Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?

Habari wana JF, Kuna kitu kinanichanganya hapa;
Nikiangalia Mwanzo palikua na wanadamu wawili tu(Yaani Adam na Eva) na nnachojua Dunia haikua na binadamu mwingine yeyote alieumbwa zaidi yao hao wawili. Sasa najiuliza je, mtiririko wa Manabii na Vizazi vyote Walizaliana kindugu yaani kaka na dada? Au kuna watu wengine waliumbwa hawajatajwa kwenye biblia ndio hao wakawa wanaoana na hawa waliozaliwa na Adam & Eva. Je biblia inaruhusu kuoana ndugu? Kama hairuhusu, Je vizazi toka Kuumbwa kwa Adamu walizaliana kwa mfumo upi ikiwa hakukuwa na watu wengine zaidi ya hao wawili?

PITIA;
MWANZO 4:17 "Kaini akamjua mkewe, Naye akapata mimba, akamzaa Henoko; Akajenga mji akauita Henoko, Kwa jina la mwanawe"

Tuanzie hapo Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi huyo mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?View attachment 2138134
Iko hivi. Adamu na hawa walikiwa wakizaa watoto mapacha mapacha, mwanaume na mwanamke baada ya hapo pacha wa kike wa upande mmoja aataolewa na pacha wa kiume wa upande wa pili. Mfano pacha wa kike wa Abeli aolewe na Kain na pacha wa kike wa Kain aolewe na Abel. Kwa mfumo huu ndipo dunia ikajazwa. Shida iliibuka pale mmoja alipopata wivu na kutaka kumwoa pacha wake yeye mwenyewe. Ikapelekea chuki na hatimaye kuuana
 
Habari wana JF, Kuna kitu kinanichanganya hapa;
Nikiangalia Mwanzo palikua na wanadamu wawili tu(Yaani Adam na Eva) na nnachojua Dunia haikua na binadamu mwingine yeyote alieumbwa zaidi yao hao wawili. Sasa najiuliza je, mtiririko wa Manabii na Vizazi vyote Walizaliana kindugu yaani kaka na dada? Au kuna watu wengine waliumbwa hawajatajwa kwenye biblia ndio hao wakawa wanaoana na hawa waliozaliwa na Adam & Eva. Je biblia inaruhusu kuoana ndugu? Kama hairuhusu, Je vizazi toka Kuumbwa kwa Adamu walizaliana kwa mfumo upi ikiwa hakukuwa na watu wengine zaidi ya hao wawili?

PITIA;
MWANZO 4:17 "Kaini akamjua mkewe, Naye akapata mimba, akamzaa Henoko; Akajenga mji akauita Henoko, Kwa jina la mwanawe"

Tuanzie hapo Kaini ni mtoto wa Adamu, je alimpata wapi huyo mkewe ikiwa binadamu wa mwanzo walikua wawili?View attachment 2138134
Adam na Eva hawakuwa watu halisi, ni characters katika hadithi ya kutungwa ya Wayahudi.

Ukielewa hili, hayo maswali mengine yote yanaondoka.
 
Kwa mjibu wa vitabu ambavyo havikuwekwa kwenye biblia kain alimuoa dada ake.

Pili biblia imeandikwa na watu ambao kwa mila zao mtoto wa kike alikuwa hahesabiki katika uzao wao. Kwaiyo wenda adam na hawa walikuwa na watoto wengne wa kike ambao hawakuhesabiwa kwenye uzao wao ambamo humo humo Kaini alijitwalia mke.
Asee 🤔.. Huu mwaka nilistruggle sana na ishue za faith. A lot has taught me
 
Ukweli upo hivi Adam na Hawa walikuwa si Binadamu wa Kwanza. Adam na Hawa walikuwa ni Hudi na Mkewe Jemi ambao walijulikana kama Adam (hudi) na Hawaii (jemi) ambaye ndie Hawa

Hudi alikimbia Kutoka lagahindi (India [emoji1128]) akakimbilia Huba ya Waajemi na Mkewe Jemi. Baada ya mkewe Jemi kupata Shida katika Uzazi Hudi Alimuona Sharka kama Mkewe wa Pili na Akazaa Watoto 12.Kama Vile
Adinai..alheri..Jehovam..Akwar..Tagra..Mathoni..Owarios..Gingua..Janaa..Atitanamus..Gabros..Zariatinatimike walizaliwa Daburi Ambayo sasa ni Israel.
Hii mpya 😂
 
Adam na Eva hawakuwa watu halisi, ni characters katika hadithi ya kutungwa ya Wayahudi.

Ukielewa hili, hayo maswali mengine yote yanaondoka.
Well said mkuu .. Naamini hivyo kwa sasa
 
Ni hivi.

Adam na Eva si watu wa kwanza.

Ni watu wa kwanza katika historia ya mapokeo ya jamii ya Wayahudi.

Na Wayahudi zamani hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.

Kihistoria watu walit9kea Afrika, hao Wayahudi historia yao iliyoandikwa imeandikwa kuanzia takriban miaka 6,000 tu.

Huku Afrika kulikuwa na watu miaka mingi sana kabla ya hiyo.

Kwa hiyo.

1. Adam na Hawa si watu wa kwanza.
2. Adam na Hawa ni watu wa kwanza katika historia za mapokeo ya Wayahudi.
3. Wayahudi wa zamani, kama makabila mengine mengi, hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.
4. Kuna watu tofauti ya Wayahudi walikuwa wanaishi pembeni ya sehemu waliyoishi Wayahudi.
5. Habari ya Adam na Eva si habari ya watu wa kwanxa, ni habari ya jamii iliyobadilika kutoka hunters and gatherers kwenda kilimo na ufugaji.

