Mtikila alipotishia kumfikisha Marehemu Ditopile, kupinga kuachiwa kwakwe kwa dhamana na ile kesi yake ya mauaji yake ya mchana kweupee! Waumini wa dini ya Marehemu unakumbuka walisema nini? Sasa kwa mazingara haya what do you expect kutoka wka viongozi wetu wa juu?

- Please do not get me wrong, sitetei waovu, lakini I am only being realistic na kuona kwamba this ishu ya uvunjanji sheria na sisi wa-Tanzania ni larger than the way we think, Wa-Tanzania hatupendi sheria kuaniza chini mpaka juu, na siku zote tunapikwepa sheria tunajisifia sana bila kujali kwamba tumeikwepa on who's expense?

- Kwa mfano, nina rafiki yangu wa karibu sana, ambaye amerudi karibuni kutoka nje kama ofisa wa ubalozi wetu mmoja huko, The fella is straight hana uongo, havunji sheria, ni mkweli, hatoi rushwa, sasa amerudi na kontena lenye mali yake, kufika bandarani ameamua kufuata sheria na ukweli, guess what leo ni miezi sita kontena halijatoka, sasa wananchi wengine wanamcheka sana kwamba sisi huwa inachukua siku tatu tu tunatoa vipi wewe nasikia unataka sheria na ukweli? Haya ndio tunayofanyiana huku chini, na kutegema wakubwa wawe tofauti na sisi!


3.
katika Utawala bora na Sheria. Chaguzi zetu zinaendeshwa kwa matakwa ya Chama au wanasiasa fulani an si umma wa Watanzania, sasa tutasema ili kuepuka na A, basi wanasiasa wanaamua kupinda sheria na kufanya mambo alimradi B la kisiasa litimie, hatuoni kuwa tunajenga utamaduni mbovu wa wachache wenye kujiamulia mambo kwa manufaa yao na kwa mtazamo wao binafsi na si mtazamo wa jumla wa Taifa?

- Ya uchaguzi wakulamumiwa sana ni wapinzani pamoja na watawala wetu, ni makosa ya wapinzani waasisi wetu kwa kiasi kikubwa sana, ndiyo tunayalipia sasa, ingawa wananchi pia tunahusika sana na hili kwa sababu ni sisi ndio tunaowawezesha wanasiasa wetu kutuchezea, lakini kuna wananchi kama wa-Tarime, Kigoma, Karatu, na Moshi ambao wanatakwia kutufundisha wengine wote how to be politically objective ndani ya utawala wa CCM. Zamani sawa tulikuwa tunapigia kura mtu na giza, lakini leo kunakuwa na wagombea wengi sasa kwa nini bado tunamchagua Mzindakaya bila kulazimishwa na bunduki? Hili sio kosa la watawala, na jawabu lake haliwezi kuwa lepesi lepesi tu, ni sisi taifa ndio tunawa-afford mafisadi, halafu tunalalamika somebody aje kutoka mbinguni kutusaidia!

- Hebu sasa tubebe responsibility na tujiangalie tumekwama wapi as a nation?


4.
Ikiwa leo tunamlaani Nyerere kwa vijiji vya ujamaa na siasa mbovu ya ujamaa na hata kumshutumu kwamfumo mbovu wa uongozi na viongoi, iweje tufumbie macho ukiukwaji wa Sheria, Kanuni na Katiba unaofanywa na Wanasiasa kwa kisingizio cha "Political Correctness"? Karamagi alikwenda London na kubadilisha mkataba kwa ajili ya "Political Correctness", Lowassa alikubali mkataba wa Richmond kwa "Political Correctness", tumenunua Ndege, Rada na kuingia mkataba wa IPTL kwa ajili ya "Political Correctness", mapato yetu ya uwekezaji ni finyu kuliko faidda anayopata mwekezajim kama vile dhahabu, tumeambiwa Dhahabu iliyovunwa mpaka mwka 2007 ilikuwa ya thamani ya US $ 3 billion, Tanzania tulichokipata kama mapato ya kosi n US $1 million ambayo ni 3.3% yote hii ni kutokana na "Political Correctness" je huoni kuwa kuna walakini katika hii mandate ya bure ya "political Correctess" tuliyo waachia Wanasiasa? Tulipoambiwa Benki Kuu na Richmond kuna hujuma, kwa nini Polisi na Usalama (Dola) havikuachiwa vifanye kazi zao bila kuomba ruhusa Ikulu? Je utakubali kuwa madaraka ya Rais ni makubwa mno na mfumo wa kiutawala na kiutendaji(ambao chama chako cha CCM kinadai hauna matatizo alimradi una manufaa kwa CCM) ni mbovu?

