Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

1722656485309.jpg
Mbeya Mpya inakuja,Mahoteli,Kumbi za mikutano na uwekezaji mwingine unakuja 👇👇

View: https://youtu.be/GK5KeilL-DY?si=phfjBcY1bx1rbOPv

Mawazo ya mh MBUNGE yapo vizuri yakifanyiwa kazi ipasavyo na wananchi wapewe elimu mambo yatakaa vizuri maana kwa Sasa jiji la mbeya limejaa eneo lenye uwaz mkubwa ni kilimo uyole na milimani ambako ni hatari kwa maporomoko ya udongo na hii hali inapunguza wawekezaji mfano ulimwengu wa sasa watu wanawekeza industrial park ,sport arena ,dry port , appertment , mall, nk yote haya yanahitaji maeneo makubwa ya uwekezaji halmashauri ikikosa eneo wanajikuta wanakosa uwekezaji na hii mbinu ya kupima mapema mbeya ni kama Kuna shida ukienda mbalizi Nako ni shida Sasa limebaki eneo ambalo ni jilani na airport ko Kuna uwekezaji mkubwa watakuwa wanaukosa shida maeneo
1722656351437.jpg
1722656462294.jpg
1722656338899.jpg
1722656291261.jpg
1722656485309.jpg
 
Hii kampuni inaenda kuchoche zaidi ukuaji wa viwanda mkoa wa njombe hasa mji uliotengwa wa viwanda makambako maana ndiko inakojenga industrial park 👇👇👇👇👇👇Kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Co. Ltd ya mjini Fuzhou katika Jimbo la Fujian kuwekeza katika kiwanda cha kuunganisha magari (assemblling plant👇👇👇👇ndo kampun iliyopewa kuchimba chuma makete DC👇👇👇👇
Kampuni ya Uchimbaji wa Chuma Fujian Hexingwang imetambulisha mradi wa Uchimbaji wa Mawe katika Kijiji cha Ipepo Kata ya Ipepo Wilayani Makete Mkoani Njombe.

Mradi huo umetambulishwa leo tarehe 5 Machi, 2024 kwa Wananchi wa Kijiji hicho mbele ya Viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya ya Makete akiwepo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Jackline Mrosso , Watalaamu ngazi ya Wilaya na Diwani Kata ya Ipepoo Mhe. Manase Nyaulawa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Jackline Mrosso amesema ujio wa Mradi huo mkubwa wa Uchimbaji wa Chuma ni fursa kubwa ya Ajira na kukuza uchumi wa Wananchi Wilayani Makete na Tanzania kwa ujumla.

Naye, Mkurugenzi wa Kampuni ya Fujan Fujian Hexingwang, Bwana Xu Xing Da amesema Mazingira mazuri ya Uwekezaji Wilayani Makete, yamepelekea kampuni hiyo, kujikita Wilayani humo sambamba na Usimamizi mzuri wa Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa Upande wake, Diwani wa Kata ya Ipepo Mhe. Manase Nyaulawa amewashukuru wawekezaji hao kwa kuamua kuwekeza katika kata hiyo na kuwaomba kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho katika kazi mbalimbali za Maendeleo.

Wananchi wa Kijiji cha Ipepo wamewakaribisha wawekezaji hao na kuwaahidi kutoa ushirikiano wakati wote na kuomba kupewa kipaumbele kwenye masuala ya Ajira pindi mradi utakapoanza kutekelezwa.
1719285557791.jpg
1722482701974.jpg
 

Attachments

  • 1722482701974.jpg
    1722482701974.jpg
    173.2 KB · Views: 2

Tanzania, Chinese firm to ink deal on iron ore project​

Tuesday, July 30, 2024
ndc-pic.jpg

The government of Tanzania will sign a contract worth USD 77.4 million with a Chinese firm, Fujian Xho Company Limited, to implement the Maganga Matitu Iron Ore project, the Industry and Trade Minister, Dr Selemani Jafo, said recently. At least Sh4.2 billion will be spent on compensating 385 people to be affected by the project.

Covering an area of 19.63 square kilometers, the Maganga Matitu Iron Ore project is part of the Liganga Iron Ore project, located in Ludewa District, Njombe Region.
 

