Mmakedonia
Member
- Sep 1, 2021
- 21
- 12
Katika maisha yangu ya elimu kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne sikuwahi kushindwa darasani, mimi kwangu kupitwa katika mtihani nilichukulia ni zaidi ya tusi, baba yangu alinisifia akisema kwamba nina akili kama alizokua nazo yeye ijapokua hakua mtu wa kunipa mahitaji muhimu ambayo mtoto anatakiwa kupata kutoka kwa baba yake.
Kila shule ambayo nilisoma niliamini kwamba naweza kuliko wanafunzi wote hivyo ilikua sio rahis kwa mwanafunzi kunishinda, nakumbuka moja kati ya vitu vilivyonipa umaarufu katika shule niliyomaliza kidato cha nne ni kwamba hiyo shule ilikua ya mwisho mwaka fulani kitaifa (sitoutaja) lakini pia kwa miaka minne mfululizo haikuwahi kufaulisha mwanafunzi yeyote lakini mwaka nilio kuwa mimi kidato cha nne Mungu alisaidia tukafaulu wanafunzi wanne huku wenzangu watatu wakipelekwa vyuo vya kati na mimi peke yangu nikachaguliwa kwenda Advance (PCM)
Kutokana na hali ya wazazi kutokujali kwao kuhusu elimu ijapokua ni kweli kwamba katika kipindi hicho walikua wameshaanza kuchoka ( kuishiwa pesa) hivyo sikubahatika kusoma hata pre-form five lakini nilijipa moyo kwamba ninaweza kufanya kitu cha tofauti licha ya ugumu wa masomo husika.
Hali ilikua tofaut baada ya kuingia kidato cha tano na kukutana na watu waliosoma twishen na ambao wapo bora kuliko mimi, kila nikijaribu kusoma nilikua nikipaniki baada ya kuona kuna watu wana uwezo kuliko mimi ila nilijipa imani kuwa nitashinda na nitafaulu japo kua mambo yalikua magumu sana kwa upande wangu.
Nilikuja kuamini kua ni kweli "ng'ombe wa maskini hazai" baada ya kumaliza kidato cha sita na matokeo kutoka nilikua na div 3 ya 15 yaani kila somo nilikua na "E" hivyo nilikua sina "principal pass" za kuniwezesha kwenda chuo, mara gafla kauli zikabadilika mtaani wale walio nisifu wote wakaanza kunikebehi kwamba nilienda kucheza shule (lakini hakuna mtu yoyote aliyenipa msaada kipindi nasoma hadi kuna kipindi nilikua nakosa hata ela ya kununulia sabuni ya kufulia)
Nikiangalia hali ya wazazi wangu ni ngumu na wote wamezeeka kwa sasa ( walitengana ningali bado mdogo sana hivyo malezi yangu muda mrefu nilipata kwa mama zangu wa kambo ambao baba aliwaleta nyumbani) naona kama nipo kwenye msitu wenye giza nene sioni njia ya kutokea kwani hakuna pa kupata msaada.
Mtu mmoja akanishauri niombe nafasi kwenye vyuo vya serikali ili nikipata nikaombe udhamini kwenye makampuni binafsi lakini mimi mtoto wa maskini sina anaenijua huko serikalini hivyo juhudi zangu ziligonga mwamba kwani nimeomba nafasi lakini bado nimekosa baada ya matokeo ya vyuo kutoka. Only God know ... Nimebakiza dua na sala tu walau nisikose ata mkate wa kila siku🙏. (This is my real life not story)
Naomba pia kura yako hapo hapo chini 👇👇👇 kwa kubofya hilo neno "vote" kama hautojal