Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?

Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?

Mstoiki

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2020
Posts
4,365
Reaction score
8,384
Habari wana JF, Kuna kitu kinanichanganya hapa;
Nikiangalia Mwanzo palikua na wanadamu wawili tu(Yaani Adam na Eva) na nnachojua Dunia haikua na binadamu mwingine yeyote alieumbwa zaidi yao hao wawili. Sasa najiuliza je, mtiririko wa Manabii na Vizazi vyote Walizaliana kindugu yaani kaka na dada? Au kuna watu wengine waliumbwa hawajatajwa kwenye biblia ndio hao wakawa wanaoana na hawa waliozaliwa na Adam & Eva. Je biblia inaruhusu kuoana ndugu? Kama hairuhusu, Je vizazi toka Kuumbwa kwa Adamu walizaliana kwa mfumo upi ikiwa hakukuwa na watu wengine zaidi ya hao wawili?

PITIA;
MWANZO 4:17 "Kaini akamjua mkewe, Naye akapata mimba, akamzaa Henoko; Akajenga mji akauita Henoko, Kwa jina la mwanawe"

Tuanzie hapo Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi huyo mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?
Screenshot_20220304-082240_Chrome.jpg
 
Haya mambo ndugu yangu tulishayajadiri sana humu. Na hayakupata mwafaka. Kwanza adam na hawa siyo binadamu wa kwanza kuwepo duniani bali niwakwanza kuumbwa kiroho na mungu jehova. Ukumbuke mamungu wapo kibao ila huyu yehova baba wa yesu naona kwa sasa ndo maarufu sana kutokana na kuwaongeza maujanja wafuasi wake wakatunza maandishi
 
Uyo mungu anataka damu Sana haiwezekeni ukatae mazao ya shamba alafu ukubali nyama, Tena yakuteketezwa kikatili mno.

Kaini alienda na dadake, ndio Mana alimlilia MUNGU kua adhabu yake nikubwa, hasinge weza kwenda pekehe.
 
Habari wana JF, Kuna kitu kinanichanganya hapa;
Nikiangalia Mwanzo palikua na wanadamu wawili tu(Yaani Adam na Eva) na nnachojua Dunia haikua na binadamu mwingine yeyote alieumbwa zaidi yao hao wawili. Sasa najiuliza je, mtiririko wa Manabii na Vizazi vyote Walizaliana kindugu yaani kaka na dada? Au kuna watu wengine waliumbwa hawajatajwa kwenye biblia ndio hao wakawa wanaoana na hawa waliozaliwa na Adam & Eva. Je biblia inaruhusu kuoana ndugu? Kama hairuhusu, Je vizazi toka Kuumbwa kwa Adamu walizaliana kwa mfumo upi ikiwa hakukuwa na watu wengine zaidi ya hao wawili?

PITIA;
MWANZO 4:17 "Kaini akamjua mkewe, Naye akapata mimba, akamzaa Henoko; Akajenga mji akauita Henoko, Kwa jina la mwanawe"

Tuanzie hapo Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi huyo mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?View attachment 2138134
Ni hivi.

Adam na Eva si watu wa kwanza.

Ni watu wa kwanza katika historia ya mapokeo ya jamii ya Wayahudi.

Na Wayahudi zamani hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.

Kihistoria watu walitokea Afrika, hao Wayahudi historia yao iliyoandikwa imeandikwa kuanzia takriban miaka 6,000 tu.

Huku Afrika kulikuwa na watu miaka mingi sana kabla ya hiyo.

Kwa hiyo.

1. Adam na Hawa si watu wa kwanza.
2. Adam na Hawa ni watu wa kwanza katika historia za mapokeo ya Wayahudi.
3. Wayahudi wa zamani, kama makabila mengine mengi, hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.
4. Kuna watu tofauti ya Wayahudi walikuwa wanaishi pembeni ya sehemu waliyoishi Wayahudi.
5. Habari ya Adam na Eva si habari ya watu wa kwanza, ni habari ya jamii iliyobadilika kutoka hunters and gatherers kwenda kilimo na ufugaji.

Kwa habari zaidi, tafuta kitabu " How To Read The Bible: A Guide To Scipture Now And Then" cha Dr. James Kugel.
 
Ni hivi.

Adam na Eva si watu wa kwanza.

Ni watu wa kwanza katika historia ya mapokeo ya jamii ya Wayahudi.

Na Wayahudi zamani hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.

Kihistoria watu walit9kea Afrika, hao Wayahudi historia yao iliyoandikwa imeandikwa kuanzia takriban miaka 6,000 tu.