- Strong points, ila ungemuweka Mwalimu pembeni kwa sababu ukianza kumusisha kwa nia ya kumsafisha na mapungufu yetu kiuongozi na la sisi wananchi kuwa mambumbu na elimu ya siasa kwa taifa letu, na kutoheshimu sheria, basi ishu nzima inakosa miguuu na kumrudia tena Mwalimu, I do not want to go there, madaraka ya rais wetu ni kweli hayana mfano, CCM kazi yao kama chama cha siasa ni kushinda uchaguzi at any cost, how they lead ni sisi wananchi ndio tunatakiwa tuwe waamuzi, lakini we are so fast a sleep kwamba tumewaachia CCM kuamua the agenda.

- Ninaheshimu juhudi kubwa inayojaribu kufanyika hapa JF katika kuwaamsha wananchi, lakini ninasema hivi tuwe wakweli na tuwe specific, na tuwe tunaelekea kwenye njia zinazotakiwa kidemokrasia kama kujinunga na vyama vyetu vya siasa, badala ya kuponda kila mtu na vyama vyote kuwa havifai, okay where do we stand yaani kwenye ardhi ipi hiyo?

- Kagoda, nani amehusika kwa sababu sio CCM wote tuliohusika, wapi? Lini? and so on, lakini ohh CCM wote ni wezi wameiba Kagoda, EPA na the rst of the story, hapana tuwe wakweli na tuwe specific, sio kusubiri kwanza mpaka kiongozi wetu Mwakyembe aguswe ndio tuanze kulalama, kwa sababu hapoa tunawaambia mafisadi kwamba next time msipomgusa the Mwakyembe likes mtakuwa salama salimini, that is a wrong message.


5.
Kwa nini basi wakati Polisi walipovunja Sheria kule Pemba au Mwembechai, ilibidi kibali kitoke Ikulu kwanza ndipo waliohusika wafikishwe kwenye sheria? Je hili la Yona, Mramba na Mgonja, kwa nini ilitakikana idhini ya Rais kuwapeleka mahakamani kama si udhaifu wa mfumo wa utendaji ambao umesababisha Rais awe mwamuzi wa kila kitu? Kama kweli mfumo huu ambao CCM inauona ni bora kwa manufaa yao leo utatuambia haufai, kwa nini basi CCM iendelee kung'ang'ania kuwa inaridhia mfumo kama huu ambao bni butu na unakidhi maslahi ya Watu Milioni 5 kati ya Milioni 40?

- Udhaifu wa mfumo unaonwa na sisi watazamaji sio wachezaji mpira wenyewe CCM, katiba yetu ndio inampa rais madaraka ya ajabu, sasa who is to be blamed for that? CCM? I do not think so, kama wananchi na wanaotakiwa kutusimamia kikatiba yaani upinzani wameridhika na kunyamaza kimya, kweli unategemea CCM isimame juu na kujisema kwamba rais wake ana power mno inahitaji kurekebishwa? Majuzi akiwa nje ya mlo Msekwa alikuwa a hero maneno mengi mazito ya kuwakilisha wananchi, sasa mbona amekuwa bubu? Kwenye hili tumeangushwa sana na wapinzani kwa maoni yangu kwa nini wapinzani hawamkumbushi maneno yake?

6.
Katika mada ya kusema CCM ni mbovu, umeitetea kwa nguvu sana na kudai ni viongozi na wanachama wachache tuu, ndio wanaoharibu mambo. Naomba nikuulize, kama CCM ina wanachama Milioni 5, halafu kuna wanachama elfu kumi (10000) ambao ndio mafisadi, wahujumu, wavunja sheria na kadhalika ambayo inaashiria ndio wanaoharibu chama na kufanya mambo mrama, je wale wanachama 4,990,000 wako wapi na kwa nini wanakaa mguu pande wasiwaondoe hawa wachache wenye kuharibu jina na sifa ya Chama?

