Kahama: Akamatwa kwa kujiunganishia huduma ya maji

Kahama: Akamatwa kwa kujiunganishia huduma ya maji

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
IKIWA imepita siku kadhaa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama (KUWASA) kukamata mwizi wa huduma ya maji, kwa mara nyingine imemkata mkazi wa mtaa wa Mwime Manispaa ya Kahama Hamisi Omary kwa tuhuma ya kujiunganishia maji kinyemela na kusababisha mamlaka hiyo kukosa mapato.

Akizungumza na NIPASHE DIGITAL Ofisa uhusiano wa Mamlaka hiyo kwenye eneo la tukio John Mkama amesema, vitendo hivyo vimekuwa vikihujumu mamlaka na kusababisha kukosa mapato yake na wahusika wote watawajibishwa kisheria baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Amesema, mteja huyo alijiunganishia huduma hiyo kupitia chooni na bafuni nakwamba maji yote aliyokuwa akitumia yalikuwa hayapiti kwenye mita ya maji ambayo inatumika kusoma kiwango cha maji mteja alichotumia kwa mwezi, huku akiacha bomba la nje kama gelesha ya kuwahadaa wasoma mita wao.

“Baadhi ya wateja wetu wamekuwa sio waminifu na wanasababisha KUWASA kukosa mapato yake, wanajiunganishia maji kwa kuchepusha mfumo(Bypass) kwenye makazi yao, nasisi tutaendelea kupambana nao ili kuhakikisha vitendo hivyo haviendeleo kujitokeza”Amesisitiza Mkama.
 
Hii ishu ya kujiunganishia maji wakifuatilia watafunga wengi...
 
Hii itapita na wengi mbona, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom