Kakobe mtumishi wa mungu au tapeli;waumini kuandikisha malizao ,mishahara,

SIO NA SISEMI AMINA.....!
BISHOP KAKOBE anabaki mtumishi wa MUNGU aliye juu.....! anaweza kuwa na mtazamo tofauti juu ya jambo fulani lakini bado anabaki GOD'S SERVANT.....!
kuorodhesha mali ni utapeli...? Mbona serikali inahitaji watumishi wake waorodheshe mali zao? je na huo ni utapeli au UTAWALA BORA...?
Anachofanya mtumishi wa MUNGU aliye hai ni KUWAEPUSHA WAUMINI NA DHAMBI YA ANANIA NA SAFIRA....! au mimi ndo nasoma BIBLIA TOFAUTI NA YA WENGINE....?
WATU HAWA KATIKA BIBLIA WALIFICHA TAARIFA MUHIMU NA WOTE MAUTI ILIWAKUTA.....!
HALAFU BIBLIA KATIKA WARAKA WA YAKOBO INATUELEZA TUSIWE WEPESI WA KUNENA BALI TUWE WEPESI WA KUSIKIA.....!
TUANGALIE TUSIJEINGIA UPOTEVUNI KWA KUWA WASEMAJI.....!

SASA NASEMA BWANA YESU APEWE SIFAAAA.!

Ni vigumu kujadili Imani. Lakini Biblia ninayosoma mimi inasema ukitoa sadaka kwa mkono wa kulia hata mkno wako wa shoto usjue!! KAKOBE May be is what you claim is. Lakini Kaingiza ubinadamu!!!! Kazi yake ni kutangaza na kufundisha injili. Sasa anapoamua kushika bakora amekuwa Mungu? Serikali sio dini kuorodhesha mali za watu ni mojawapo ya kukbili wimbi la rushwa na wizi. Je motive ya kakobe ni nini kama ni kukwapua pesa za watu? Maana ajijua kipato chako theni anakuwa Mungu huwezi kukwepa. Je ana pension ukistaafu? NO NO FUNGUKA MACHO USIWEKE KAKOBE IN A PLACE OF GOD.
 
Jana Kp kanifurahisha sana check katuni yake

Hawa ndio watumishi wa Mungu baadhi yao tulionao

4515d1241770282-kakobe-mtumishi-wa-mungu-au-tapeli-waumini-kuandikisha-malizao-mishahara-kakobe.jpg
 
Attachments

  • kakobe.jpg
    kakobe.jpg
    17.2 KB · Views: 134
mtumishi wa mungui MAHESABU.ni kweli kabisa unachoongea .na kama nimesoma vizuri kilichoandikwa gazetini ni kwamba watu wanaitaji ufahamu wa mungu kwanza ndipo utakapojua unaitaji kutoa zaka ama lah;mimi binafsi naweza kusema kama mwananchi ama mtu anaeitajika kwenda mbinguni ananafasi ya kuuliza pale ambapo hatawea kuelewa.....na jinsi ya kusaidika ni kwa kupitia wewe na mimi.....
bado naendelea

Lete vitu baba!!!!!!
 
Pdidy bado hutakuwa umeweka mizani yako sawa kwani KAKOBE majibu aliyotoa bado hujayaambatanisha ......!
DO HIM A FAVOR ON THIS....!
 
narudia tena P DIDY na wenzako ambao mmekua wa mstari wa mbele kumuita mtumishi wa Mungu 'words' jitokezeni tena kwani amewajibu katika muda muafaka......!
Mkuu MAHESABU kama nilivyokueleza mwanzoni kwamba hatuko katika kubishana bali kuelimishana...kwanza naomba nikuelekeze kama nilivyokujibu kwenye PM kwa alichonitumia KAKOBE..kwamba hii ni sehemu ya wazi na kwamba ni vyema watu wakaokolewa pale ambapo wanaona hawaelewi.....nini maana yake mi nimekuelekeza nami nimetoa kwenye gazeti ndugu nikitaka kupata ufahamu kwamba hii ni sawa nami naweza kumshauri mchungaji wangu tukaamua kutangaza waumini wataje mali zao..lakini toka mwanzo we umekuwa ni kama mshabiki na si kutaka kuelimisha watu...ndugu nilikuwa trainning nimerudi jana ..naomba kama wewe una roho wa MUNGU na umeitwa kwa ajili ya MUNGU nadhani ni vyema ukaandika haya MAJIBU HADHARANI badala ya kushindana tuwasaidie ama kuwaelimisha wengine.......
natumainii tupo pamoja.....