WAZIRI JAFO AIPONGEZA NDC KWA KAZI NZURI​

Leave a Comment / Habari / By ndcAdmin
Mradi wa kwanza wa kuzalisha chuma nchini na Afrika Mashariki wa Maganga Matitu unatarajiwa kuanza utekelezaji Januri 2025 na tayari mwekezaji amepatikana huku uwekezaji wake ukifikia dola milioni 77.4.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Nicolaus Shombe alisema hayo Dares Salaam mbele ya Waziri wa Viwanda na Biashara alipotembelea shirika hilo kuzungumza na wafanyakazi.
Alisema mkataba kwa ajili ya kuanza kwa mradi huo utasainiwa ijumaa wiki hii(Agosti 2,2024) na wanatarajia kuanza kuchimba kiasi cha tani milioni moja kwa mwaka lakini kadri uwekezaji unavyoendelea wanaweza kuongeza pia.
Alisema mwekezaji anaaza kulipa fidia watu wapndoke na kuweka mashimo Kwa ajili ya kuanza. “Mkataba wa mradi huu una mpango wa utekelezaji kwamba mwekezaji asipotekeleza mkataba unaweza kusitishwa,” alisema Shombe na kuongeza kuwa katika uwekezaji huo, mwekezaji atakuwa na asilimia 64 na Serikali 36.
Akimtaja mwekezaji huyo kuwa ni Fujian Hexingwang Industry Tanzania Co. Limited ambaye wameingia naye ubia na kwamba yuko nchini na ana kiwanda kingine hapa. Shombe alisema Kwa sasa hivi viwanda vyote vya chuma vinatumia malighafi za chuma chakavu, hivyo kiwanda hicho kitazalisha chuma ghafi ambazo zitatumiwa na viwanda vingine na bidhaa nyingi za chuma zitasaidika na kiwanda hicho.
Alisema ukikamilika utakuwa na faida kubwa, kutoagiza tena bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi, lakini pia Tanzania inaweza kuuza nje ya nchi na kupata fedha za kigeni na kusaidia viwanda kupata malighafi na kuongeza ajira na kusaidia taifa.
Kuhusu mradi wa Liganga na Mchuchuma alisema umefikia hatua ya kuanza utekelezaji, kwa maana kwamba taratibu zote ikiwamo za kufanya tafiti, uchambuzi, upembuzi yakinifu, kupata cheti cha mazingira vinafanyika.
Alisema pia mwaka jana Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha sh bil 15.4 ambazo zimeenda kulipa fidia kwa waliopo kwenye eneo hilo. Alisema mradi huo ni makubwa wa kuzalisha makaa ya mawe na chuma na hatua zote za maandalizi zimekamilika kuna shughuli zinaendelea kule ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombi ya barabara, na maji.
Shombe alisema mradi mwingine ni wa magadi soda, wa Engaruka ambapo shirika limefanya tafiti zote na hatua iliyobakia kwa sasa ni kutoa fidia ya sh bilioni 14 na uzalishaji uweze kuanza. Akizungumza Jafo aliagiza NDC kuhakikisha miradi yote inafanyiwa kazi na kusimamia taratibu ziweze kukamilika na kupata wawekezaji. Alisema NDC ni shirika kubwa linategemewa na Taifa hivyo liifanye vizuri Kwa kuwa ni roho ya uchumi.
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, serikali haitakubali kuchimba madini kabla ya kupata mikataba iliyobora itakayonufaisha taifa.

Mhe. Dkt. Biteko ameyasema hayo Agosti 02, 2024 alipokuwa mkoani Njombe mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa uchimbaji wa madini ya chuma Maganga Matitu wilayani Ludewa mkoani Njombe kati ya shirika la Taifa la maendeleo (NDC) na mwekezaji wa Kampuni ya Fujian hexingwang industry Tanzania Co. Ltd.

Aidha, Dkt. Biteko amewahakikishia wawekezaji kuwekeza hapa nchini kwani serikali ya awamu ya Sita imeweka mazingira bora na salama ya uwekezaji.

