Kajiandae; Balaa jipya toka kwa Ommy Dimpoz na Alikiba

Ngoma hii kali ukisikiliza mara nying kidogo utanielewa
 

[emoji23][emoji23][emoji23] hivi kumbe Salome ulisha chuja [emoji23][emoji23], no wonder siku hizi mtu akisema nyimbo ya Salome mimi namkumbuka Dully Sykes [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huu wimbo ni noma. Nimeukubali sana
Naupa namba moja katika nyimbo kali zilizotoka within the three months time
 
Mimi bado aiseeeee naona kama Ali siku hizi anazingua akishirikishwa kuanzia ule nisamehe ni kawaida ukija huu ni kawaida pia.

Hawa wanaomshirikisha Ali inabidi wajue sasa Ali sio wa kuimba verse bora wawe wanampa chorus na back vocal maana hizo ndio silaha zake.

Angalia Jike shupa au mbonga 7 kapiga fresh chorus zao ila akipewa verse lazima aboronge.

Wimbo sio mbaya ni wimbo wa kawaida...Nilidhani utakuwa mkali kuliko wa NaiNai ila imekuwa tofauti na iko wazi nguvu ya Ommy Dimpozi inazidi kwenda chini.
 
Bola jike shupa
Teh mmeshakuja..mwisho wa siku mtasifia nyimbo zake zote na alizoshirikishwa..kiba ni kama maji..usipoyanywa utayaoga!!
 
Nimetoka kuusikiliza bado sijauelewa,Ommy atafute shughuli nyingine ya kufanya na kiba kama aliipania sana hivi matokeo yake ameharibu. KAMA WIMBO WAKO HAKUNA UNACHOPATA KWA KUKAA YOUTUBE BASI YOUTUBE SI MUHIMU,ILA KAMA HUWA UNALIPWA BASI YOUTUBE MUHIMU SANA.
 
Sauti iko vzr, na wimbo hauchezeki kiviiiile in general ni ya kawaida sana, plus
watu wa light walizembea kuna sehem light imezidi sana kuliko kawaida
 
Kabisa Mkuu! Nahisi kama kiba alipania sana huu wimbo yani mpaka kwenye video amejichetua chetua kidizaini flani hivi tofauti na kawaida yake ya kuwa mtulivu kwenye video.. Kwa ufupi wimbo ni wa kawaida sana! Ommy dimpoz watu wamemsubiria sana alafu ndio anarudi kidizaini hii, aisee [emoji17] [emoji17]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…