PDIDY,

KUBALI YAISHE, acha wanaoorodhesha mali zao waendelee, maana

wameelimishwa, ni watu wenye visomo mbalimbali (kama alivyosema

WABEROYA)na ni waelewa. Kumbuka ile ni habari ya IMANI, na imani huweza

kuhamisha milima!

MTUMISHI TUKO PAMOJA MI SIPO KWA AJILI YA KUMHUKUMU MTUMISHI WA BWANA NA NAOMBA NIELEWEKE NAMHESHIMU KAKOBE KAMA MTUMISHI WA MUNGU NA NAFIKIRI NILICHOKISOMA KWENYE GAZETI NDICHO NILICHOANDIKA HAPA NA LENGO LANGU NI KUELIMISHWA NA SI KUBISHANA AMA KUSHINDANA..ILI TUANGALIE JINSI GANI YA KUWASAIDIA WALE AMBAO HAWANA UFAHAMU.......INAWEZEKANA KABISA MTUMISHI YUKO SAWA KABISA ILA KUNA WALE AMBAO HAWAJAMUELEWA NA NAFIKIRI MMOJA WAPO NI WALE WA LIOANDIKA KWENYE GAZETI SASA MIMI NA WEWE TUKO KWA AJILI YA KUWAELIMISHA WATU..KAMA ULIVYOKUWA PAMIJA TOKA MWANZO NILITARAJIA MAJIBU YAKOA KAMA IFUATAVYO

1?)KUTOKANA NA WARAKA WA PDIDY NAOMBA NIWAELIMISHE WATUKAMA IFUATAVYO A.........B........C.....................

BAADA YA HAPO NAMI NATOA MAWAZO YANGU KAMA BINADAMU MWENYE HAKI YA KUJUDGE KAMA SAWA AMA LAH......

NAFIKIRI HAPO MUNGU ATAKUPA THAWABU KWA KUWASAIDIA WATU KUWAELEKEZA BADALA YA MIMI NA WEWE KUSHINDANA NA KUTUMIANA VITISHO KWENYE PM......
 
MAHESABU
Fungu la kumi ni agizo la Mungu au kwa maneno mengine ile ni kama kodi kila pato unalopata 10% sio yako ni ya Mungu. soma Malaki 3. unapotoa unatimiza agizo la Mungu sasa kusimamishwa kanisani na kuombewa inaweza kuwa ni utaratibu wa hilo kanisa, lakini cha muhimu ni wewe kutoa na kabla hujatoa wewe peke yako mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufanya kazi/biashara au chochote kilichokupa pato hilo, na umuombe Mungu aipokee sehemu yake maana usipotoa unamwibia Mungu.
_________________
HALELUYA
 
Tunaweza kulikabili swala la "Fungu la Kumi" kwa njia nyingi ili tuielewe vizuri.

Njia moja ni kuangalia Kazi aliyoimaliza Yesu Kalvari.

Je, kwa Neema, Yesu alichukua dhambi zetu? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua umaskini wetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua udhaifu wetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua magonjwa yetu ? Ndio.
Je, kwa Neema, Yesu alichukua kushindwa kwetu? Ndio

Ikiwa ni kwa Neema(grace), hakuna kazi tunayoweza kufanya ili tupate hivyo vitu ila kumwamini Yesu tu. Inawezekanaje katika ukombozi wetu kuwa baraka zingine zinakuja kwa neema na zingine zinakuja kwa matendo (works) ? Yesu alifanya kazi kamili na Neema na matendo(works) haziendi sambamba katika ukombozi wetu.

Kama tuko na ile mindset ya kwamba hatuwezi tukabarikiwa tusipotoa fungu la kumi, hio ni kazi (works). Neema na Kazi haziendi pamoja katika ukombozi wetu. Watu wengi wana hiyo "mindset" (fikira) kwamba "nitafanya nitakavyo, nitaishi maisha yangu nipendavyo" lakini nitatoa tu fungu la kumi na Mungu ataendelea kunibariki ama ni lazima nitoe "fungu la kumi" ili Bwani anibariki.

Ikiwa tuna hiyo "mindset", basi tumekosea lakini kama tunatoa fungu la kumi kubariki kazi ya Bwana basi hiyo ni sawa kabisa.

