ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
HATUA ZA AWALI UJENZI WA UWANJA WA NDEGE NJOMBE ZAANZA
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo tarehe 06 Februari 2024 ametembelewa ofisini kwake na Timu ya Wataalamu kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) waliokuja kwa lengo la kutoa taarifa ya kukabithi eneo la mradi wa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina.
Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Njombe kinakwenda kujengwa kwa hadhi ya Kiwanja cha Ndege cha Kikanda (Daraja 4E) na Mtaalamu Muelekezi (Consultant) kutoka Kampuni ya Intercontinental Consultants and Technocrats Pvt.Ltd ya nchini India.
Mradi huu ni wa miezi 10 unatarajiwa kukamilika mnamo mwezi Oktoba,2024 na kisha taratibu za manunuzi ya kandarasi ya ujenzi itaanza.
Mawanda ya mradi yatahusisha ujenzi wa Barabara ya kutua na kuruka ndege, Barabara ya kiungio na maegesho ya Ndege kwa kiwango cha Lami; Ufungaji wa taa za kuongozea ndege (AGL); Jengo la mizigo likiwa na mitambo ya kuhifadhia ubaridi; Jengo la kuongozea ndege; Jengo la abiria; Kituo cha zimamoto na vifaa vyake pamoja na ujenzi wa miundombinu wezeshi kama uzio wa usalama.
Tutaitegemea ATCl Cargo hapoHATUA ZA AWALI UJENZI WA UWANJA WA NDEGE NJOMBE ZAANZA