Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Makambako STEEL INDUSTRIAL PARK KAZI zinaendelea
1740365210798.jpg
1740365299200.jpg
1740365241477.jpg
1740365457135.jpg
 
UFUNGAJI MGODI WA BUZWAGI HAUTAATHIRI SHUGHULI ZA UCHUMI KAHAMA – DRK. KIRUSWA

Kamati ya Kudumu ya Bunge Yavutiwa na Mpango wa Ufungaji Mgodi

📍 Kahama

Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, amesisitiza kuwa ufungaji wa mgodi wa Buzwagi hautaathiri shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Kahama, kwani mipango madhubuti imewekwa kuhakikisha kuwa eneo hilo linaendelea kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa kupitia miradi mipya ya uwekezaji na maendeleo.

Alisema hayo Februari 16, 2025 Kahama Mkoani Shinyanga wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea eneo la Mgodi wa Buzwagi ambao uko kwenye hatua za kufungwa baada ya kusitisha uzalishaji wa madini ya dhahabu.

Dkt. Kiruswa alibainisha kuwa, mradi wowote unapoanzishwa lazima mwekezaji aonyeshe mpango wa ufungaji mgodi kabla ya kukabidhiwa leseni na kuendeleza maeneo husika ambako moja ya masharti ni pamoja namna ya kuendeleza shughuli za kiuchumi katika jamii zinazozunguka mradi bila kuathiri maendeleo endelevu ya kiuchumi na mzunguko wa fedha.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Kilumbe Ng’enda alieleza jinsi Kamati ilivyovutiwa na mchakato huo wa ufungaji Mgodi wa Buzwagi na kwamba wakazi wa Kahama na Tanzania kwa ujumla.

Mhe. Ng’enda alisisitiza kuwa, maelekezo ya Bunge ni kuhakikisha eneo hilo linabaki kuwa mfano wa uwekezaji wa viwanda hapa nchini kwa manufaa ya kiuchumi kwa jamii na taifa.

Naye, Meneja wa Ufungaji Mgodi wa Barrick Buzwagi, Zonnastral Mumbi, amesema Barrick itaendelea kushirikiana na Serikali wakati wote kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango vya kimataifa na kuwa mfano wa kuigwa kwa kufunga shughuli za mgodi na kuacha eneo lililokuwa mgodi linakuwa na miradi endelevu ya kuwanufaisha Wananchi na taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa, nia ya Kampuni ya Barrick ni kuhakikisha kuwa inaacha urithi mzuri ambao utaendelea kuhudumia jamii kwa muda mrefu baada ya uchimbaji kufikia mwisho katika mgodi huo, kupitia miradi ya kilimo, ufugaji wa kuku na nyuki, chuo cha ufundi na miundombinu mengine ya maji, barabara na uwanja wa ndege wa kahama ambao hivisasa unauw
Kiufupi hakuna maisha tena pale Kahama kumepauka labda wapate wawekezaji wa viwanda hapo Buzwagi industrial park 😁😁
 
RASMI SASA MJI WA NJOMBE NA MAKAMBAKO INAENDA KUUNGANA MAANA KIKWAZO KIKUBWA ILIKUWA NI MSITU WA TANWAT TAYARI ENEO HILO WANAENDA KUJENGA UWANJA MKUBWA WA NDEGE MKOA WA NJOMBE UMEJIPAMBANUA HAYA WAMEANGALIA WAPI NI KATOKATI YA MIJI MIWILI YA NJOMBE NA MAKAMBAKO NDO UWANJA UNAJENGWA HAKIKA HUU UWANJA UTAKUA NA ABIRIA WA KUTOSHA 👇👇👇👇Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akutana na Uongozi wa TANWAT Kujadili Utwaaji wa Ardhi kwa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na uongozi wa Kampuni ya TANWAT, ukiongozwa na Meneja Mkuu wa Misitu, Anther Kiwale, kwa mazungumzo ya kina kuhusu utwaaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanja kipya cha ndege cha mkoa huo. Mazungumzo hayo ni muendelezo wa juhudi za kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa kwa mujibu wa muongozo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa ameagiza wataalamu wanaohusika katika ngazi ya mkoa kwa kushirikiana na uongozi wa TANWAT kufanya tathmini ya fidia kwa haraka ili kampuni hiyo iweze kuachia eneo hilo na kuruhusu hatua za ujenzi wa kiwanja cha ndege kuanza. "Hili ni jambo la msingi kwa maendeleo ya mkoa wetu. Tunahitaji wataalamu wetu kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha fidia inafanyika kwa haki na haraka, na hatimaye TANWAT kuachia eneo kwa ajili ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi," alisema Mhe. Mtaka.

Eneo jipya lililopendekezwa kwa ujenzi wa kiwanja hicho lipo ndani ya shamba la TANWAT, likiwa na urefu wa mita 6200 na upana wa mita 1250. Uamuzi wa kuhamisha eneo la awali umetokana na tathmini iliyobaini kuwa halikutosha kwa mahitaji ya kiwanja cha ndege chenye viwango vinavyotakiwa.

Mkuu wa Mkoa ameweka wazi kuwa mradi huo ni wa kimkakati na utachochea maendeleo ya Njombe kwa kufungua fursa mpya za kiuchumi na biashara kupitia sekta ya usafiri wa anga. Pia ameahidi kushirikiana na wadau wote husika ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unafanyika kwa wakati na kwa ufanisi.
 
