Habari wanajukwaa,
Jana wale vijana wenye uwezo wa kuburudisha, kufundisha na kuhamasisha (ROMA + STAMINA = ROSTAM) waliachia wimbo uliozua gumzo kwa ujumbe na ubunifu uliopo ndani yake.
Kuna mistari (mashairi) fulani wanasema hivi -:
R.O.M.A: Nasikia Koyu Keza Mbochi
STAMINA: 'Mano Likwelikwe'
Kama mnakumbuka kuna mchezo ulikuwepo sana mashuleni, yaani watu wanaongea maneno kwa kinyume ili kumficha muhusika au watu wasielewe haraka.
Hivyo hapo walimaanisha hivi-:
R.O.M.A: 'Nasikia Yuko Zake Chimbo'..
STAMINA: 'Noma Kwelikweli'
Je walikuwa wanamsema Nani?
Msafwa,
Uporoto, Mbeya