Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Na mwanaume mwingine ambaya ataki kukaa na mtoto na anakuambia tuu mpeleke mtoto wa Baba yake.
Au muache mtoto kwa wazazi wako

Na hakuna kuja nyumbani,
Nimewahi ona dada mmoja alizalia home jamaa alimkataa mtoto.
Dada akaolewa mtoto kamuacha kwa wazazi na hajawahi kwenda kwa mama yake. Ni mama tuu anakuja kumtembelea mara chache sana.
Hii inakaaje
 
Watoto hufuata na kuiga kile mzazi anafanya sio anachosema. Watoto wakishaona mama anaishi bila baba na wao watafuata huo mlengo hivyo hivyo watazaa na mwanaume kisha watataka kulea wenyewe in the future.

So tunapopambania ndoa iheshimiwe tunajenga mazingira ya kuua hiki kizazi cha hovyo kinachotengenezwa sasa.
 
Napenda mtu akijibu kwa hoja ili wote tujifunze kuliko kupinga.
Hilo jina tu unalotumia ni la yule Single mother anayevuruga ukoo wa malkia kule kwa kuleta vituko as if alilazimishwa kuolewa kwenye ukoo wa ufalme kisha anaanza wapangia yeye namna ya kuishi.
 
Shida ni kupasha kiporo [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Umepangilia hoja zako vizuri, nakubaliana na wewe..... tatizo ni hizi stereotypes za kiafrika.... single moms wanakua antagonized wakati wanaume waliowapa mimba hawapati lawama wanazostahili.
Wewe umeshawahi kuona wapi uhalifu ukizidi analaumiwa mwalimu badala ya askari.
 
Ni hivi, ni ufala na ufenge kuoa singo maza.
Kwani hizo P2 unadhani singo maza hamezi, tena wengine mpaka wanaamua kuzaa ni sababu wataalam wamemuonya kuwa this time akitoa haponi au anapoteza kizazi mazima. So, kama ulitaka kuwapa ushujaa katika hilo jua kwamba they are no better at all. Wajitunze.
Akiamua kubeba mimba basi ajitoe kwenye ligi aendelee na maisha yake, siyo kuleta mada za kiharakati kuhalalisha mambo ya hovyo ma ya kinyonge. Kama hawezi kuishi bila kuolewa basi ajioe mwenyewe atunze watoto wake.

Akitaka ajitunze hakuna lugha wala namna ya kumshawishi mwanaume.
Kama unaona siyo fair basi shawishi kaka zako uwatafutie singo mamaz au lea mtoto wako uje umuoze kwa singo maza.

Kuhusu sisi, we are no match na nyie, sisi tunawafyatueni tu halafu muda wa kuoa tunatakiwa kutafuta mwanamke/msichana atakayeitwa mama fulani, siyo unaenda kumuoa mama fulani, hiyo haipo that's nature.
Mama fulani yeye tayari ana baba fulani, apambane naye hadi aolewe naye. Hizo nguvu mngezielekeza kwenye kuwalazimisha hao walio wazalisha singo mamaz kuwa ndiyo wawaoe, siyo mnaenda kupigia kelele watu wasio husika.

NB. Tunapoongelea single mama hatuna mipaka, ni awaye yeyote.
 
Hao wenzako ni akina nani?! Maana usianze kutufananisha na jamii za mataifa ya kimagharibi. Huko ambako kuna matatizo lukuki ya kijamii. Mbona unataka kuchukua faida tu hasara unaacha.

Ngoja nikusaidie.

90% ya vijana waliopo jela wanaotokea kwenye single parent house holds.

Wale wahalifu wanaofanya matukio kama ya mass shootings huwa wanahistoria ya kutoka katika broken homes lead by single mothers. Fuatilia data usibishane na mimi.

Tunapokemea hivi tunalenga kulinda jamii zetu za kiafrika tusifike huko.

Nenda kaongee na askari wakupe data za kifamilia za Panya road utaanza kuelewa shida ipo wapi.