Huku Afrika kulikuwa na watu miaka mingi sana kabla ya hiyo.

Kwa hiyo.

1. Adam na Hawa si watu wa kwanza.
2. Adam na Hawa ni watu wa kwanza katika historia za mapokeo ya Wayahudi.
3. Wayahudi wa zamani, kama makabila mengine mengi, hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.
4. Kuna watu tofauti ya Wayahudi walikuwa wanaishi pembeni ya sehemu waliyoishi Wayahudi.
5. Habari ya Adam na Eva si habari ya watu wa kwanxa, ni habari ya jamii iliyobadilika kutoka hunters and gatherers kwenda kilimo na ufugaji.

Kwa habari zaidi, tafuta kitabu " How To Read The Bible: A Guide To Scipture Now And Then" cha Dr. James Kugel.
Mkuu Kiranga shikanoo

Huko USA sasa hivi ni saa ngapi?
 
Mara nyingi watu wenye nia mbaya na Biblia huuliza swali hili,
“ikiwa Adamu na Hawa walikuwa na wana wawili, Kaini na Abeli, mke wa Kaini alitoka wapi?” Swali hili lina-ulizwa ili tu kuwa-vuruga watu, na kujaribu kuonyesha kwamba Biblia si kitabu cha Mungu kwa kuwa ina makosa!Hata hivyo niseme wazi,Biblia haina makosa,na inaji-tosheleza kabisa katika kujibu swali hili na mengine kwa ufasaha na kwa njia inayofaa.

Katika Mwanzo sura ya 3 na ya 4 tunapata habari zifuatazo: (1) Hawa alikuwa mama wa kila mtu anayeishi.(2) Muda fulani ulipita kuanzia wakati Kaini alipozaliwa mpaka wakati alipotoa dhabihu ambayo ilikataliwa na Mungu. (3) Baada ya kufukuzwa na kuwa mwenye kutanga-tanga na mkimbizi, Kaini alikuwa na wasiwasi kwamba huenda mtu yeyote akakutana naye na kujaribu kumuua. (4) Mungu aliweka ishara ya kumlinda Kaini, jambo lililo-onyesha kwamba ndugu au dada zake, au watu wengine wa ukoo wange-jaribu kumuua. (5) Baadaye Kaini alilala na mke wake katika nchi ya Ukimbizi(Mwanzo 3:20; 4:3, 12, 14-17)
Kutokana na habari hizo, tunaweza kusema kwamba mke wa Kaini, ambaye haijulikani alizaliwa wakati gani, alikuwa uzao wa Hawa. Andiko la Mwanzo 5:4 linasema kwamba katika miaka 930 ambayo Adamu aliishi, alizaa wana na mabinti. Biblia haisemi wazi mke wa Kaini alikuwa binti wa Hawa. Hata hivyo, kwa kuwa mke wa Kaini anatajwa baada ya Kaini kufukuzwa, jambo hilo linaonyesha kwamba wakati wa kutosha ulikuwa umepita na angeweza kuwa mmoja wa wajukuu wa Adamu na Hawa. Kwa hiyo, tafsiri ya Biblia The Amplified Old Testament inasema tu kwamba mke wa Kaini alikuwa “mmoja wa watoto wa Adamu.”
Mfafanuzi wa Biblia wa karne ya 19 Adam Clarke, alionelea kwamba hatua ya Mungu ya kuweka ishara kwa sababu Kaini aliogopa kuuawa, ilitokana na kuwapo kwa vizazi kadhaa vya wazao wa Adamu,vizazi vingi vya kutosha “kuanzisha vijiji kadhaa!”

Wazo la kwamba Kaini alimwoa dada yake au mzao wa baadaye wa Adamu kupitia mmoja wa wana au mabinti zake, ni jambo lisilokubalika katika jamii fulani leo. Sababu ni kuwa jamii hizo huliona kuwa jambo lisilo-kubalika au huogopa kwamba litasababisha kasoro za kimaumbile. Hata hivyo, F. LaGard Smith anasema hivi katika kitabu The Narrated Bible in Chronological Order: “Inaelekea kwamba ndugu na dada hao wa karibu walioana ingawa ndoa kama hiyo ingeonekana kuwa jambo lisilofaa katika vizazi vya sasa.” Inafaa kuzingatia kwamba ngono kati ya watu wa ukoo haikukatazwa wazi-wazi mpaka Musa alipopokea sheria za Mungu kwa ajili ya taifa la Israeli mwaka wa 1513 K.W.K(Mambo ya Walawi 18:9, 17, 24).

