Kahama VS Njombe/Mafinga

Kahama VS Njombe/Mafinga

Zoom πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Tu zoom wakati vijiji vinaonesha na tumesha pita huko Wacha njombe iendelee kutanua mji wa viwanda na biasharaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa soko la Makambako ulianza baada ya Serikali kuona umuhimu wa kujenga masoko ya kimkakati (Strategic Markets) kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa mazao ya Wakulima. Soko hilo lilibuniwa, ili kufanikisha upatikanaji wa soko la uhakika kwa mazao ya kilimo hususan nafaka za mahindi na mchele ambazo huzalishwa kwa wingi katika Mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya.

Mheshimiwa Spika, napenda kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kwamba, mwaka 2018 Serikali ililipa kiasi cha shilingi 3,026,341,089.58 ikiwa ni fidia kwa wananchi 209 wa Makambako ili kupisha ujenzi wa soko hilo. Aidha, wakati wa ulipaji fidia, walijitokeza wananchi 15 ambao wakati wa uhakiki wa mwisho hawakupatikana na wananchi 20 ambao hawakuwepo kwenye daftari wala taarifa ya uhakiki. Kwa muktadha huo, Serikali imeamua kufanya tathmini tena kwa wananchi ambao hawajalipwa fidia zao ili waweze kulipwa kama wanastahili.

Mheshimiwa Spika, ninaupongeza uongozi wa Mkoa wa Njombe na Waheshimiwa Wabunge wanaotoka Mkoa huo kwa ushirikiano walioutoa katika zoezi zima la ulipaji fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa ujenzi wa soko la Kimataifa la Makambako. Zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi wote l
 
Unapost kijumba kimoja kimoja why can't you post the whole thing?πŸ€­πŸ€­πŸ€”
Na utapata tabu Sana wenzenu wanaenda kwa future na geographical position ya eneo KATIKA uwekezaji πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge Neema Mgaya kwa namna anavyofuatilia changamoto za wananchi wa Mkoa wa Njombe, nakupongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza la Mheshimiwa Mgaya ni kwamba lini tathimini itakamilika. Kwa kuzingatia azma ya Serikali ya kuhakikisha tunawasaidia wakulima wetu kupata masoko ya uhakika, jambo hili tunalichukulia kwa uzito na tathmini, tutahakikisha inafanyika haraka iwezekanavyoo na kwa vile kupitia Wabunge, wananchi watatupa ushirikiano katika kukamilisha suala la fidia, basi nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tathmini itakamilika haraka iwezekanavyo, ili kupitia soko la kimataifa la Makambako, wakulima wanaotoka kwenye Nyanda za Juu Kusini waweze kuzalisha kwa wingi na kupata masoko ya uhakika kupitia soko la kimataifa la Makambako.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mgaya angependa kujua nini mkakati wa Wizara yetu katika kuhakikisha tunaongeza viwanda vidogovidogo ili kuchakata mazao ya wakulima. Nimhakikishi Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali tayari ina mikakati mizuri, bilaterally kwa kuandaa makongamano mbalimbali nchini, ambapo wafanyabiashara kutoka nchi za SADC, wafanyabishara kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanakuja hapa Tanzania kukutana na wafanyabiashara na wenye viwanda hapa nchini, lengo hilo na mkakati wa Serikali ni kuhakikisha kupitia forum hizi tunavutia uwekezaji lakini tunasaidia wafanyabiashara na wenye viwanda nchini ku-network na wenzao ambao wanatafuta fursa za kuwekeza hapa nchini na kwa vile utekelezaji wa blue print unakwenda vizuri, basi nina imani kabisha mikakati hii itaweza kusaidia kuchochea ujenzi wa viwnada nchini.
Ndio maana nakuambia ushamba unakusumbua, yaani kila Kijiji huko ni old-fashioned 🀣🀣🀣 wait nikutoe matongotongo.
 
Ndio maana nakuambia ushamba unakusumbua, yaani kila Kijiji huko ni old-fashioned 🀣🀣🀣 wait nikutoe matongotongo.
Mzee wa mapaa angalia wenzenu Wana deal na nn Ndo utajua njombe imejipanga ko mnavopanga kuwa mnataka mji wa aina gani lazima mwende kwenye mataifa makubwa yaliyopiga hatua na yamewekeza kwa mfumo huo πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Diwani wa kata ya Kitandililo katika Halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe Imani Fute ameliomba taifa la china kuisaidia Tanzani kupata soko la parachichi, chai,korosho na ufuta.

Fute ametoa ombi hilo akiwa nchini china kwenye semina ya diplomasia ya uchumi wakati akizungumza katika semina hiyo yenye wawakilishi 42 kutoka mataifa 11 duniani, ambapo ameiomba china iisaidie Tanzania kwenye soko la mazao hayo huku akitaka ije iwekeze kwenye soko la kimataifa Makambako ambalo eneo limetengwa.

Fute amesema ombi hilo ni kutokana na jitihada za Rais Dkt.Samia Suluhu Hasan katika kukuza uchumi wa wananchi na Taifa letu.

#IceFmHabari
#NisikilizeMimi
Na @cleefmlelwah
1729580715634.jpg
 
MAENDELEO YA UWEKEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA
Wakati Serikali ikiendelea na jitihada mbalimbali za kutafuta mwekezaji wa mradi wa Liganga na Mchuchuma uliopo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,Tanzania inatarajiwa kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya chuma Barani Afrika.

Wakati jitihada hizo zikiendelea mnamo Agosti 3 , 2024 Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) lilitia saini makubaliano ya uchimbaji wa makaa ya mawe na chuma katika mradi wa Maganga Matitu na kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania Co.Ltd itakayowekeza kiasi cha Dola za Marekani milioni 77.

Ikumbukwe kwamba hivi karibuni ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dkt.Samia Suluhu Hassan aliiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara , Mipango na Uwekezaji kukamilisha mchakato wa kupata kampuni itakayowezesha kuanza kwa mradi wa Liganga na Mchuchuma.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa mradi wa Liganga na Mchuchuma ukikamilika utazalisha kiasi cha tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa kipindi cha zaidi ya miaka 70, na madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni pamoja na Titanium tani 175,400 kwa mwaka na madini aina ya Vanadium tani 5000 kwa mwaka.

Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 , uanzishwaji wa kiwanda cha kuchenjua chuma na bidhaa zitokanazo na chuma.
Ndio maana nakuambia ushamba unakusumbua, yaani kila Kijiji huko ni old-fashioned 🀣🀣🀣 wait nikutoe matongotongo.
SOma hiyo ndo UTAELEWA kwanini wenzenu wame plan kuwa na mji mkubwa wa viwanda na biashara πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡MAENDELEO YA UWEKEZAJI MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Back
Top Bottom