Wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Makambako imepanga kununua tani elfu 91 za mahindi na mpunga kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kati ya tani hizo elfu 91,mahindi ni tani elfu 66 na mpunga ni tani elfu 25,ambapo wakala huo unanunua mahindi kilo moja kwa shilingi 650 kwa kituo cha Makambako mjini na Kituo cha Igula Ilembula kilichopo wilayani Wanging'ombe ni shilingi 600 kwa kilo moja huku mpunga ikinunua kwa kilo moja kwa shilingi 750 kwa vituo vilivyopo vijijini na mjini Makambako ni shilingi 800.
Hayo yamebainishwa na meneja wa wakala wa hifadhi ya chakula kanda ya Makambako Revocatus Bisama wakati akizungumza na iceFm ofisini kwake,ambapo ameeleza kuwa wakala huo umeaanza kununua mahindi na mpunga kwenye baadhi ya wilaya hasa Wanging'ombe na Mbarali.
Hata hivyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya kilimo kupitia wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula kuanza kununua mahindi kwa shilingi 700 kwa kilo moja nchini kote.
#IceFmhabari
#NisikilizeMimi
Na @cleefmlelwah