Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Wale wanaosema asiwe na mawasiliano na aliyemzalisha, hii inaweza ikakupeni furaha ya muda mfupi. Sababu kama mtoto anajua baba yupo hai na huna mawasiliano naye huku upo busy na mwanaume wako mwingine (mume wako), hii itampelekea mtoto kujenga chuki kwako na kwa mume wako na watoto wenu na hata akafikiria kuwadhuru.

Yeye atakua anajiona ni outsider tu, ikifika wenzake wanaenda kutembelea upande wa baba yao, yeye ataachwa pembeni au hata akienda basi kule lazima kuna mambo watamtenga sababu ni mtoto wa watu.
Yeye pia akienda kumtembelea baba yake au upande wa baba yake lazima kuna mambo wenzake watatengwa tu.
Hiyo hali inakua inajenga mpasuko mkubwa sana kwa watoto siku za baadaye, huku nyinyi mkijidanganya mnapendana wakati mfumo wa maisha umekaa.

Mbaya zaidi baba yake awe na uwezo duni kuliko nyie ndiyo chuki itakua zaidi kwa kuhisi kuna dhurma ilifanyika.
Haya mambo siyo mepesi, bora aendelee na maisha yake tu, lakini si kutafuta ndoa bali ije yenyewe na hata ikija atatakiwa kutafakari sana.
Na mwanaume mwingine ambaya ataki kukaa na mtoto na anakuambia tuu mpeleke mtoto wa Baba yake.
Au muache mtoto kwa wazazi wako

Na hakuna kuja nyumbani,
Nimewahi ona dada mmoja alizalia home jamaa alimkataa mtoto.
Dada akaolewa mtoto kamuacha kwa wazazi na hajawahi kwenda kwa mama yake. Ni mama tuu anakuja kumtembelea mara chache sana.
Hii inakaaje
 
Mara nyingi getting in trouble is not an issue the issue is how you get out of trouble,learn from it and move on.
Trust me anaweza kutumia mfano wake kuonya wanae na maisha yakaendelea.
Na malezi mazuri hayaangalii historia ya mzazi kuna wazazi ambao hawakua single mothers/fathers lakini ndio wanamalezi mabovu na watoto wenye kila tabia mbovu.
Unataka kuniambia mashoga baba zao walikua mashoga??? Mzazi ni sehemu tu ya malezi ya mtoto, dunia pia ina nafasi yake ambayo mzazi hawezi kuzuia! So hoja ya jamaa haina mashiko
I am sure unamifano kibao ya familia ambazo ziko vizuri Ila watoto wako hovyo.
Watoto hufuata na kuiga kile mzazi anafanya sio anachosema. Watoto wakishaona mama anaishi bila baba na wao watafuata huo mlengo hivyo hivyo watazaa na mwanaume kisha watataka kulea wenyewe in the future.

So tunapopambania ndoa iheshimiwe tunajenga mazingira ya kuua hiki kizazi cha hovyo kinachotengenezwa sasa.
 
Napenda mtu akijibu kwa hoja ili wote tujifunze kuliko kupinga.
Hilo jina tu unalotumia ni la yule Single mother anayevuruga ukoo wa malkia kule kwa kuleta vituko as if alilazimishwa kuolewa kwenye ukoo wa ufalme kisha anaanza wapangia yeye namna ya kuishi.
 
Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Shida ni kupasha kiporo [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Umepangilia hoja zako vizuri, nakubaliana na wewe..... tatizo ni hizi stereotypes za kiafrika.... single moms wanakua antagonized wakati wanaume waliowapa mimba hawapati lawama wanazostahili.
Wewe umeshawahi kuona wapi uhalifu ukizidi analaumiwa mwalimu badala ya askari.
 