- Kwa sababu wananchi wengine nje ya hao Millioni tano ambao ni wanachama wa CCM hawaoni tatizo, kuacha wananchi wachache tuliomo humu JF, ambao wengi tuna-claim to be non members wa chama chochote cha siasa Tanzania na sio siri wala sio wapiga kura kwenye uchaguzi muhimu wa taifa letu, sasa tunalisaidiaje taifa na this kind of CV as wananchi wataka mabadiliko kutoka kwa watawala? Otherwise, una hoja nzito sana Mchungaji lakini umezielekeza to the wrong place!

Mungu Aibariki Tanzania na tuendelee kuelimishana.

FMES!
 
Kishoka, FMES,
What bothers me is that it can only happen in Tanzania. We do not follow the rule of law. How do we know the money has been returned? How can we trust a government that first denied the theft and only accepted when the evidence was overwhelming? Why are those who are supposedly returning the money remaining anonymous? Clearly the laws have been broken and someone must be accountable. Yaani mtu kaibia hazina ya taifa, anajulikana kwa serikali lakini serikali inasema rudisha kimya kimya hatutakufanyia kitu eti kwa sababu tunaogopa utahonga mahakama? Inaingia akilini kweli?
 
Kishoka, FMES,
What bothers me is that it can only happen in Tanzania. We do not follow the rule of law. How do we know the money has been returned? How can we trust a government that first denied the theft and only accepted when the evidence was overwhelming? Why are those who are supposedly returning the money remaining anonymous? Clearly the laws have been broken and someone must be accountable. Yaani mtu kaibia hazina ya taifa, anajulikana kwa serikali lakini serikali inasema rudisha kimya kimya hatutakufanyia kitu eti kwa sababu tunaogopa utahonga mahakama? Inaingia akilini kweli?



- Ni kwa sababu historia iko wazi, kwamba viongozi kama Kiula walishinda kesi pamoja na ushahidi wote wa kamati ya Warioba, Matajiri kama Lugakingira walitoroka rumande wakusibiri kesi, Marehemu Ditopile aliachiwa kwa dhamana in some few days pamoja na kwamba mahabusu wengine wenye kesi kama yake wamekuwepo Rumande kwa miaka zaidi ya kumi kusubiri kesi zao bila dhamana, Lowassa mpaka leo tunabishana kama alionewa au ilikuwa sawa,

- Kuepuka haya watawala wakamua wezi wetu warudishe tu hela walizoiba, sad indeed kwa the future of our nation, inasikitisha sana.

FMES
 
................ How do we know the money has been returned? ............

Good Question!

Mkuu Jasusi....kwa kweli ni ngumu sana kujua.........the bottom line now is......the CASE is CLOSED!
 
Jasusi,
Mkuu sometimes inabidi kujichana tu maanake kama haiwezekani basi haiwezekani...kilichobaki labda kujiachia tu, usiweke fedha zako benki,tafuta serengeti baridiii ujiburudishe..

Nikuacheni na kisa hiki..

Dr. Mark Farber the investment guru, concluded his monthly bulletin with the following comments.

Dr. Marc Faber tells it how it is:-

"The federal government is sending each of us a $600 rebate. If we spend that money at Wal-Mart, the money goes to China. If we spend it on gasoline it goes to the Arabs. If we buy a computer, it will go to India. If we purchase fruits and vegetables it will go to Mexico, Honduras and Guatemala. If we purchase a good car, it will go to Germany. If we purchase useless crap, it will go to Taiwan and none of it will help the American economy.
The only way to keep that money here at home is to spend it on prostitutes and beer, since these are the only products still produced in the US.
I've been doing my part....."
 
Which means nothing will ever be resolved until CCM is out, even if it will take us 100 years!

Mkuu, Katiba ya nchi ilivyo sasa ni tamu sana kwa viongozi kiasi kwamba hata CCM ikitolewa madarakani, chama kitakacho tawala hakitaibadilisha. This you can bet.
 
Back
Top Bottom