Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe imekusudia kuanza ujenzi wa kituo cha maegesho ya malori katika mtaa wa jeshini uliopo kata ya Maguvani kwa mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 chenye uwezo wa kuegesha malori zaidi ya 150 ambacho kitatumia fedha zaidi ya bilioni mbili.

Pia katika mwaka huu wa fedha halmashauri itaanza ujenzi wa kituo cha maegesho ya malori katika eneo la A one lilipo mtaa wa Kahawa,ambacho kitatumiwa na malori yote yanatoka barabara ya Songea -Makambako huku kituo cha jeshini kikitumiwa na malori yanayotoka Barabara ya Iringa- Mbeya.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako Kenneth Haule wakati akizungumza na iceFm ofisi kwake,ambapo amesema lengo ya ujenzi wa vituo vya maegesho ya malori ni kuupanga mji na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi na mapato ya halmashauri na kueleza kuwa mpaka sasa fedha milioni 800 zimepatikana kutoka bodi ya mikopo ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ili kuanza ujenzi wa kituo cha maegesho ya malori jeshini.

Aidha Mwenyekiti wa mtaa wa jeshini ambako kituo hicho kinajengwa Meckson Mchape na mwenyekiti wa mtaa wa mizani Kelvin Mwangili wamesema endapo kituo hicho kitakamilika kitasaidia kupandisha thamani ya maeneo yao na itaongeza ajira kwa wananchi hasa wajasiliamali wadogo.

Nao baadhi ya wananchi wa mtaa wa jeshini wameitaka halmashauri kukamilisha kwa wakati ujenzi huo ili kukuza fursa za kiuchumi kwao.

Mpaka sasa eneo lenye ukubwa wa ekari 13 limepatikana katika mtaa wa jeshini kwaajili ya ujenzi wa kituo cha maegesho ya malori ambapo shughuli za kukata miti zimeshafanyika ili kuanza ujenzi huo.

#IceFmHabari
#NisikilizeMimi
@makambakotc
Na @cleefmlelwah
1721269380730.jpg
1720847404224.jpg
 
Wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) kanda ya Makambako imepanga kununua tani elfu 91 za mahindi na mpunga kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Kati ya tani hizo elfu 91,mahindi ni tani elfu 66 na mpunga ni tani elfu 25,ambapo wakala huo unanunua mahindi kilo moja kwa shilingi 650 kwa kituo cha Makambako mjini na Kituo cha Igula Ilembula kilichopo wilayani Wanging'ombe ni shilingi 600 kwa kilo moja huku mpunga ikinunua kwa kilo moja kwa shilingi 750 kwa vituo vilivyopo vijijini na mjini Makambako ni shilingi 800.

Hayo yamebainishwa na meneja wa wakala wa hifadhi ya chakula kanda ya Makambako Revocatus Bisama wakati akizungumza na iceFm ofisini kwake,ambapo ameeleza kuwa wakala huo umeaanza kununua mahindi na mpunga kwenye baadhi ya wilaya hasa Wanging'ombe na Mbarali.

Hata hivyo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameitaka wizara ya kilimo kupitia wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula kuanza kununua mahindi kwa shilingi 700 kwa kilo moja nchini kote.

#IceFmhabari
#NisikilizeMimi
Na @cleefmlelwah
 
Back
Top Bottom