Duuuh Ndg Hapo umewadanganya😃,, miji midogo mkoa wa geita Ni miwili tu inayotambulika kisheria ambayo Ni: 1.katoro township Na wa 2. Ushirombo township, : kwa upande wa mji wa katoro unaundwa na Kata tano ambazo ni: katoro,buseresre, Ludete, butengolumasa Na Kata ya Ibondo. Kwa upande wa mji wa ushirombo unaundwa na Kata nne ambazo ni : Ushirombo, Katente, Bulangwa Na Igulwa.

Sasa kwa ulivoeleza hizo data hapo ndg uwadanganya wadau: mana hizo miji mingine bado inajulikana kama vijiji mfano Runzewe pale mjini ile Ni Kata Moja tu ambayo Ni Kata ya uyovu tu Na kwa upande wa masumbwe hvyo hvyo, kwa lugha nyingine bado hazijafikia hadhi ya Kuitwa miji midogo!!
 
𝐍𝐄𝐌𝐂 𝐘𝐀𝐄𝐋𝐄𝐙𝐀 𝐒𝐀𝐁𝐀𝐁𝐔 𝐙𝐀 𝐊𝐔𝐄𝐍𝐄𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐆𝐔𝐆𝐔𝐌𝐀𝐉𝐈 𝐀𝐈𝐍𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐀𝐋𝐕𝐈𝐍𝐈𝐀 𝐙𝐈𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐂𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeueleza Umma wa watanzania juu ya uwepo wa gugumaji vamizi aina ya Salvinia SPP pamoja na jitihada zinazoendelea ili kulitokomeza katika ziwa Victoria.

Akizungumza na vyombo vya habari leo tarehe 2 Machi, 2025, Meneja wa Kanda ya Ziwa bwana Jarome Kayombo amewataka wananchi kuacha tabia za kutupa taka ovyo, kuacha shughuli za kibinadamu hasa kilimo ndani ya mita sitini ili kuzuia ongezeko la uchafu katika ziwa Victoria.

Meneja Kayombo ametolea ufafanuzi juhudi zinazoendelea kufanywa na NEMC kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine za Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Wadau wa Maendeleo, NGOs na wananchi kwa ujumla katika kutafuta mikakati ya muda mfupi, wa kati na muda mrefu ili kutokomeza magugumaji vamizi kwenye Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.

Mbali na mikakati mbalimbali, Kayombo aliongezea kuwa uwekezaji kando na ndani ya Ziwa Victoria uzingatie Sheria ikiwemo kufanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira ( TAM) kabla ya kuanza uwekezaji ili uwekezaji uweze kuzingatia misingi ya uwekezaji endelevu ili kupunguza uchafu kwenye Ziwa. Mikakati mingine ni kufanya kaguzi maalum katika maeneo yote yanayozunguka ziwa Victoria hususani viwanda, mashamba, hoteli, migodi, miundombinu ya majitaka na ukusanyaji wa taka ngumu ili kubaini vyanzo vya uchafuzi katika Ziwa Victoria ili kupunguza uchafu ndani ya Ziwa.

Alisema NEMC itaendelea kufanya kaguzi pamoja na utoaji elimu kwa wafugaji wa samaki ili kubaini wale wote wasiozingatia matakwa ya kisheria ya kufuga kwa mujibu wa miongozo waliyopewa pamoja na kuzingatia misingi yote ya utunzaji wa ubora wa maji ya ziwa.

Kayombo ametoa onyo kali kwa wawekezaji wote ( wanaowekeza kando au ndani ya ziwa) kufanya Tathimini ya Athari kwa Mazingira ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji ili uwekezaji ndani ya Ziwa Victoria uwe uwekezaji endelevu wa kutunza mazingira, wawekezaji kuzingatia masharti ya vibali vya mazingira ili kupunguza uchafu kwenye ziwa.

Baraza linatoa wito kwa Halmashauri zote nchini, Mamlaka zinazosimamia taka maji na ngumu pamoja na wananchi kwa ujumla kuimarisha mifumo ya uzoaji taka na utupaji taka ili kupunguza uchafuzi kwenye mito, mabwawa, maziwa na bahari kutogeuzwa kuwa maeneo la kutupa taka (dampo).

#magugumaji #ziwavictoria #matokeochanya #maendeleo #pressconference #samiaapp

#magugumaji #ziwavictoria #matokeochanya #maendeleo #pressconference #samiaapp #mwanzatanzania #lakevictoria #Mazingira #mwanza
mwanzatanzania #lakevictoria #Mazingira #mwanza
 
WAZO LA MKOA WA NJOMBE KUWA NA MJI MKUBWA WA VIWANDA NA BIASHARA NYANDA ZA JUU KUSINI LILIANZA MIAKA MINGI YA NYUMA KABLA HATA HAUJAWA MKOA KWA SASA KINACHOFANYIKA NI UTEKELEZAJI MOJA YA MAANDIKO HAYO NI HAYA 👇👇👇
IMG-20250302-WA0097.jpg
IMG-20250302-WA0096.jpg
IMG-20250302-WA0098.jpg
IMG-20250302-WA0099.jpg
 
Back
Top Bottom