Dissertation yangu nilifanya juu ya athari za uwekezaji mkubwa (Mega investments) kwenye spatial growth pattern za miji.
Kwa mfano kuimarika kwa uwekezaji kwenye Gas hakuathiri sana ukuaji wa Lindi na mtwara.. na uwepo wa migodi wa Bulyanhulu na Buzwagi athari yake kwa ukuaji wa kahama ni mdogo sana..
Nimeraise issue hiyo kwa sababu ya miradi uliyoitaja.. ya chuma nk.. athari yake kwa mji wa NJOMBE ni ndogo sana.. spending na contracts kubwa zilikuwa zikifanyika DSM japo mgodi uko kahama kwa kesi ya Barrick.. huku Geita gold athari kubwa ilikuwa kwanza kuliko Geita kwenyewe..
Mwanzoni kuna influx inayotokana na speculation.. ambayo.inaphase out in just few years mwanzoni wafu walikimbilia kahama kuwekeza wakidhani madini na biashara ya mgodi itahusisha wafu kila siku.. just to realize majority of contractors wako headquartered DSM the most walichopata ni kusupply matunda na catering 🙂
Kahama imejaa wachuuzi.. yes ila kwa sasa imekwisha panua catchment yake... Kuanzia Kibondo, Kakonko, Nyakanazi, Ushirombo, Runzewe, Masumbwe, Kakola, Kharumwa, Geita, Segese, Ulowa, Ushetu, Nzega, Isaka, Ngara, Shinyanga, Hadi tabora wanaprocure vitu vya jumla kutoka Kahama.
Mchele wa kahama unatoka mbali sana, Nzega, Bukoli, Ulowa, Busangi, Msalala, Salawe, Mapaka maeneo ya tabora urambo huko wote wanapeleka mchele kahama, kwa sababu moja, pamejiaestablish kama soko la uhakika, mashine za kisasa, umeme wa uhakika na storage facilities.. na ukipata fedha yako Banking facilities ziko nyingi kukusaidia.
Manufacturing is the new era, uzalishaji unaongezeka kila siku na hii itaendelea kuistrengthen kama a go to place kwa wakulima na wanunuzi wa bidhaa za jumla.. vyakula vya wanyama animal feed, usindikaji wa mchele, matunda na mahindi.. utendenezaji wa nguo, soon karibu textiles na nida kutaifanya kahama kubwa kitovu cha biashara ya zao la pamba.. mafuta ya kula na sabuni.. kiwanda cha kutengeneza ceiling boards kutokana na pumba za mchele nk..
Mabadiliko ni makubwa... Na Ulisikia Jafo akisema.. mpango kilomita 36 zilizo kwenye mpango tayari zitakuwa ni proper asphalt na sio surface dressing tunazojenga... Ila kwa kupandishwa hadhi nadhani kutakuwa na kilomita zaidi ya 30 za ziada hiyo pekee itabadilisha kahama mno.. .maana kuna maeneo mengi yenye nyumba bora sana ila hazifiki.