Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Lami zinazidi kupigwa Mitaan makambako HII imechochechea watu kuanza kujenga mijengo ya gorofa
1705752845206.jpg
IMG_20241205_115708_246~2.jpg
IMG_20241205_120036_997.jpg
IMG_20241205_115708_246~2.jpg
 
Njombe to ifakara na mbeya to ifakara mwamba anazidi kushusha vyuma
1733685345957.jpg
 
Kasi iongezewe ujenzi wa mradi wa miji 28- Kundo

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Mathew (Mb) ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 wa Njombe, Makambako, Wanging'ombe na Rujewa kwa gharama ya shilingi Bilioni 157

Mhandisi Kundo amesema mradi huo upo nyuma ya utekelezaji wake, ambapo amemtaka mkandarasi kuongeza wafanyakazi watakaofanyakazi usiku na mchana.

Amewaelekeza wasimamizi wa Wizara ya Maji kuhakikisha mkandarasi anatekeleza mradi huo kwa kuzingatia viwango vya ubora ulioainishwa kwenye ujenzi wa miundombinu inayotekelezwa.

Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Zakaria Mwansasu na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Maulid Surumbu licha ya kushukru kwa utekelezaji wa mradi huo, pia wameiomba Serikali iharakishe kutekeleza ili wananchi wa maeneo hayo waweze kunufaika.

Mradi wa Miji 28 utanufaisha wananchi zaidi ya laki tano wa miji ya Njombe, Makambako, Wanging'ombe na Rujewa
1733982103864.jpg
 
Hata kama madini yapo sio mengi kwa kiasi hicho, Buzwagi ndio hiyo inakauka miaka michache ijayo kutapauka, pili Kahama sio mji wa transport hub Kama Njombe ni suala la muda tu Kahama itapauka wakati Njombe ndio kuna kucha hivyo. Pindi barabara za Njombe/Itoni kudewa mbamba bay, Njombe Ifakara mikumi na Njombe makete Mbeya zikikamilika zitakuwa ni ufunguo mkubwa sana huku kwa fursa.

Pia usisahau kwamba Njombe ni mkoa wa wachapa kazi na pia kumbuka kuna mabwawa 4 ya kufua umeme yako mbioni kujengwa yote hiyo inakupa picha ya Njombe ya Kesho sio sawa na huko mnakoongoza kwa maskini wengi.
HAZIKUTOSHI WEWE
 
Njombe makelele mengi hamna kitu wenzenu wanasonga mbele View attachment 3175984
Uongozi wa Avocado Avenue Tanzania Ltd Wazuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Njombe, Desemba 13, 2024 – Uongozi wa Kampuni ya Avocado Avenue Tanzania Ltd ukiongozwa na Bw. Amin Manji, leo umefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kupokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka.

Katika mazungumzo yao, walijadili masuala muhimu yanayolenga kuimarisha uchumi wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe. Miongoni mwa mambo yaliyopatiwa msisitizo ni kuanza kwa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata parachichi ambacho pia kitatengeneza mafuta ya parachichi. Aidha, kampuni hiyo imeahidi kununua parachichi zote, ikiwemo zile zilizokataliwa, na kuzigeuza kuwa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya masoko ya ndani na ya kimataifa.

Mbali na kiwanda, Avocado Avenue Tanzania Ltd imeeleza mipango yao ya kutoa soko endelevu la parachichi kwa wakulima wa Njombe. Kampuni hiyo pia imeahidi kutekeleza programu za kuwawezesha wakulima kwa:
✅ Kutoa maarifa ya kitaalamu kuhusu kilimo bora cha parachichi.
✅ Kutoa msaada wa utunzaji wa mazao.
✅ Kuwasaidia wakulima kufanikisha mavuno bora na kuendeleza kilimo endelevu.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025, ambapo kampuni hiyo itaanza kupokea mazao ya parachichi kutoka kwa wakulima. Aidha, kiwanda hicho kitatoa ajira za kudumu kwa watu 100 na ajira za mikataba kwa takriban watu 300, huku wakitarajia kushirikiana na kuwafikia zaidi ya wakulima 1,500.

Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Avocado Avenue Tanzania Ltd kwa kuamua kuwekeza mkoani Njombe. Akizungumza wakati wa kikao hicho, alisema:
“Nawashukuru sana kwa kuja kuwekeza katika sekta ya parachichi mkoani Njombe. Uamuzi wa kujenga kiwanda cha kuchakata parachichi hapa Njombe utaongeza thamani ya tunda hili moja kwa moja kuanzia hapa hapa mkoani. Hatua hii itakuza uchumi wa wakulima wetu na kuongeza ajira kwa wananchi wa Njombe na maeneo ya jirani.”

Kampuni ya Avocado Avenue Tanzania Ltd imeonyesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na mkoa wa Njombe kuimarisha sekta ya kilimo cha parachichi na kuboresha maisha ya wakulima.
1734111760366.jpg
 
Uongozi wa Avocado Avenue Tanzania Ltd Wazuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Njombe, Desemba 13, 2024 – Uongozi wa Kampuni ya Avocado Avenue Tanzania Ltd ukiongozwa na Bw. Amin Manji, leo umefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kupokewa rasmi na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka.

Katika mazungumzo yao, walijadili masuala muhimu yanayolenga kuimarisha uchumi wa wakulima wa parachichi mkoani Njombe. Miongoni mwa mambo yaliyopatiwa msisitizo ni kuanza kwa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata parachichi ambacho pia kitatengeneza mafuta ya parachichi. Aidha, kampuni hiyo imeahidi kununua parachichi zote, ikiwemo zile zilizokataliwa, na kuzigeuza kuwa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya masoko ya ndani na ya kimataifa.

Mbali na kiwanda, Avocado Avenue Tanzania Ltd imeeleza mipango yao ya kutoa soko endelevu la parachichi kwa wakulima wa Njombe. Kampuni hiyo pia imeahidi kutekeleza programu za kuwawezesha wakulima kwa:
✅ Kutoa maarifa ya kitaalamu kuhusu kilimo bora cha parachichi.
✅ Kutoa msaada wa utunzaji wa mazao.
✅ Kuwasaidia wakulima kufanikisha mavuno bora na kuendeleza kilimo endelevu.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025, ambapo kampuni hiyo itaanza kupokea mazao ya parachichi kutoka kwa wakulima. Aidha, kiwanda hicho kitatoa ajira za kudumu kwa watu 100 na ajira za mikataba kwa takriban watu 300, huku wakitarajia kushirikiana na kuwafikia zaidi ya wakulima 1,500.

Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Avocado Avenue Tanzania Ltd kwa kuamua kuwekeza mkoani Njombe. Akizungumza wakati wa kikao hicho, alisema:
“Nawashukuru sana kwa kuja kuwekeza katika sekta ya parachichi mkoani Njombe. Uamuzi wa kujenga kiwanda cha kuchakata parachichi hapa Njombe utaongeza thamani ya tunda hili moja kwa moja kuanzia hapa hapa mkoani. Hatua hii itakuza uchumi wa wakulima wetu na kuongeza ajira kwa wananchi wa Njombe na maeneo ya jirani.”

Kampuni ya Avocado Avenue Tanzania Ltd imeonyesha dhamira ya dhati ya kushirikiana na mkoa wa Njombe kuimarisha sekta ya kilimo cha parachichi na kuboresha maisha ya wakulima.View attachment 3176039
Ndo hayo makelele lakini hamsogei eti leo mpo level moja na Rufiji
 
Back
Top Bottom