Baba yetu anataka kuondoa hii mindset. Maisha yetu yote ni yake. Kila kitu tulichonacho ni chake. Hakuna Baba anayemwabia mtoto wake ni lazima alipe ili amsaidie na ninaamini wachungaji wanaowambia watu kwamba watapata laana wisiotoa "fungu la kumi" wanamhuzunisha Bwana sana. Baba gani anataka watoto wake wamwone hivyo?

Njia ya kuelewa mada yoyote kwenye Biblia ni kuisoma mpaka unaelewa context yake. ktk Malachi, ni vizuri kusoma Malachi yote na kueielewa kabisa. Kulikuwa na ukame mkubwa ktk nchi hii na Bwana kwa kupitia Malachi aliwambia makosa yao.

Kwanza hawa watu walikuwa wakitoa "fungu la kumi" lakini walikuwa wanafanya mambo mengine mabaya yaliyomhuzunisha Bwana. Hata ile "fungu la kumi" wiliyotoa ilikuwa mbaya (Mal 1:14). Bwana alitaka watoe "fungu la Kumi" iwasaidie mayatima na wajane Mal 3:5. Je "fungu la kumi" linawasaidia mayatima, wageni na wajane siku hizi katika makanisa yetu? Mimi ninamini nikitoa "fungu langu la kumi" niwapelekee hawa wajane na mayatima bila kupitia kanisa, Baba anafurahi kuliko nipeleke hii fedha kwa makanisa wale hawaangalii maslahi ya wajane na mayatima.

Kwendelea na Malachi 3:10, ile baraka Bwana alisema atawapatia wakigeuza mienendo yao na kuleta "fungu la kumi" safi ilikuwa Mvua. kumbuka kulikuwa na ukame. Walikuwa wamemwibia Bwana wa njia ngani? Kwa kukosa kuleta "fungu la kumi" safi ili mayatima, wageni na wajane wasaidike.

Kumbuka pia maandao ya Bwana (Gods provision) ni kwa neema na neema pekee 2Cor 8:19.
kwa ufupi, ile "mindset" uliyonayo nayo unapotoa "fungu la kumi" ndio inayotambulisha kama ni vizuri au hapana.
 
kweli kuna maandiko nitatafuta muda lakini ningependa kusema hata Yesu mwenyewe alifundisha sana utoaji. angalia Luka 6:38 " wapeni watu vitu kipimo cha kujaa na kusindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Hii ina maana mlango wa kupokea ni kutoa sasa tukisema tumeokolewa kwa neema na kila kitu ni kwa neema basi tusifanye chochote inakuwa ni kinyume cha neno tunatakiwa kuwa watendaji pia na kuwa watendaji haina maana tunalipia wokovu hapana. Wagalatia 6:7 anasema "Msidanganyike Mungu hadhihakiwi kwa kuwa chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.ili uvune ni lazima upande. Ili upate pesa lazima upande pesa. Hadithi ya Kornerio pia iko kwenye Agano jipya kwamba kwa sababu ya utoaji wake Mungu alipokea sala zake akamtuma malaika kumwambia kwamba sadaka zake zimefika mbinguni atume watu waende kwa Petro aje awabatize yeye na familia yake inamaana huyu alikuwa anatoa sadaka lakini alikuwa bado hajaokoka Mungu akaona sadaka peke yake hazitampeleka kwenye ufalme wa Mungu ila anahitaji wokovu
lakini kilichotangulia kwanza ilikuwa ni sadaka.

Agano Jipya halipingi Agano la kale, Yesu alisema sikuja kutangua torati bali kuitimiliza sasa hatuwezi kukataa yaliyopo kwenye Agano la kale. "Tunapookoka tunakuwa Uzao wa Ibrahimu na baraka hizo zinafuatana nasi haijalishi ziko kwenye Agano la kale au Agano Jipya.
Angalia Wagalatia 3:29,Wagalatia 3:13,14

ila Anahitaji wokovu
 
TOFAUTI YA ZAKA NA DHABIHU

Kutokutoa zaka na dhabihu ni kumwibia Mungu. Mtu aliye mkristo asipotoa zaka na dhabihu anaitwa mwizi. Kuna wakristo ambao ni wezi lakini wao hawajui yakuwa ni wezi. Wamemwibia Mungu zaka na dhabihu. Mungu anasema hivi:

Je! mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia ZAKA na DHABIHU(Malaki 3:8)

Kati ya amri tulizopewa na Mungu ni kwamba tusiibe. Kuiba ni dhambi. Na dhambi ina adhabu yake. Popote palipo na dhambi, laana hutokeza. Kwa wale wanaomwibia Mungu kwa kutokutoa zaka na dhabihu, wamefunikwa na laana. Ndiyo maana Mungu alisema hivi:

.. Mmeniibia Zaka na Dhabihu. Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote (Malaki 3:8b, 9).

