Kaka yangu anaelekea kuoa bomu, nimnusuru vipi?

Kaka yangu anaelekea kuoa bomu, nimnusuru vipi?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Huyu mwanamke nimemfahamu mwaka jana mwezi wa pili jijini Dar. Kila siku nilimkuta kwenye bar X yenye jina kubwa tu hapa Dar. Hakuwa mhudumu, bali alipretend kuwa mteja, kiuhalisia alikuwa anauza japo kwa kutumia akili pana sana! Alikaa kwenye moja ya meza mle bar akiwa katika mavazi na mikao ya kimtego huku vidole vyake vyenye kucha ndefu za kizungu vikibofya screen ya simu yake, ndipo ungelijitokeza na kuanza mazungumzo naye, ungempatia pesa si chini ya 30k na bia za kumlewesha, kiulaini ungevuta chombo guest, maana zilikuwa mle mle kwa hotel. Kusema ukweli, hata mimi mwenyewe niliwahi kumchakata mara mbili tena kwa kukesha naye usiku kucha. Hakika anayajua mauno, anaijua miguno.

Mwezi wa saba mwaka huu nilienda kutembelea nyumbani Mwanza, ndipo kumkuta kaka yangu tayari kashafika. Safari hii alikuwa na binti mrembo asiye na mfano wa kufananishwa naye(yule yule binti). Nilipigwa butwaa mara ya kwanza nilipoonana nae, lakini licha ya kushangazwa kumkuta pale nyumbani, yeye binafsi hakunikumbuka kabisaa, wala kunivutia hata picha, tulisalimiana tu kibinadamu zaidi na ndipo dakika chache kaka yangu alinitambulisha kwa huyo binti. Ndipo ushemeji ukaanzia hapo. Nilithibitisha hili baada ya kuona hata mama yetu yuko serious kwenye mahusiano ya mwanae, huyu binti ndiye aliyekuwa anatupikia chakula pale nyumbani, hakika ni fundi pia wa mapishi jikoni.

Huyu binti anaonekana wazi kuwa tayari kashabadili mfumo wake wa kale wa maisha, kwa sasa ni mtu wa kusoma vijitabu vya ki Mungu Mungu i.e mnara wa mlinzi, kuangalia katuni sana na tamthiliya za star swahili. Simu yake haina password, pia yuko huru kuiacha sebuleni bila kuhofia chochote. Kuna siku nilikuwa nikimtazama na kumwongelesha kwa mtindo ule ambao niliutumia kipindi kile, ili ajigundue kuwa yeye ni nani aachane na kaka, lakini ndio kwanza hanikumbuki wala hakumbuki chochote.

Msaada wakuu, jinsi gani nitamnusuru kaka na huyu mwanamke? Shida sio kutafunwa na wanaume wengi, ila tatizo ni kuwa na mimi nishawahi kumtafuna mara mbili, tena kwa kumtangulizia pesa mbele! Nahisi namvua utu na heshima kaka yangu. Na kama watafanikisha, nahisi kuna siku nitapasha kiporo tu, kwa sababu namfahamu fika huyu binti.

Msaada tafadhari!
 
Yamkini umemfananisha au alikesha Kawe kaamua kumrudia Mila wake 😂😂
 
Huyu mwanamke nimemfahamu mwaka jana mwezi wa pili jijini Dar. Kila siku nilimkuta kwenye bar X yenye jina kubwa tu hapa Dar. Hakuwa mhudumu, bali alipretend kuwa mteja, kiuhalisia alikuwa anauza japo kwa kutumia akili pana sana! Alikaa kwenye moja ya meza mle bar akiwa katika mavazi na mikao ya kimtego huku vidole vyake vyenye kucha ndefu za kizungu vikibofya screen ya simu yake, ndipo ungelijitokeza na kuanza mazungumzo naye, ungempatia pesa si chini ya 30k na bia za kumlewesha, kiulaini ungevuta chombo Guest, maake zilikuwa mle mle kwa hotel. Kusema ukweli, hata mimi mwenyewe niliwahi kumchakata mara mbili tena kwa kukesha naye usiku kucha. Hakika anayajua mauno, anaijua miguno.

