Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

P
Hakuna picha Mpya?
Sema saiz project njombe tc zimepungua Sana tofauti na mwanzo ulivotangazwa mkoa Kasi ilikuwa kubwa ya ujenzi wa gorofa saiz zilizoongezeka za biashara ni kama tatu na ofisi idara mbalimbali za mkoa ndo maana utaona picha ni zilezile
 
Makambako
IMG_20240723_113405_469.jpg
 
KWA IDADI HII NI HALALI MKOA UWE NA MJI WA VIWANDA NA BIASHARA HIZI PLAN ZILIANZA TOKA 2015 ILA AWAMU YA SITA INATEKELEZA KWA VITENDO UWEKEZAJI UNAONEKANA 👇👇👇👇👇👇👇Zaidi ya wachina elfu sita (6,000) wanatarajiwa kuingia katika Mkoa wa Njombe kwenye sekta ya madini hasa makaa ya mawe na Chuma kwenye eneo la Liganga na Mchuchuma wilayani Ludewa.
Hayo yamesemwa jana kwenye Ukumbi wa Lutheran Makambako na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi alipokuanaongea na watumishi wa Halmashuri ya Mji Makambako,alisema kuwa Mradi wa Linganga na Mchuchuma unatarajiwa kuanza kuchimbwa makaa ya m awe na chuma hivi karibuni utatoa ajira zaidi ya Elfu thelathini (30,000) zikiwepo za wazawa na wageni.
Kutokana na hilo amewataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya Ardhi kuakikisha wanaweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi na kupima viwanja ili kuwavutia wawekezaji mbalimbali katika ujenzi wa Hoteli za kisasa na halmashuri kuakikisha wanaboresha miundombinu ya Maji na barabara .
Dk .Nchimbi alisema kuwa mpaka sasa shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) limeanza mchakato wa uthamini wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia kupisha mradi huo.
Aliwataka wananchi wa Makambako na Njombe kwa Ujumla kujiandaa na ujio wa wageni mbalimbali kwa kufuga kuku ,Ng’ombe pamoja na mifugo mingine ili kuweza kuwauzia wageni hao na kuongeza kipato cha familiya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa wanajiandaa kwa kuwapokea wageni hao kwa kuakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi katika eneo la Makambako.
 
Kamati ya ALAT Taifa Julai 24,2024 imefanya ziara ya siku moja Mkoani Njombe ikiwa na lengo la kujifunza namna Mkoa wa Njombe unavyotekeleza shughuli zake za Kimaendeleo.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Ndugu.Murshid Ngeze imepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka.

Wakati akitoa salamu za Serikali Mhe.Mtaka ameipongeza Kamati hiyo kwa kuja Mkoani Njombe na kukagua baadhi ya Miradi inayotekelezwa na alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha kutazama fursa mbalimbali zinapotikana Mkoani Njombe haswa kwenye Maeneo ya kiuwekezaji kwenye Mradi Mkubwa Madini ya Chuma na Mkaa ya mawe lakini pia kwenye Kilimo na biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja bidhaa za misitu.
1721869113630.jpg
 
Mambo ni moto roli zidazidi kufurika songea road na soon vikikamilika viwanda vya chuma zinaenda kufurika zaidi
1721870152403.jpg
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe wameupongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara ya Itoni - Lusitu kwa kiwango cha zege yenye urefu wa kilometa 50 ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Itoni -Ludewa - Manda (Km 211.4).

Barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Malawi na Tanzania upande wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania na ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vivutio vya utalii, kuwa kiungo kizuri kati ya mgodi wa makaa ya mawe (Mchuchuma) bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa. Pia Barabara hii ikikamilika itakuwa kiungo kizuri na barabara za ushoroba wa Makambako hadi Ruvuma.

Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani Njombe, Katibu wa CCM Mkoa wa mkoa huo Ndg Julius Peter amempongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ndiyo watekelezaji.

#kilichoborakabisa
1721916827005.jpg
 
CCM NJOMBE, RC MTAKA WARIDHISHWA NA UJENZI WA BARABARA YA KIWANGOCHA ZEGE YA ITOLI-LUDEWA-MANDA

Chama cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe wameupongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa usimamizi madhubuti wa ujenzi wa barabara ya Itoni - Lusitu kwa kiwango cha zege yenye urefu wa kilometa 50 ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Itoni -Ludewa - Manda (Km 211.4).

Barabara hiyo ni kiunganishi cha nchi za Malawi na Tanzania upande wa nyanda za juu kusini mwa Tanzania na ukikamilika utachochea ukuaji wa uchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa usafiri, urahisishaji wa kufanya biashara na kuwezesha wananchi kuchangamana kwa urahisi, kuwezesha kufikika kwa urahisi kwenye vivutio vya utalii, kuwa kiungo kizuri kati ya mgodi wa makaa ya mawe (Mchuchuma) bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mombasa. Pia Barabara hii ikikamilika itakuwa kiungo kizuri na barabara za ushoroba wa Makambako hadi Ruvuma.

Akizungumza mara baada ya ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM mkoani Njombe, Katibu wa CCM Mkoa wa mkoa huo Ndg Julius Peter amempongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) ndiyo watekelezaji.

Amesema kuwa CCM imeridhishwa na ujenzi huo ambao ulisimama kutokana na mvua kubwa za El-Nino ambazo zilizokuwa zinaendelea kunyesha na baada ya mvua hizo kumalizika sasa amewasihi wakandarasi kuendelea na kazi ya ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe Antony Mtaka amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetibu vikwazo vya miradi mbalimbali mkoani Njombe ambapo ameridhia kuanza kwa mradi wa Mchuchuma na Liganga kwa kutoa shilingi Bilioni 15 kulipa fidia pamoja na kukubali kuanza kwa mradi mkubwa wa chuma wa Maganga-Matitu.

Vikwazo vingine vilivyotibiwa ni pamoja na kuimarisha na kujenga miundombinu ya barabara ikiwemo kutoa jumla ya shilingi Bilioni 120.9 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itoni -Ludewa - Manda kipande cha Itoni - Lusitu kwa kiwango cha zege ambayo ni barabara yenye gharama kubwa kuliko zote Tanzania.

"Dhamira ya Mhe Rais kuhakikisha barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha zege ndani ya muda kama ilivyokusudiwa, Pesa zipo wakandarasi wapo, tulipata changamoto ya mvua lakini kwa sasa miradi inaendelea na wananchi waanze kufuatilia fursa za uwekezaji zitakazoimarisha uchumi wao" Amekaririwa Mhe Mtaka

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa Wakala ya Barabara Tabzania (TANROADS) mkoa wa Njombe Mhandisi Ruth Shalua amesema kuwa Mkataba wa Ujenzi wa Barabara hii ulitiwa saini kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkandarasi M/s China Civil Engineering Construction Cooperation kutoka China tarehe 29 Machi, 2022 kwa gharama ya Shilingi 120.9 pamoja na VAT.

Amesema kuwa Mhandisi Mshauri anayesimamia mradi huo ni Cheil Engineering Co. Ltd ikishirikiana na kampuni ya Hana E&C Co. Ltd na ENGTEC Engineering (T) Ltd zote za Tanzania.

MWISHO
 
Back
Top Bottom