Wanaume kuna wakati mnashangaza sana. Unakuta mtu anasema hawezi kuoa single mama…. Hebu tuambieni kipi bora kuoa single mama ambae Yes alikosea but katunza mimba Kazaa mtoto na sasa ametulia Kajifunza kutokana na makosa AU bora kuoa binti alie bwia ma contraception hadi kizazi kimepinda au katoa mimba mpka kizazi kina makunyanzi utamuoa hata msipate mtoto? Kipi bora???
Wengi humu ni wazazi wa mabinti na wazazi watarajiwa unajuaje binti yako hata zaa kabla ya ndoa? Je vijana wakija kuonyesha interest utawaambia usimuoe binti yangu ni single maza?
Wangapi humu ni zao la single maza? Hivi mnavyo andika humu ndivyo mnavyoangalia mama zenu kua huyu Hana thamani ni single maza?
Na mshawahi kujiuliza anaempa binti mimba akamuacha yeye akaenda kuoa a fresh girl (as you think) is he not as guilty as well ???
Natamani ifike mahala jamii yetu isimnyooshee binti kidole kisa ni single mom bali tujikite pia kwenye kuongea na vijana wetu as they are also “single dads” na kuna mabinti pia hawatataka single dads kwa kuogopa pia baby mama dramas so it goes both ways!!!
Single mamas sio shida kikubwa jiridhishe kwamba ametulia na anajiheshimu hata Kama baba mtoto yupo kwenye picha, kuliko kuoa binti ambae anabwia ma P2 kila mwezi na Maria Stopes Ana Loyalty card!

Disclaimer: Read this with an open mind maana mtahisi ni maoni ya single mom which is quite the opposite [emoji3577]
Ni hivi, ni ufala na ufenge kuoa singo maza.
Kwani hizo P2 unadhani singo maza hamezi, tena wengine mpaka wanaamua kuzaa ni sababu wataalam wamemuonya kuwa this time akitoa haponi au anapoteza kizazi mazima. So, kama ulitaka kuwapa ushujaa katika hilo jua kwamba they are no better at all. Wajitunze.
Akiamua kubeba mimba basi ajitoe kwenye ligi aendelee na maisha yake, siyo kuleta mada za kiharakati kuhalalisha mambo ya hovyo ma ya kinyonge. Kama hawezi kuishi bila kuolewa basi ajioe mwenyewe atunze watoto wake.

Akitaka ajitunze hakuna lugha wala namna ya kumshawishi mwanaume.
Kama unaona siyo fair basi shawishi kaka zako uwatafutie singo mamaz au lea mtoto wako uje umuoze kwa singo maza.

Kuhusu sisi, we are no match na nyie, sisi tunawafyatueni tu halafu muda wa kuoa tunatakiwa kutafuta mwanamke/msichana atakayeitwa mama fulani, siyo unaenda kumuoa mama fulani, hiyo haipo that's nature.
Mama fulani yeye tayari ana baba fulani, apambane naye hadi aolewe naye. Hizo nguvu mngezielekeza kwenye kuwalazimisha hao walio wazalisha singo mamaz kuwa ndiyo wawaoe, siyo mnaenda kupigia kelele watu wasio husika.

NB. Tunapoongelea single mama hatuna mipaka, ni awaye yeyote.
 
You are right kwa wenzetu it’s not even a deal breaker….mwenye mtoto/watoto anaolewa na maisha yanaendelea na Kama kuna mawasiliano na baba mtoto yanakua ya heshima life goes on.
Swali langu bado linabaki kwa wanaume ni utajuaje asie na mtoto ametoa mimba ngapi?? Kipi bora Mwenye mtoto au huyu mama mwenye watoto alio waflash ???? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hao wenzako ni akina nani?! Maana usianze kutufananisha na jamii za mataifa ya kimagharibi. Huko ambako kuna matatizo lukuki ya kijamii. Mbona unataka kuchukua faida tu hasara unaacha.

Ngoja nikusaidie.

90% ya vijana waliopo jela wanaotokea kwenye single parent house holds.

Wale wahalifu wanaofanya matukio kama ya mass shootings huwa wanahistoria ya kutoka katika broken homes lead by single mothers. Fuatilia data usibishane na mimi.

Tunapokemea hivi tunalenga kulinda jamii zetu za kiafrika tusifike huko.

Nenda kaongee na askari wakupe data za kifamilia za Panya road utaanza kuelewa shida ipo wapi.

Single mother ni definitely a deal breaker usichukulie kirahisi hivyo.
 
