Kaka yangu kaforwadiwa ujumbe huu kwenye simu, afanyeje?

ndiyo mke kwanza maana zile sarakasi pale kwa bed ananeng'eneka peke ake
 
Duuh huyo kama shemeji yangu mimi,nomaa hata salamu hataki
 
Wengi mmemtuhumu huyo mwanamke wamba ni mchoyo, mbinafsi, ana roho ya kimaskini n.k. Binafsi napenda kutofautiana nanyi. Nadhani huyu yako sahihi kwa asilimia nyingi sana. Nadhani mke yeyote ambaye anaelewa nafasi yake anasisitiza sana jambo hili.

Nilivyoelewa mimi huyu mke/mwanamke having kusaidia ndugu za mume bali anachohitaji ni kutambuliwa na kuheshimiwa nafasi yake kama mke. Kiufupi, kama tunakubaliana kuwa mume ni "kichwa cha nyumba", basi mwanamke ndiye "shingo ya nyumba" na familia ni "kiwiliwili".

Mleta mada mwambie brother wako amshirikishe mkewe katika mipango na mikakati mbalimbali ya maendeleo na ya kusaidia ndugu. Asimsirikishe mtu yeyote kabla ya mkewe na wala asifanye pekeyako. Hii inaweza ikaleta chuki na kutoelewana kati ya mume na mke, mke na ndugu na baadae mume na ndugu. Kama kweli anataka familia imara hilo halikwepeki. Leo tupo lakini hatuna uhakika na kesho.
 
Huyo bado girlfriend, kwahiyo asiwatishe. Hata hivyo kama ndiye kaka yenu.keshaamua kumuoa.mkae chonjo.maana manaweza kosa mlichokuwa mnakipata toka kwa kaka.
 
endelea na msimamo huo ndugu ni mzuri sana. Ila baadae usirudi tena hapa kuomba ushauri baada ya kushindwa kwenda kwa ndugu zako kuomba msaada kwa kuwa uliwanyima slot katika familia yako
 
Mama yako miezi tisa, uchungu wa leba, na miaka 2 ya kukunyonyesha alineng'eneka na nani??
haijalishi mama ana thamani yake kubwa tu!Ila asiwe kigezo cha kumnyima furaha mtoto wake
ndo maana tunaambiwa tunawaacha wazazi wetu kuanza upya wawili!!
sisemi asimhidumie ile mke ana nafasi yake na mzazi ana nafas yake
kuna wakwe wengine hekima zero kabisa ktk ndoa za watoto wao na kama wataka mwanao asiwe guru na maisha yake basi kaa nae km mapambo tu !Ila akioa jua mke ndo mshauri wake mkuu and everything as long as mke nae anajua maana ya mke
 
mtu anapoamua kuoa ama kuolewa haimaanishi asisaidie familia yake alikotoka! ila lazima wanafamilia mjue kuwa habari za kutegemeana hazipo...watu wanatakiwa wafanye kazi !...waache habari za dada mara kaka! mara watoto wa kaka awasomeshe mwenye uwezo! kwann alizaa sasa?...
 
Wanachelewesha maendeleo hizo hela ni zake hivi huyo mwanamke anajua uchungu wa huyo mumewe zaidi ya ndugu zake walio hangaika nae? Hivi alimsomesha?

Yani mtu mmekutana ukubwani halafu unataka aache kuwasaidia nduguze.

Wanawake mmeumbwa na ubinafsi wa hali ya juu sana na unaweza kukuta huyo jamaa ana wasaidia ndugu wa mwanamke lakini kuona mumewe anasaidia wa kwake basi ni nongwa.

Ukweli ni kwamba mwanamke anaye pambana kumtenganisha mumewe na ndugu huwa hafanikiwa na hata akifanikiwa ni kwa muda na mara nyingi hukimbilia kwa waganga.

Wanawake wa aina hii hawana tofauti na wachawi na wao kwenda kwa waganga ni kawaida.
 
Roho mbaya ya ubinafsi ki africa Africa kusaidiana muhimu aiseee
Mimi huwa nashangaa wanawake mlio wengi sijui kwanini mnakumbwa na huu ugonjwa? Hivi mtu mmekutana ukubwani wala hujui makuzi yake au watu walihangaika vipi jamaa kusoma au lah lakini unakuja na kutafuta sababu za kuwatenganisha ndugu.. Hivi kwani wengi wenu huwa hamjaribu kuvaa viatu vya ndugu hao..?
 
Sasa na yeye ofisini ameshatangaza mume wake kibosile, pesa ya kubadilishia gari unaambiwa ni ada ya mdogo wangu, kule alikotangaza ufalme heshima itashuka mkuu.
 
Wewe ni mwanamke? Umeolewa? Yani mimi nikitaka kusaidia ndugu zako nikae kikao na mke wangu? Hahahahaha Kamwe kama kuna mwanaume ana fanya hivyo ujue ana tatizo kubwa.

Ukisha mpa nafasi mwanamke wako kushiriki kwenye maamuzi ya kusaidia nduguzo na wazazi wako ujue kuna tatizo kubwa na kamwe hutowasaidia kamwe.

Ukitaka kujua mwanamke ni mchawi basi utamsikia akikwambia kuwa ukitaka kumsaidia ndugu au mzazi wako nishirikishe. Hivi huwa mnafikiri hawa ndugu na wazazi walipata shida kiasi gani kuwalea na kuwakuza hao mnao waita wame zenu?
 
Sasa na yeye ofisini ameshatangaza mume wake kibosile, pesa ya kubadilishia gari unaambiwa ni ada ya mdogo wangu, kuwa alikotangaza ufalme heshima itashuka mkuu.
Nime amini wanawake wengi ni wachawi na ukitaka kujua basi ingiza swala la ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…