Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Wanaume kuna wakati mnashangaza sana. Unakuta mtu anasema hawezi kuoa single mama…. Hebu tuambieni kipi bora kuoa single mama ambae Yes alikosea but katunza mimba Kazaa mtoto na sasa ametulia Kajifunza kutokana na makosa AU bora kuoa binti alie bwia ma contraception hadi kizazi kimepinda au katoa mimba mpka kizazi kina makunyanzi utamuoa hata msipate mtoto? Kipi bora???
Wengi humu ni wazazi wa mabinti na wazazi watarajiwa unajuaje binti yako hata zaa kabla ya ndoa? Je vijana wakija kuonyesha interest utawaambia usimuoe binti yangu ni single maza?
Wangapi humu ni zao la single maza? Hivi mnavyo andika humu ndivyo mnavyoangalia mama zenu kua huyu Hana thamani ni single maza?
Na mshawahi kujiuliza anaempa binti mimba akamuacha yeye akaenda kuoa a fresh girl (as you think) is he not as guilty as well ???
Natamani ifike mahala jamii yetu isimnyooshee binti kidole kisa ni single mom bali tujikite pia kwenye kuongea na vijana wetu as they are also “single dads” na kuna mabinti pia hawatataka single dads kwa kuogopa pia baby mama dramas so it goes both ways!!!
Single mamas sio shida kikubwa jiridhishe kwamba ametulia na anajiheshimu hata Kama baba mtoto yupo kwenye picha, kuliko kuoa binti ambae anabwia ma P2 kila mwezi na Maria Stopes Ana Loyalty card!

Disclaimer: Read this with an open mind maana mtahisi ni maoni ya single mom which is quite the opposite [emoji3577]
 
Kutoka disclaimer napenda kukupa pole sana dada, usingle mother sio kilema hivyo siku moja waweza ambulia boya wako mmoja akanasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ivi kwa mfano mwanamke alishazaa ila mtoto akafariki huyo nae yupo kundi la single maza?
 
Mtoa mada kasema kuwa, yule mwamba amehoji.

Huyu mwanamke aliyezaa nje ya ndoa(ingawa anasema ilikuwa bahati mbaya) atawahusiaje wanawe na wao wasizae nje ya ndoa? kuwa aje awahusie pindi wakiwa wanazini kabla ya ndoa wawe makini wasipate mimba?.

Hizi hoja za yule mwamba ni nzito zinahitaji majibu.

Tupatieni majibu ya hizi hoja kwanza.
 
hahahaha
 

Mara nyingi getting in trouble is not an issue the issue is how you get out of trouble,learn from it and move on.
Trust me anaweza kutumia mfano wake kuonya wanae na maisha yakaendelea.
Na malezi mazuri hayaangalii historia ya mzazi kuna wazazi ambao hawakua single mothers/fathers lakini ndio wanamalezi mabovu na watoto wenye kila tabia mbovu.
Unataka kuniambia mashoga baba zao walikua mashoga??? Mzazi ni sehemu tu ya malezi ya mtoto, dunia pia ina nafasi yake ambayo mzazi hawezi kuzuia! So hoja ya jamaa haina mashiko
I am sure unamifano kibao ya familia ambazo ziko vizuri Ila watoto wako hovyo.
 
Hilo haliwezi kuhalalisha hili tunalolikataa hapa.
 
Kweli Pond boy
 
Hela ni zetu, wachoyo kwa vyetu, tafuta vyako.
 
Ni uhuni wake na ukicheche ndiyo umemletea nuksi, siyo mtoto. Binamu yako ni aina ya wanawake wahuni na much know wale, yaani wale mashangingi.
 
Wewe uzungumzia kuoa!!!!

Mi kutembea na mwanamke mwenye mtoto ambaye sio mke wangu hata sijawahi kuwaza kama naweza kufanya kitu kama hicho

Nikijua una mtoto hisia Inakata hapo hapo..

Kivip sijawahi kuwaza hata km naweza kulala na mwanamke mwenye mtoto tena katika ulimwengu huu ambao wanawake wasio na watoto wapo wengi
Lakini sijui ya mbeleni huko labda tena labda inaweza kutokea bahati mbaya
 
Umepangilia hoja zako vizuri, nakubaliana na wewe..... tatizo ni hizi stereotypes za kiafrika.... single moms wanakua antagonized wakati wanaume waliowapa mimba hawapati lawama wanazostahili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…