Ila na ww usijidai kisa kilolo mna kilimo cha imwagiliaji..nidanganye kwingine sio hiyo sekta..! mtu unajipinda kulima nyanya then unakuja uza tenga kwa 3000??[emoji57][emoji57] yaan kafaida kanakuwa kadoogoo ...hapana aisee..nyie limeni tu kwakwel na vifaida vya laki 6 miez 3[emoji57][emoji57]!
^
huku bwana unalal.maskn unaamka.tajiri[emoji23][emoji23]..unalala.tajiri after a short tym u akuwa maskini! sasa huku wenye akili kama kina Manengelo lazima tutusue tu..starehe zinakaa kando na kusoma mchezo kwa ustadi mkubwa! endelen kulima fingamba be!
So far, Kilimo ni reliable kuliko madini,
Nimeenda Migodini na na nimechimba, naijua dhahabu, in and out,
I am telling you ule msoto wa kutafuta dhahabu watu tunakunywa na kupikia dona na dagaa kwa maji ya madimbwi, kulala kwenye vihema vya Mifuko ya cement, hapo unakuta msoto ni wa wiki tatu hadi mnapata mawe na kwenda kusaga, na mwisho wa siku mnaweza kuporora, au mnajikuta na gramu 8, hapo tupo watano,
Ukilipa madeni hapo na mgao wa mwenye crem basi mnayobakiwa nayo yote mnanywea pombe usiku huohuo na kesho asubuhi shimoni tena,
Uzoefu wangu unaonesha wanaofanikiwa kwenye madini ni wafanyabiashara pekee, ambao ni wachache sana na sio wachimbaji ambao ndio rundo,
Na maeneo ya migodini hapa bongo hakuna mtu anafikiria elimu, wala Afya, Wala miundombinu, The priority is money, money, money. watoto hawasomi shule wanafikiria kuchimba, ndio maana ni vigumu sana haya maeneo kupiga hatua, Nenda sehemu cha Makongirosi, Sangambi au hata Rukwa huko utakubaliana na mimi,
Contrary, kwa Kilimo kila anaejihusisha nacho atapata pesa hata kama si nyingi ila ataipata,
Pesa ya kilimo inakuwa kwenye mikono ya wengi zaidi na so long as mtu haipati overnight basi haifujwi, ndio maana ni rahisi sana watu wengi kujikwamua kwenye umaskini kwa njia ya Kilimo kuliko Madini.
Pia kilolo hatulimi nyanya tu, sasa tunalima mashamba ya Matunda, (parachichi n.k), Viazi, Mahindi, Misitu ya mbao ya Kutosha, Chai, Maharage, Njegere, Mbogamboga nk