Awali Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaudi Kigahe amesema mradi huu utatumia rasilimali za ndani kuchimba na kuchenjuwa chuma ghafi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt. Nicolaus Shombe amesema mradi umechukuwa miaka Kumi na saba bila kufanyakazi ambapo katika mkataba huo uliosainiwa mwekezaji atamiliki asilimia sitini na nne na serikali asilimia Thelathini na Sita.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amesema mradi huo utasaidia kukuza hali ya uchumi wa wananchi wa Mkoa wa Njombe
1722668757847.jpg
1722668783949.jpg
 
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, serikali haitakubali kuchimba madini kabla ya kupata mikataba iliyobora itakayonufaisha taifa.
Waliopita walisema watasaini mikataba ya kulitia taifa kwenye unyonyaji ?

Haya mambo waache ngonjera cha kufanya mambo yawe full transparent zaidi ya hapo ni brah brah brah tupu...
 
Mkoa wa njombe unaenda kufunguka zaidi zaidi maana chuma kipo kwenye ushindani mkubwa Sasa KATIKA mapinduzi ya nne ya viwanda duniani mataifa mengi ya Africa yataenda njombe kufata chuma kwaajili ya viwanda vyao na uzuri mwekezaji kiwanda Cha kuchenjua chuma kajenga mkoa wa njombe
1722740109078.jpg
1722740116681.jpg
 

Safi na mkoa wa njombe umeomba kupitia mradi wa chuma wajenge reli kutoka linganga na mchuchuma hadi makambako km 200 na hii ITARAHISISHA kuyafikia masoko mengi ya SADC NA EAC na kwenda bandari ya dsm nk"HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA WA DOLA MILIONI 77.45 ZA UCHIMBAJI CHUMA CHA MAGANGA MATITU - NJOMBE - YouTube"
View: https://m.youtube.com/watch?v=AW9Ecpd24JI&pp=ygUVUmVsaSBtYWthbWJha28gbHVkZXdh
 
Battle ya Njombe iwekwe na wilaya za Kasulu, Masasi, Mafinga, Mbinga, Igunga, Geita- Katoro, Ifakara lakini sio Kahama
hv sasa nmefika Njombe na Kahama , kahama bado sana , mwanzoni nlikuwa sijafika Njombe nkawa na picha kichwan ila nmepaona Njombe , kwasasa unaizidi kahama hata hiyo Shinyanga makao makuu ya mkoa , Kahama inapewa kiki tangu zamani ila sehem ya kawaida sana kimiundo mbinu ila kifursa pia wako vzr kwa kulinganisha na maeneo ya kanda moja , kahama ipo ndani ndani tofautina Njombe ipo Main road , Kahama wapo juu kwenye kilimo na madini kuliko Njombe ila watu wa Njombe wameuwekea mkoa wao mazingira ya kupiga hatua kwa kasi kwa kutumia kile kile kidog walichonacho kusonga mbele
 
hv sasa nmefika Njombe na Kahama , kahama bado sana , mwanzoni nlikuwa sijafika Njombe nkawa na picha kichwan ila nmepaona Njombe , kwasasa unaizidi kahama hata hiyo Shinyanga makao makuu ya mkoa , Kahama inapewa kiki tangu zamani ila sehem ya kawaida sana kimiundo mbinu ila kifursa pia wako vzr kwa kulinganisha na maeneo ya kanda moja , kahama ipo ndani ndani tofautina Njombe ipo Main road , Kahama wapo juu kwenye kilimo na madini kuliko Njombe ila watu wa Njombe wameuwekea mkoa wao mazingira ya kupiga hatua kwa kasi kwa kutumia kile kile kidog walichonacho kusonga mbele
Na bado ndo kunaenda kucha zaidi maana huu mradi wa chuma unaenda kuvuta watu wengi na uwekezaji unaenda kuongezeka zaidi ndo watajua kWanini TULIWAMBIA mkoa wa njombe umejipambanua vizuri na upo Kasi na toka Hawa wawekezaji walivoanza program ya ujenzi wa viwanda vya chuma uwekezaji unazidi kukua Sana hasa ujenzi wa mahotel ,viwanda na visima vya mafuta kampuni mbalimbali zinajenga visima
1721914395704.jpg
 
Back
Top Bottom