Single mother ni definitely a deal breaker usichukulie kirahisi hivyo.
 
Hapa umeassume kuwa kila binti ambaye hana mtoto basi anatoa mimba, hii ni wrong thinking and a terrible way ya kumake assumptions.

Huku mtaani wapo mabinti ambao hawajawahi toa hata mimba. Katika umri wa miaka 20 hadi 25 wapo mabinti bikra au ambao wameingiliwa mara moja tu. Mbona wapo.
 
Umechukua kasehemu kadogo sana na kuanza kutengeneza hoja ili utete uzembe mkubwa. Yaani watu kukemea kitu ambacho kina waathiri wewe unaita ni kutengeneza "Stigma"?
 
Umetoa makavu kitaalamu sana. Naomba uwe shemeji yangu.
 
Nimekumbuka uzi wa jamaa aliekuwa kaoa single maza mama mkwe na shemeji zake wa kike wakawa wanampa shavu baba mtoto wa yule mkewe. Mara wamwambie yule mwenzio ulimkuta 🤣🤣🤣 usilete wivu
 
Hahahah single maza bile hela ni mtihani. Uwoya ana 90% success rate ya kupata ndoa kuliko mwanamke singo maza wa mtaani ambaye ni kula kulala kwa mama yake.
 
Msichana wa miaka 15 au 16 kama haujielewi huruhusiwi hata kukaa na wavulana maana ni mtoto mdogo sana bado upo chini ya wazazi na hauna ruhusa ya kujihusisha na mahusiano.

Kwa upande mwingine, mwanamke ndie ana amua kupata mtoto na mtu ama la. Mwanamke ameshaelekezwa kuwa asiwe na mahusiano au makubaliano ya kuanza kulala kingono na mwanaume hadi pale amepata approval ya wazee wake ( aidha baba na mama au walezi wengine). Tukisimamia huu msingi hata mahusiano yatakuwa salama.
 
Ila unawalaumu zaidi wanawake lakini wanaowaribia future hao wanawake huwalamu [emoji23][emoji23]

Pamoja na hayo umesomeka
Ukitaka kujua akili za mwanamke mpindulie swali uone atakavyogeuka exactly alichokisema nitakupa mifano.

Muulize single mother single mother yoyote hapa kuwa yeye ana haki ya kuanza maisha ya hati safi baada ya kuzalishwa na muhuni mwenzake utaona atakavyoshabikia na kujitetea kuwa ni stahiki yake.

Sasa mgeuzie swali, muulize mfano wewe hapo ulivyo ni single mother, ukapata mtoto wako wa kiume. Ukasomesha kwa shida sana kwa kuuza vitenge, maandazi, kufanya shughuli za mama ntilie ukajinyima 90% ya mapato yako yakaenda kwa huyu mtoto na kweli mtoto akafanya jitihada na kufanikiwa ukaenda mbali zaidi hata kupigia magoti watu wazito mtoto wako apate ajira.

MUNGU akafunua njia na kusikiliza kilio chako single mother miaka 10 baadae mwanao huyu uliyempambania akafanikiwa baada ya kusota na mishahara ya laki tatu akapata contract nzuri ya milioni tano kwa mwezi. Akapewa nyumba na kampuni, gari nzuri ya kutembelea.

Then within a month baada ya kuhamia makazi mapya then akaja kukutambulisha kwa mwanamke kwanza kamzidi umri kidogo halafu ana watoto watatu wadogo sana kila mtoto na baba yake. Na huyu mwanamke anatokea familia ya kipato cha chini sana kwao ndie tegemeo na hajiwezi kuwasaidia kwao.

Then mwanao anakuja kukutambulisha kuwa huyu ndie love of his life na ameamua kuwachukua watoto kama wake na atawaandika kwa majina yake ya ukoo na kuwa asili kuwa wanae kinyaraka na warithi wa mali zake.

Wewe single mother utabariki huu uhusiano wa mwanao au utapinga?!

Kumbuka huyo nae ni Single mother kama wewe ila tu yeye ana watoto zaidi yako. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…