Kaka yangu amechomwa Moto kwa kudhaniwa ni mwizi

Sawa kaenda sehemu hajulikani, nmekubali.

Vipi suala la kumpiga mpk kumchoma,
Unataka kunambia walimkuta wakapiga tu Bila hata kumhoji?

Mbona haiingii akilini?

Uku kwetu mbona wehu na vichaa mbalimbali wanazurura mji mpk mji na hatujawai sikia kesi ya mwehu au kichaa kauwawa bahati mbaya akidhaniwa Ni mwizi?

Unajua nikwambie kitu mkuu,
Hapo huwez pata sapoti yoyote ile.

Hata hao polisi wenyewe ulikoenda kushtaki washawachoka hao wezi na Vibaka, wanawaharibia kazi yao.

Ndo maana kesi za vibaka kuuwawa na Sungu Sungu huwa hazna Nguvu kabisa hata uende ikulu maana serikali yenyewe inajua kabisa wezi ndo Hawa Hawa tunaioshi nao.

Na wazazi ndo Kama nyie mnaowafuga.

Na sungusungu na viongozi wanawajua wezi wanaosumbua mtaa.

Hiyo kesi achana nayo mkuu, Fanya tu ishu nyingine.
 

Kaka huyo mtu hana akili vizuri, kama wewe ushaishi kitaa hawa watu wenye matatizo ya akili anaweza kupita mbele ya nyumba yako akachukua chochote anachokiona si kwa sababu ni mwizi ila hana ufahamu wa kuishi na watu wengine kama wewe

Inawezekana ndio situation iliyomkuta jamaa na uwezo wa kujitetea hana na sungusungu uwezo wa kumuelewa hawana
 
Wewe mbona umemkalia kooni mwenzio kwamba huyo ndugu yake alikuwa mwizi vipi yule aliyeuliwa Mtwara alikuwa na kosa gani hata wewe unaweza kuuliwa kwa kuitiwa kelele za mwizi acha ujuaji hii Dunia kuna mauwaji yanauotokea ukihadithiwa huwezi amini kama wewe
 
Alafu jamaa anaongea utafikir hatuwajui tabia za sungu sungu ni washenz sana hao jamaa ndo wakabaji wenyewe hao wakikuta usiku..
 
Acha roho mbaya sheikh.. haya jamaa kashapoteza ndugu yake na ww umefaidika nn sasa!!
Kesi anavyoielezea haiingii akilini kabisa, hata wewe Apo.

Hata Kama humjui mtu, huwez mkuta kwako ukaanza kumshambulia mpk kumchoma Moto Bila kua na uhakika kua Ni mwizi.

Haiingii akilini eti
Uyo Mpk anafikia kuchomwa Moto anaiungua anateketea maana ake alikosa kabisa hata mmoja tu wa kumtetea Wala kuita polisi asaidiwe.

Pale inavoonesha alikutwa ready handled.

Unajua mkuu hizi kesi za upande mmoja hasa matukio ya wizi Kama haya,
afu zinazohusisha ndugu wa damu huja na hoja nyepesi nyepesi zilizokaa kiutetezi Sana ili kusaka huruma ya jamii.

Ifike mahala, tuweke ubinadamu pembeni tuwaze beyond the box.

Vinginevyo unambie hujawai ibiwa na ukapeleka mwizi polisi, akarudishwa mtaani.
 
Tujijue WaTz kwa sasa tunaongoza kwa roho mbaya ya ukatili! Hii katiba mpya ihakikishiwe haki ya mtu na utu wake (uhai), vinalindwa na ni marufuku mtu mwingine kujichukulia uamuzi wa kuutoa uhai wa mwingine, haijalishi kafanya kosa gani.
 
Poleni sana!
 
Alafu jamaa anaongea utafikir hatuwajui tabia za sungu sungu ni washenz sana hao jamaa ndo wakabaji wenyewe hao wakikuta usiku..
Sungusungu wengi wanachukuliwa randomly Tu mkuu, hakuna kigezo au mafunzo yoyote ya kumuandaa mtu. Japo wanaleta unafuu kwenye mitaane ila ukikutana nao usiku na hawakujui lazma wazae na wewe
 
ficha ujinga wako we kenge
 
Ila wewe jamaa bana na vistori vyako vya michepuko kumbe ndio tahira ivo.?
 
Kaka,
Hicho kipimo Cha kumpima mtu huo utimamu wake wa akili usiku wa manane na nmeshamkamata ready handled na mali yangu kaniibia nakipata wapi?

Hebu vingine jiongeze mwnyw, ungelikua wee unafanyaje?
 
Mkuu tumia busara, jamaa amesema Kaka yake alikuwa na Down's Syndrome, maana yake alikuwa mlemavu, na mtu wa aina hii anahitaji mwangalizi muda wote. Na ukimuona tu mtu mwenye downs syndrome unamtambua tu. Sasa hukumu unayotoa ni halali kweli?!
 
Tujijue WaTz kwa sasa tunaongoza kwa roho mbaya ya ukatili! Hii katiba mpya ihakikishiwe haki ya mtu na utu wake (uhai), vinalindwa na ni marufuku mtu mwingine kujichukulia uamuzi wa kuutoa uhai wa mwingine, haijalishi kafanya kosa gani.
Siku hizi ukipiga yowe ya mwizi,
mwizi mwnyw anawakimbia raia na anajipeleka mwyw polisi.

Siku mbili kushapoa, anaruhusiwa aanrudi Tena uraiani.

Maana ake polisi Ni sehemu salama Sana kwa wezi na Vibaka.
 
Sasa ww ushaambiwa jamaa anamatatzo ya akili na alikuwa anafungiwa ndan bahat mbaya akatoroka.. bado unajitoa uelewa.. angekuwa mzima wa akil nisingetilia mashaka sana
 
Nasemaga humu tuache kujichukulia sheria mkononi jamani, tena hao ni sungusungu kabisa, hata kama mtu kaiba kweli, adhabu ya kuchoma mtu moto ni kali sana, haiendani na kosa hiko hata kidogo!!!
 
Na wakati mwingine Ni wavuta bangi waliokubuhu wanawabandika Majina ya walemavu wa Akili.. Ana cheti Cha Daktari kuthibitisha ulemavu??

Sungusungu wa Mtaa husika wasimjue huyo Kaka yake??
 
Mkuu tumia busara, jamaa amesema Kaka yake alikuwa na Down's Syndrome, maana yake alikuwa mlemavu, na mtu wa aina hii anahitaji mwangalizi muda wote. Na ukimuona tu mtu mwenye downs syndrome unamtambua tu. Sasa hukumu unayotoa ni halali kweli?!
Mkuu,
Mimi Ni mwelewa Sana.

Kwa kesi Kama hiyo sidhan Kam anatakiwa kwenda mahakamani kushtaki watu.

Maneno Ni magumu Sana,
Ila Ni Lazima TU yasemwe,

Uyo mtoa mada ahesabu tu Ni bahati mbaya iyo ndugu yake kafariki.

Kama vile alivyo mlemavu ambavyo angefariki kwa ajali ya kugongwa barabarani au railway crossing.

Wakulaumiwa ni waangalizi wake hao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…