Laana maana yake ni kutokufanikiwa, kutofaulu, kutokustawi, kukosa furaha, kukosa amani, na kukosa mwelekeo sahihi. Ni wazi kuwa wakristo wengi hawana furaha, hawana amani na hawafanikiwi katika maisha yao ya kila siku, kwa sababu hawamtolei Mungu zaka na dhabihu.

Unapokosa kumtolea Mungu ili ujenzi wa nyumba yake kanisa uendelee, Hagai 1:6 anatuambia Mungu anasema hivi;

Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka

Zaka ni kitu gani?

Zaka ni fungu la kumi la pato lako. Hebu isome na kuitafakari mistari ifuatayo;

Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana.Tena zaka yote ya nGombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; SEHEMU YA KUMI watakuwa ni watakatifu kwa Bwana (Mambo ya Walawi 27:30 ,32).

Toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako; na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo(Kumbukumbu la Torati 14:28-29).

Zaka ni fungu la kumi la pato toka mshahara wako ofisini, shambani au kwenye mifugo. Tena zaka hii ni ya Bwana na ni Takatifu.

Mtu asipoitoa zaka hii anamwibia Mungu. Zaka si yako hustahili kukaa nayo wala kuitumia nje ya utaratibu wa Mungu.

Lakini Malaki 3:10a anasema; Leteni zaka KAMILI Maana yake nini maneno haya? Maana yake ni hii; ikiwa kwa mfano mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/= ( kabla ya makato) fungu la kumi au zaka unayotakiwa kutoa ni shilingi 200/= ambayo ndiyo zaka kamili ya mshahara wako. Ukileta pungufu yake hiyo si zaka kamili.

Tena kwa mfano umevuna magunia 10 ya mahindi toka shambani mwako zaka kamili unayotakiwa kutoa ni gunia moja bila kupungua. Kumbuka mzaliwa wa kwanza wa mifugo yako ni wa Bwana.

Unaweza ukasema habari za kutoa zaka ni za agano la kale na siyo za agano jipya.

Waebrania 7:5-10 inatuambia wazi ya kuwa Ibrahimu alitoa fungu la kumi. Kama Ibrahimu alitoa sehemu ya kumi, Je! si zaidi sana kwetu sisi tulio uzao wake kwa imani ndani yake Kristo? Maana imeandikwa hivi;

Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ahadi (Wagalitia 3:29). Soma pia Wagalitia 3:13,14).

Dhabihu ni kitu gani?

Dhabihu ni matoleo yanayotolewa baada ya kutoa sehemu ya kumi ya pato lako. Kwa mfano, kama mshahara wako kwa mwezi ni shilingi 2,000/=, basi sehemu ya kumi (zaka) ni shilingi 200/=. Kiasi cho chote utakachotoa ju ya shilingi 200/= ndiyo matoleo yako. Kwa mfano ukitoa shilingi 210/= toka kwenye mshahara wako wa shilingi 2000/=, Basi, shilingi 200/= ni zaka; na shilingi 10/= ni dhabihu au matoleo au sadaka ya kawaida.

Kiasi utakachotoa katika dhabihu/matoleo, ndicho kitakachokuwa kipimo kitakachoweka kiwango chako cha kupokea. Imeandikwa hivi:

Lakini nasema neno hili, APANDAYE HABA ATAVUNA HABA; APANDAYE KWA UKARIMU ATAVUNA KWA UKARIMU. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, MKIWA NA RIZIKI ZA KILA NAMNASIKUZOTE,mpatekuzidisanakatikakilatendojema;kamailivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, haki yake yakaa milele. Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye ATAYAONGEZA MAZAO YA HAKI YENU, MKITAJIRISHWA KATIKA VITU VYOTE MPATE KUWA NA UKARIMU WOTE; umpatiao Mungu shukrani kwa kazi yetu. Maana utumishi wa huduma hii HAUWATIMIZII WATAKATIFU RIZIKI WALIZOPUNGUKIWA TU, Bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu; kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, WANAMTUKUZA MUNGU kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote(2Wakorintho 9:6-13)

Soma tena mistari hiyo hapo juu, lakini sasa tafakari zaidi maneno niliyoyaandika kwa herufi kubwa. Utaona kuwa usipokuwa mwaminifu katika utoaji, wewe mwenyewe unakosa kufanikiwa, na pia unamkosesha Mungu shukrani na utukufu ambao angepata kwa utoaji wako.