Kwa habari zaidi, tafuta kitabu " How To Read The Bible: A Guide To Scipture Now And Then" cha Dr. James Kugel.

Nakuelew nakuelewa
 
Kiranga kumbe maneno mengi ,ana kiboko yake humu ya maneno.
Sijawahi kushindana katika ujinga.

Kuna wajinga wengi tu nimewaweka ignore list, kwa sababu sipendi zogo nao.

A wise man once told me, don't argue with a fool. Cause people from a distance, can't tell who is who.

That is my right, and no amount of psychological trick is going to change that.

I choose who to engage. I don't just engage every dumb fuckery throwing yokel out there.

That's the difference between Kiranga and most of you.
 
Biblia haielezi kwa kina juu ya mke wa kaini kama alikuwa nani. Jibu linalotarajiwa ni kwamba mke wa kaini alikuwa dadake. Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao. Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye (mwanzo 5:4). Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili (mwanzo 4:14) inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana. Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana (mambo ya walawi 18:6-18). Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa. Kadri dunia inavyoendelea, vilema hivi vinaendelea kuzidi. Lakini Adamu na Hawa hawakuwa na kilema chochote ndani yao na ika sababisha jamii zao kuwa na afya njema sana kuliko yetu hivi sasa. Haifurahishi kuona ya kwamba mke wa Kaini alikuwa dadake. Kwa kuwa Mungu alianza na mke mmoja na mme mmoja, waliofuata hawakuwa na lengine ila kuoa dada zao.
 
Ni hivi.

Adam na Eva si watu wa kwanza.

Ni watu wa kwanza katika historia ya mapokeo ya jamii ya Wayahudi.

Na Wayahudi zamani hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.

Kihistoria watu walitokea Afrika, hao Wayahudi historia yao iliyoandikwa imeandikwa kuanzia takriban miaka 6,000 tu.

Huku Afrika kulikuwa na watu miaka mingi sana kabla ya hiyo.

Kwa hiyo.

1. Adam na Hawa si watu wa kwanza.
2. Adam na Hawa ni watu wa kwanza katika historia za mapokeo ya Wayahudi.
3. Wayahudi wa zamani, kama makabila mengine mengi, hawakuhesabu watu wa makabila mengine kuwa ni watu.
4. Kuna watu tofauti ya Wayahudi walikuwa wanaishi pembeni ya sehemu waliyoishi Wayahudi.
5. Habari ya Adam na Eva si habari ya watu wa kwanza, ni habari ya jamii iliyobadilika kutoka hunters and gatherers kwenda kilimo na ufugaji.

Kwa habari zaidi, tafuta kitabu " How To Read The Bible: A Guide To Scipture Now And Then" cha Dr. James Kugel.
Common sense
 
Guys mm ni mkristo, ila bibilia ni kitabu cha historia ya mambi ya kale kilichotungwa na binadamu, bibilia si kitabu cha mungu, yes sijakosea sio cha mungu, mungu hajaandika kitabu chochote, dini pia ndio uongo mkubwa kabisa uliowahi kufanywa na binadamu na watu wengi wameanguka humo mungu hana dini
adam sio binadam wa kwanza kuumbwa, ni kuwa tu aliyeandika hicho kitabu alimjua adam kabla ya jamii ingine, nna usingizi ngoja niishie hapa
 
Biblia haielezi kwa kina juu ya mke wa kaini kama alikuwa nani. Jibu linalotarajiwa ni kwamba mke wa kaini alikuwa dadake. Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao. Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye (mwanzo 5:4). Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili (mwanzo 4:14) inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana. Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana (mambo ya walawi 18:6-18). Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa. Kadri dunia inavyoendelea, vilema hivi vinaendelea kuzidi. Lakini Adamu na Hawa hawakuwa na kilema chochote ndani yao na ika sababisha jamii zao kuwa na afya njema sana kuliko yetu hivi sasa. Haifurahishi kuona ya kwamba mke wa Kaini alikuwa dadake. Kwa kuwa Mungu alianza na mke mmoja na mme mmoja, waliofuata hawakuwa na lengine ila kuoa dada zao.
Well said SweetyCandy .. Kama kweli ni "Ke" Hakika mmeo amepata/atapata mke Mwema.

God Bless you.
 
Guys mm ni mkristo, ila bibilia ni kitabu cha historia ya mambi ya kale kilichotungwa na binadamu, bibilia si kitabu cha mungu, yes sijakosea sio cha mungu, mungu hajaandika kitabu chochote, dini pia ndio uongo mkubwa kabisa uliowahi kufanywa na binadamu na watu wengi wameanguka humo mungu hana dini
adam sio binadam wa kwanza kuumbwa, ni kuwa tu aliyeandika hicho kitabu alimjua adam kabla ya jamii ingine, nna usingizi ngoja niishie hapa
Polepole mkuu... Yo're not alone. Life has taught me alot.
 
Biblia haielezi kwa kina juu ya mke wa kaini kama alikuwa nani. Jibu linalotarajiwa ni kwamba mke wa kaini alikuwa dadake. Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao. Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye (mwanzo 5:4). Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili (mwanzo 4:14) inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana. Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana (mambo ya walawi 18:6-18). Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa. Kadri dunia inavyoendelea, vilema hivi vinaendelea kuzidi. Lakini Adamu na Hawa hawakuwa na kilema chochote ndani yao na ika sababisha jamii zao kuwa na afya njema sana kuliko yetu hivi sasa. Haifurahishi kuona ya kwamba mke wa Kaini alikuwa dadake. Kwa kuwa Mungu alianza na mke mmoja na mme mmoja, waliofuata hawakuwa na lengine ila kuoa dada zao.
Huna uhakika.
 
Back
Top Bottom