Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Nipo katika moja ya nchi za Ulaya kikazi na nimebahatika kuingia katika duka kubwa la Costco.
Humo katika pitapita kwenye sehemu ya groseries nimekuta kahawa ya kutoka Tanzania sehemu ya Lyamungo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Kahawa hii ni nzima na imeokwa (roasted) na mtumiaji hutakiwa kuitengeneza mwenyewe kwa kutumia mashine maalum (coffee maker) na chujio.
Baada ya kusagwa kahawa huwekwa kwenye sehemu ya chujio na kisha maji ya moto hutumika kuchanganya ili kupata kahawa nzuri.
Kahawa hii ni ya muda maalum yaani "limited edition" na ni "special" sana kwa utamu na harufu nzuri ya kahawa yaani "aroma".
Katika maelezo yalo kwenye mfuko wake wenye gramu 907, kahawa hii yapakiwa na kampuni ya Kirkland na yauzwa kiasi cha dola 7.80 au shilingi kama 18,140 fedha za madafu.
Je, mkulima wa Tanzania anapata kasi gani kabla ya kahawa hii kusafirishwa nje ya nchi?
Na vyama vya ushirika vinalipa kiasi gani kwa kilo kwa mkulima?
Kahawa ya Tanzania yasifika sana kwa harufu yake nzuri na usafi wake.
Ipo pia kahawa kutoka Congo DRC jimbo la Bukavu ambayo bei yake imezidi kidogo kwa dola moja.
Je, wizara ya kilimo ina mikakati ipi ya kuhakikisha bidhaa kama hii ya Kahawa, Chai na zingine zafika huko nje na kumuinua mkulima wa kitanzania?
Ila hatua hii ya kuuza kahawa ya Tanzania katika maduka makubwa Ulaya ni hatua ya kujipongeza.