Zaka na dhabihu zitolewe wapi?

Hili jambo linahitaji uongozi wa Roho Mtakatifu, ili upate ufahamu Mungu anataka upeleke wapi zaka na matoleo uliyo nayo.
Hili ni muhimu kwa kuwa Biblia inazungumza juu ya kupeleka kanisani (Malaki 3:10-11), kwa watakatifu (2Wakorintho 9:12), kwa maskini (2Wakorintho 9:8-9), kwa watumishi wa Mungu (1Wafalme 17:10-24; 1Wakorintho 9:7-14); kwa wajane, - na kadhalika.

Muombe Mungu akuongoze mahali pa kupeleka. Amani ya Kristo na iamue moyoni mwako.

Baraka Tele!

Kuna baraka tele za mafanikio kwa mkristo aliye mwaminifu katika kumtolea Mungu zaka na matoleo.

Katika Malaki 3:10 imeandikwa hivi; Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo (YA UTOAJI) asema Bwana wa Majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA AU LA

Je! umewahi kukutana na mkristo ambaye anashuhudia kuwa Mungu amempa baraka nyingi hata HANA MAHALI PA KUZIWEKA? Ni wazi kuwa ahadi hii haijatimia kwa kuwa hatujawa watendaji na Neno kikamilifu katika utoaji.

Soma mistari hii hapa chini uone baraka zingine zinazotokana na utoaji; “Azaria Kuhani Mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa Bwana, tumekula na KUSHIBA NA KUSAZA TELE; kwa kuwa Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa. Ndiko Hezekia akaamuru kutengeneza vyumba nyumbani mwa Bwana; wakavitengeneza. Wakayaingiza MATOLEO na ZAKA na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu (2Mambo ya Nyakati 31:10-12).

Kwa nini wakristo wengine wanapungukiwa vyakula, wakati tuna nafasi ya kumruhusu Mungu kutubariki kwa vyakula tele? Mpe Mungu nafasi ya kukubariki kwa kumtolea zaka na matoleo!

Anza Sasa!
 
FUNGU LA KUMI
Hii nayo ilikuwa sehemu ya Torati ya Musa(Hesabu 18:21), ambapo Wayahudi walitoa Fungu la kumi katika vitu vyao na kuwapa kabila ya Lawi ya ukuhani. Kwa kuwa sasa hakuna ukuhani wa kibinadamu, shurutisho haliwezi kuwapo tena la kutoa fungu la kumi kwa mzee awaye yote wa kanisa. Wazo potofu tena (katika suala hili la kuhusu makuhani) limewaongoza kwenye lingine (yaani, la kutoa fungu la kumi). Mungu mwenyewe hana haja ya matoleo yetu ya sadaka, kwa kuwa vitu vyote ni vyake (Zab. 50:8-13). Tunamrudishia Mungu tu kile ambacho ametupatia sisi (1 Nyak 29:14). Hatuwezi kupata wokovu kama tokeo la kutoa vitu vyetu viwe sadaka, kama katika masharti ya fedha. Katika kushukuru zawadi kubwa ya Mungu aliyotupatia, hatutoi tu sehemu ya fungu la kumi bali tunato maisha yetu yote. Katika haya , Paulo ameweka mfano, kweli akitendea kazi kile alichokihubiri: "Iitoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana" (Rum 12:1).
 
acha kupotosha mafundisho ya mwenyezi Mungu. Kama huelewi uliza wanaojua wakufundishe.
 
samahani kwa kukukwaza naona umekimbilia upande mmoja na kusahau mengine yalioandikwa mungu akuwezeshe kutenda mema.....
 
Tatizo wabongo hatujifunzi kutokana na makosa ya wengine.

Huko Kenya mwaka juzi watu waliliwa fedha zao na DECI. Mwaka huu kitu hicho hicho kimetokea Tanzania.

Nyie wafuasi wa Kakobe, mnaliwa. Amkeni sasa. Mkichelewa mkaja kuamka baadae sana na kudai chakwenu, atawafungia ndani ya majengo ya FGBF na kuwaKibwetere.

Nimewaonya.
 
Ila hata mimi nadoubt juu ya Askofu Kakobe,kwa nini haruhusu mtu mwingine yeyote kusumama madhebaun kwenye lile kanisa lake?coz utakuka akisafiri waumini wanahubiriwa na recorded kwenye tv?
 
Back
Top Bottom