Mzee,
Uwezi kustua gari lilo-knock Engine. Hapo ndiyo mwisho wake! Kama pato linaruhusu nunua gari nyingine au vipi endelee kutembea kwa miguu mpaka sori za viatu siishe ebo!
Manji alirudisha fedha kwa niabaya "Kagoda" akidai kuwa aliyehusika ni marehemu baba yake. Serikali ikapokea fedha hizo na kuzijumlisha kwenye ile jumla ya Rais.
a. Kama wamerudisha fedha na serikali imekubali kupokea kuna haja ya kujua nani alifanya kosa kweli?
b. Kama serikali imekubali kupokea fedha hizo ina maana imekubali maelezo ya Manji na hivyo "case closed"?
c. Kama fedha zilizochukuliwa kwa kiasi kikubwa ndizo zilizotumika kumuingiza JK madarakani na sasa kazirudisha bado mnataka kumbana?
d. Rostam ndiye aliyehusika na kutumiwa kama alivyohusika kwenye Dowans na kutumiwa kwanini ni nani anaweza kumnyoshea kidole wakati wao wanajua bila yeye wasingeweza kuingia madarakani? NI kweli huwezi kumgusa Rostam bila kugusa karibu nusu ya Wabunge na Rais na huwezi kumuachilia bila kuachikilia kesi kadhaa za kifisadi! So what do you do?
e. Je kwa kujaribu kujifanya wanaichunguza Kagoda wakati tayari wanajua ni nani (ni wao wenyewe!) kwanini wasije tu na kusema mbele ya wananchi kuwa "Kagoda ndiyo sisi! hatukujijua na tumegundua kuwa tulikuwa tumezichota wakati tumelala, lakini tumezirudisha yaishe"!? vinginevyo kwanini wanajifanya kana kwamba hawajui Kagoda ni nani wakati wamepokea fedha kutoka kwake!?
f. Je wananchi wanasababu yoyote ya kujua Kagoda ni hata kama wamesharudisha fedha na fedha zishaliwa? Manake hawawezi kumkamata Manji (aliyerudisha) wala Rostam (aliyechukua kwa kutumia vyombo vyake kwa niaba yake na ya chama chake (hakufanya kama charity work!)
g. Sasa kwanini DPP asije tu na kusema kuwa hili haliwezi (kwani linamgusa Rais moja kwa moja!).
h. Kwanini Wabunge na watu mashuhuri ndani ya CCM au wana CCM hawaandamani kutaka Kagoda ifiikishwe mahakamani na wahusika wote wafikishwe mahakamani kama wanavyoshangilia kina Mramba kufikishwa mahakamani. Je mtu anaweza kuufikisha mkono wake wa kushoto mahakamani bila ye yeye mwenyewe kuwa huko huko mahakamani?
La Kagoda tulimalize vipi baada ya kujua kuwa fedha zimerudishwa, wezi wanajulikana, zilipita wapi inajulikana na zirudi nchini kwa namna gani inajulikana?
well... I was just thinking out loud. Nauliza nilivyowahi kuuliza huko nyuma kwenye hili la Kagoda tukubali yaishe? Au tuendelee kugangamala huku tukijua "haliwaki" hata tulisukume na "kushtua"?
Tatizo siyo kwamba ndoto haitimiliki, watu wamepeleka mtu mwezini itakuwa kuiondoa CCM katika nchi yenye umasikini kama Tanzania? Tatizo strategy hamna, hamna upinzani, watu hawajaelimika, umasikini umetawala mpaka inatisha, hata alternative ya kuchukua nchi hamna, haya ndiyo matatizo.kwa hiyo lets focus kujenga a strong opposition CCM inatusaidia yenyewe kujiengua, otherwise tunacheza kama unavyosema.Lakini I would rather advance slowly than give up.
But strategically. If we decide today, I believe we CAN!
Kikwete anatolewa na ethical propaganda zitakazowafungua watu macho.Wapinzani wana mpango gani wa kuanzisha vituo vya televisheni vya kanda na kuonyesha TV bure kwenye public places? Vipi kuhusu vijarida? Vipi kuhusu kufanya a permanent campaign ambayo ina lengo la kuzidisha wanachama na wapiganaji wake vijijini? Vipi kuhusu kuwa na uongozi unao inspire watu? Vipi kuhusu kusambaza kanda za hotuba? Wapinzani wetu wanafanya yote wanayotakiwa? Vipi move ya kubadili katiba na kuwa na tume huru ya uchaguzi, sisikii kitu.Kuna mengi sana ya kuvalia njuga ambayo hayajafanywa kiasi siamini mtu akisema "regime change is out of the question" tatizo letu tuko softies, hatujui guerilla warfare, tumepewa uhuru on a silver platter, kutoka hapo tumekuwa bulldozed literally na Nyerere na hatukusema kitu.Too weak to act, too docile to protest, too quick to proclaim we can't.
Mbaya zaidi tunasumbuliwa na njaa ya siku moja! Hebu angalia watu kama Lamwai, Kabour, Mtemvu n.k. Hakuna anayefikiria kuwa unaweza kufa masikini lakini ukaacha watanzania wakiwa matajiri. Amini watakuenzi milele. Ila mbaya zaidi ni kwamba tunaendelea kushughulika na mamluki! Juzi nimepata habari za kushtua sana kwamba hata Lipumba ni mzee wa UWT. Kama ni kweli basi kazi ipo!
