Hizo barabara hapo juu section ya Kahama barabara za mikoa za kujaribu kuipush Kahama isizidi Kusinyaa wakati kwa section ya Njombe hizo zote ni barabara kuu(trunk roads) za kuinganisha na mikoa mingine isipokuwa hiyo ya Njombe-Iyayi na Makete-Makete-Isyonje/Mbeya,,hizo za sections za Njombe-moronga na Moronga-Makete zimekamilika tena kwa asphalt standard sio kwa surfae dressing kama za huko Kajamaa.
Kuna barabara nyingi ambazo zinaendelea kujengwa na zimetajwa kwenye ilani hujaziweka kwa mfano Itoni/Njombe-Ludewa-Manda iko inajengwa tena kwa zege umbali wa km 100,,pia hujaiweka barabara ya Manda-Mbamba bay Ruvuma,Ludewa-Madaba/Songea na pia hujaweka ukarabati wa barabara kuu ya Makambako-Njombe-Songea,zote hizi ziko kwenye ilani ila unajifanya hujaziona.
Kuhusu reli naomba ieleweke kwamba Isaka sio kahama halikadhalika sgr ya Mtwara-mbambabay itakuwa na matawi mchuchuma na liganga,sio Njombe mjini ila ni mkoa wa Njombe kama tu ambavyo Tazara inapita Makambako ndani ya Njombe..Hoja yangu hapa ni kwamba hakuna haja ya kuiweka isaka maana sio Kahama hata kama iko ndani ya Wilaya ya Kahama.Mkuu kiufupi ni safe kuwekeza Njombe kuliko Kahama maana wenzio huku kila kona ya hizo roads hapo juu zinafungua fursa kubwa ya mazao ya matunda/parachichi,nafaka na bidhaa za miti.