Leo, maelfu ya miaka imepita tangu wazazi wetu wa kwanza wapoteze ukamilifu wao. Huenda matatizo yanayotokana na chembe za urithi leo hayange-wapata. Isitoshe, uchunguzi wa hivi karibuni, kama ule uliochapishwa katika jarida Journal of Genetic Counseling, unaonyesha kwamba watoto wanaozaliwa katika ndoa kati ya binamu wa karibu, hawana kasoro nyingi za urithi kama inavyowaziwa na wengi. Kwa kweli, hayo hayangekuwa mambo yenye kutia wasiwasi mwingi siku za Adamu au hata kabla ya siku za Noa. Kwa hiyo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba mke wa Kaini alikuwa mmoja kati ya watu wake wa ukoo.
 
Ukweli upo hivi Adam na Hawa walikuwa si Binadamu wa Kwanza. Adam na Hawa walikuwa ni Hudi na Mkewe Jemi ambao walijulikana kama Adam (hudi) na Hawaii (jemi) ambaye ndie Hawa

Hudi alikimbia Kutoka lagahindi (India [emoji1128]) akakimbilia Huba ya Waajemi na Mkewe Jemi. Baada ya mkewe Jemi kupata Shida katika Uzazi Hudi Alimuona Sharka kama Mkewe wa Pili na Akazaa Watoto 12.Kama Vile
Adinai..alheri..Jehovam..Akwar..Tagra..Mathoni..Owarios..Gingua..Janaa..Atitanamus..Gabros..Zariatinatimike walizaliwa Daburi Ambayo sasa ni Israel.
 
Mwanzo 5:1 “Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
2 mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
3 Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi”
Lakini pia Biblia haiishi hapo, inasema Adamu alizaa watoto wengine wakiume na wakike baada ya kumzaa Sethi.

Mwanzo 5:4 “Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake”.
Na hao watoto wakike waliozaliwa ndio waliokuja kuwa wake wa hao watoto wengine wa kiume wa Adamu.

Hivyo Biblia haitoi idadi kamili ya watoto wa Adamu, pengine walikuwa 5 au 10 au 20 au 30, hatujui lakini zaidi ya Sethi, walikuwapo pia watoto wengine wa Adamu ambao habari zao hazikuandikwa katika biblia.

ADAMU ALIISHI MIAKA MINGAPI?

Jibu tunalipata katika Mstari wa 5

Mwanzo 5:5 “Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.”
Kwahiyo siku zote za Adamu ilikuwa ni miaka 930, akafa.
 
Kwa mjibu wa vitabu ambavyo havikuwekwa kwenye biblia kain alimuoa dada ake.

Pili biblia imeandikwa na watu ambao kwa mila zao mtoto wa kike alikuwa hahesabiki katika uzao wao. Kwaiyo wenda adam na hawa walikuwa na watoto wengne wa kike ambao hawakuhesabiwa kwenye uzao wao ambamo humo humo Kaini alijitwalia mke.
 
Biblia inasema katika kitabu cha Mwanzo.

Mtoto mwingine aliyezaliwa na Adamu na Hawa alikuwa ni Sethi.

Lakini pia Biblia haiishi hapo, inasema Adamu alizaa watoto wengine wakiume na wakike baada ya kumzaa Sethi.

Na hao watoto wakike waliozaliwa ndio waliokuja kuwa wake wa hao watoto wengine wa kiume wa Adamu.

Hivyo Biblia haitoi idadi kamili ya watoto wa Adamu, pengine walikuwa 5 au 10 au 20 au 30, hatujui lakini zaidi ya Sethi, walikuwapo pia watoto wengine wa Adamu ambao habari zao hazikuandikwa katika biblia.

ADAMU ALIISHI MIAKA MINGAPI?

Jibu tunalipata katika Mstari wa 5

Kwahiyo siku zote za Adamu ilikuwa ni miaka 980, akafa.
930 au 980?
 
Haya mambo ndugu yangu tulishayajadiri sana humu. Na hayakupata mwafaka. Kwanza adam na hawa siyo binadamu wa kwanza kuwepo duniani bali niwakwanza kuumbwa kiroho na mungu jehova. Ukumbuke mamungu wapo kibao ila huyu yehova baba wa yesu naona kwa sasa ndo maarufu sana kutokana na kuwaongeza maujanja wafuasi wake wakatunza maandishi
Duuuh ngoja nipite
 
Back
Top Bottom