Mwezi wa saba mwaka huu nilienda kutembelea nyumbani Mwanza, ndipo kumkuta kaka yangu tayari kashafika. Safari hii alikuwa na binti mrembo asiye na mfano wa kufananishwa naye (yule yule binti). Nilipigwa butwaa mara ya kwanza nilipoonana nae, lakini licha ya kushangazwa kumkuta pale nyumbani, yeye binafsi hakunikumbuka kabisaa, wala kunivutia hata picha, tulisalimiana tu kibinadamu zaidi na ndipo dakika chache kaka yangu alinitambulisha kwa huyo binti. Ndipo ushemeji ukaanzia hapo. Nilithibitisha hili baada ya kuona hata mama yetu yuko serious kwenye mahusiano ya mwanae, huyu binti ndiye aliyekuwa anatupikia chakula pale nyumbani, hakika ni fundi pia wa mapishi jikoni.

Huyu binti anaonekana wazi kuwa tayari kashabadili mfumo wake wa kale wa maisha, kwa sasa ni mtu wa kusoma vijitabu vya kimungu mungu i.e Mnara wa mlinzi, kuangalia katuni sana na tamthiliya za star swahili. Simu yake haina password, pia yuko huru kuiacha sebuleni bila kuhofia chochote. Kuna siku nilikuwa nikimtazama na kumwongelesha kwa mtindo ule ambao niliutumia kipindi kile, ili ajigundue kuwa yeye ni nani aachane na kaka, lakini ndio kwanza hanikumbuki wala hakumbuki chochote.

Msaada wakuu, jinsi gani nitamnusuru kaka na huyu mwanamke? Shida sio kutafunwa na wanaume wengi, ila tatizo ni kuwa na mimi nishawahi kumtafuna mara mbili, tena kwa kumtangulizia pesa mbele! Nahisi namvua utu na heshima kaka yangu. Na kama watafanikisha, nahisi kuna siku nitapasha kiporo tu, kwa sababu namfahamu fika huyu binti.

Msaada tafadhari!
Sio wote wanapenda kuwa malaya na kujiuza, kuna Mazingira wanakutana nayo! Ila wengi ubadilika na kuwa wema na waaminifu kwenye Ndoa, Maisha ni Fumbo wapo walioolewa wakaja kuwa malaya ndani ya Ndoa! Wapo walioolewa malaya wakaja kuwa wake Bora kwenye Ndoa. Nna jamaa zangu zaidi ya 3 wameoa hawa watu wa aina hii na wengine wana wajukuu sasa na wametulia kwenye ndoa zao!Kumbuka Kama Yesu aligeuza Maji kuwa Divai hakika Mungu anaweza badili Mtu
 
Kama ni kweli usemayo basi jivike mabomu umueleze kaka yako kila kitu,nasisitiza tena kila kitu hata suala la kumchakata mueleze,yabaki maamuzi yake tu.
 
Anakukumbuka. Anasubiri tu afunge ndoa kwanza. Mwambie kaka yako mavi ya kale hayanuki, shemeji ni mavi ya kale.
 
Wewe uliyemuoa anajua umewahi nunua malaya?

Na wewe uliyemnunua huyo shemeji ako, na yeye aliyekuwa anauza mna tofauti gani?

Kikubwa hapo kwa kuwa hakukumbuki basi vunga, na hakikisha hatokaa ajue maana the moment ukimuambia jua umeshaharibu kila kitu na hatakuwa na amani tena na mtakuwa hamuivi naye.

Binadamu huwa wanabadilika. Unaweza ukaoa mcha Mungu lakini baadaye akawa malaya wa kutupwa anagawa uroda mtaa kwa mtaa. Na unaweza ukaoa malaya lakini akakutulizia ndoa yenu mpaka ukashangaa mwenyewe.
 
Kama anaonekana kubadilika kweli na siri unaijua wewe pekee yako, vunga acha bro wako aendelee na maisha yake. Halafu kkaa mbali na shemeji yako.
Kila mtu anahitaji nafasi ya pili

Unaweza kuta wapo mapacha.
 
Back
Top Bottom