Jibu ni moja kwa Tanzania kuweza kuendelea na kuwa na mazingira ya demokrasia ya kweli, uwajibikaji, uadilifu na haki yanayoambatana na Utawala bora, Uongozi bora na Siasa safi, nalo ni kuiondoa CCM madarakani.
kama kweli zile hela zilitumika kwenye uchaguzi kuisaidia ccm ishinde basi kuna uwezekano mkubwa wabunge tulionao wengi wa ccm hawakustahili kuwa wabunge. huenda hata jmk hakustahili ushindi wa kishindo
raisi na wabunge wake wanaweza kuona ni vigumu sana kuachia madaraka kwasasa.
lakini lazima waone umuhimu wa kuzuia mambo kama yale kutokea miaka ijayo. hii ifanyike kwa ccm kutuomba msamaha. waseme kiasi cha pesa kilichochukuliwa, kiasi gani kiligharamia nini au mbunge yupi na kiasi gani kilitumika kugharamia ushindi wa raisi.
wakishamiliza watuambie wanafanya nini au wamefanya nini kuhakikisha miaka ijayo watakuwa hawajichukulii hela watakavyo. pia watuambie mipango yao ya kutafuta hela za kugharamia chaguzi zao. wasipokuwa na mipango mizuri na endelevu ya kutafuta hela wataendelea kutuibia
MKJJ naomba ulifikirie hili kwa makini
kama unavyosema hizo hela zimetumika katika kampeni CCM, inamaanisha zimetumika hazikuwekwa benki ili zizae riba.
swali gumu, wamepata wapi hizo hela nyingine za kurudisha?
CCM/manji/ra/kagoda wamepata wapi $30m walizorudisha?
ku raise $30m in TZ sio mchezo?
Nakukatalia hela haijarudishwa zimechukuliwa sehemu moja zikapelekwa kwingine wazungu wanakuambia "creative accounting"
"MKJJ umezungushwa kwenye roundabout ya samora"
mtihani, hela iliyorudishwa imetoka wapi? shimo limeachwa wapi?
maana yake hela yote ilitumika katika kampeni...
mchana mwema....
But strategically. If we decide today, I believe we CAN!
Mbaya zaidi tunasumbuliwa na njaa ya siku moja! Hebu angalia watu kama Lamwai, Kabour, Mtemvu n.k. Hakuna anayefikiria kuwa unaweza kufa masikini lakini ukaacha watanzania wakiwa matajiri. Amini watakuenzi milele. Ila mbaya zaidi ni kwamba tunaendelea kushughulika na mamluki! Juzi nimepata habari za kushtua sana kwamba hata Lipumba ni mzee wa UWT. Kama ni kweli basi kazi ipo!
Haitoshi kunuia na kutamania. Haitoshi kusema CCM iondoke au iondolewe; haitoshi kuombea kuwa CCM ibadilishwe na uje utawala mwingine. Let me do some reality check:
a. Chama kikuu cha upinzani Tanzania hakina Mbunge hata mmoja Tanzania bara licha ya mabilioni ya fedha. Na uchaguzi mdogo wa Geita huko wala msitarajie kupata chochote.
b. Chama kikuu cha upinzani tanzania bara hakina mbunge hata mmoja Tanzania Visiwani na kwa muda kimekuwa na matatizo yake ya ndani.
c. CCM bado inapata wanachama wengi wa kutosha kubadili matokeo yoyote ya uchaguzi. Na wanaendelea kuandikisha wanachama wapya na sitoshangaa tunapoelekea uchaguzi hata baadhi ya waliokuwa upinzani watahama na kurudi CCM! Wapinzani wamepewa miaka miwili ya kupata wanachama wapya hadi leo wameshindwa hata kuanzisha matawi nje ya nchi wakati CCM inaendelea kama kawaida! Wamepewa nafasi tatu za kihistoria za kuingiza wanachama wengi lakini wameshindwa kuzitumia na wamebakia "maslahi ya taifa". Gharama yake ni kushindwa uchaguzi mkuu ujayo may be not to the same extend kama 2005.
d. CCM bado ina miundo mbinu na nyenzo nyingi za kutosha na mitandao yake ya kisiasa ni imara zaidi na mara nyingi zaidi kuliko chama kingine chochote kile.
e. Kuombea kuwa mabadiliko ya kisheria yafanyike, Katiba ibadilishwe ili x, na y yatokea maana yake ni kukiomba chama chenye wabunge wengi zaidi na kilichoshikilia serikali kibadilishe sheria za mchezo ili timu nyingine ishindwe! Ni sawa na kumwambia papa atoe mafuta yake halafu ayaweke kikaangoni huku yeye mwenyewe akifuatia! CCM imejifunza vizuri kutoka Zambia na Kenya na hata Malawi na haitafanya kosa hilo.
f. Bila kashfa upinzani Tanzania unakufa.
Which means nothing will ever be resolved until CCM is out, even if it will take us 100 years!
Mchungaji, if you are a betting man, don't bet on that.. watoto wa watoto wao na wajukukuu wa wajukuu zao watakuwa madarakani na wataendelea kutamani vile vile tunavyotamani sisi.