Hayo unayoyasema kama ni mambo hakuna unatakiwa ujue kuna improvement kubwa Sana,ungekuwepo kabala ya 2015 ndio ungejua kwamba kuna improvement kubwa..
Hiyo barabara ya Malawi unayosema sio muhimu kibiashara hiyo ni shida yako binafsi maana Mji unakua zaidi njia ya Ileje na Sumbawanga..
Kuhusu maji hata hayo unayiosema ni ya kisima ni ushukuru kuna hata visima kwa sasa ila zamani tulikuwa tunafuata Chimbuya huko,Mjini kule kuna mradi wa maji ya Bomba japo mradi mkubwa wa uhakika mtapata kutoka Ileje..
Barabara za lami za mitaani walau zipo za kutafutiza miaka hii,hiyo Tunduma unayoiona hata mitaa ilikuwa haipo vyote hivyo vimefangika Kati ya 2010 hadi sasa,kwa kuwa TARURA sasa ipo mtapata hizo barabara maana ilibidi makazi yavunjwe Ili kupata mitaa kutokana na ujenzi holela..
Mambo ya Elimu kwa sasa Tunduma inajitahidi hasa kwenye elimu ya msingi na Sekondari,Mambo ya Vyuo bado ila huo mpango wa Veta upo maana hata Mkoa wa Rukwa hakuna Veta ya Serikali na haki iko hivyo Kwa maeneo mengi ya Nchi..
Mambo ya biashara ndio mahali pake na hizo vituo vya mafuta ni ishara kwamba kuna biashara kubwa sio tuu hiyo bali hata maduka ni mengi Mji mzima ni biashara..
Mwisho unatakiwa kujua.kwamba Halmashauri ya Mji wa Tunduma imeundwa mwaka 2010 kwa hiyo kwa yaliyofanyika so far naona wamejitahidi Sana maana ndani ya miaka 12 tayari kuna hospital Kubwa ya Mji,stand nzuri ya mpemba,mashule kibao zikiemo English medium za serikali,wanapima viwanja na kupanga Mji,mitaa inaanza kuwekwa na pia kitu kikubwa ni kwamba hapo kuna wageni wengi tofauti na unavyosema maana huo Mji ni WA wahamiaji zaidi..