You are right kwa wenzetu it’s not even a deal breaker….mwenye mtoto/watoto anaolewa na maisha yanaendelea na Kama kuna mawasiliano na baba mtoto yanakua ya heshima life goes on.
Swali langu bado linabaki kwa wanaume ni utajuaje asie na mtoto ametoa mimba ngapi?? Kipi bora Mwenye mtoto au huyu mama mwenye watoto alio waflash ???? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hapa umeassume kuwa kila binti ambaye hana mtoto basi anatoa mimba, hii ni wrong thinking and a terrible way ya kumake assumptions.

Huku mtaani wapo mabinti ambao hawajawahi toa hata mimba. Katika umri wa miaka 20 hadi 25 wapo mabinti bikra au ambao wameingiliwa mara moja tu. Mbona wapo.
 
…pia no one is forcing the guy to love/get married to the girl it’s his choice. In fact hata Mimi namlaumu huyo binti kwa kutomjulisha kijana mapema, she has no one to blame but herself!
Yuko hapa tunajadili not only in their context but kuna ka stigma against single moms vijana wanajazana ujinga, so lazima tu reason kwa upana sio tu kwa a single case!
Umechukua kasehemu kadogo sana na kuanza kutengeneza hoja ili utete uzembe mkubwa. Yaani watu kukemea kitu ambacho kina waathiri wewe unaita ni kutengeneza "Stigma"?
 
Nakwambia hivi, mwanamme anayetoa justification kwa nini hataki kuwa na mwanamke huyu kashakosea.

Kwa sababu uamuzi wa mwanamme anataka kuwa na mwanamke gani hauhitaji justification, ni haki ya mtu tu.

Yani mwanamme ana haki ya kusema yeye hapendi kuwa na single mothers tu. Ni kitu ambacho hapendi tu, ni haki yake kutopenda single mothers. Hahitaji justification.

Na si kila mtu yuko against abortion, wewe umeandika kama it's a given kwamba kila mtu yuko against abotion.

Yani umechukua viewpoint yako ukaifanya kama ni automatic, undisputed, universal truth.

That is a very unspophisticated and unbalanced viewpoint.

Kitu muhimu ni kwamba, ukishakubali kwamba mwanamme ana uhuru wa kuamua awe na nani, huna haki ya kulalamika akiitumia hiyo haki.

Na kama mwanamme ana some crazy puritanism hataki mwanamke aliyezaa, hiyo ni haki yake pia. Kwa nini unamnyanyapaa kwenye kuitumia haki yake?

Wewe nani kakupa haki ya kunyanyapaa watu wanaoamua kutumia haki zao?

Unapotaka kulazimisha watu wasiokupenda wakupende utasemaje hiyo si desperation?

Kwa nini usiwe na mtu anayekupenda na kuacha wasiokupenda na kuepuka malalamiko ambayo hayana msingi?

Umekosa mtu anayekupenda ulivyo mpaka ulazimishe watu wasiokupenda wakupende?
Umetoa makavu kitaalamu sana. Naomba uwe shemeji yangu.
 
Ha ha haaa...hawatambui nafasi yao katika jamii hao, wanajikuta kutaka kutambulika kama tunavyotambulika sisi.
Matukio yanatutambulisha tofauti, halafu wanakuja kutulilia sisi eti kuwa na mtoto siyo shida, kasema nani?
La kuoa mwanamke asiye bikira waliokubali wamelivumilia, sasa wanataka waoe wenye watoto, what next? Watataka hata wakiwaoa wakubali ku share na wanaume waliozaa nao sababu wamewakuta na ni wazazi wenzao.
Jamii inapaswa kumheshimu mwanamke katika nafasi yake, lakini jamii inayowaendekeza wanawake na kuwasikiliza kwa kila kitu kamwe haijawahi kuwa salama.
Nimekumbuka uzi wa jamaa aliekuwa kaoa single maza mama mkwe na shemeji zake wa kike wakawa wanampa shavu baba mtoto wa yule mkewe. Mara wamwambie yule mwenzio ulimkuta 🤣🤣🤣 usilete wivu
 
Mpaka Sasa nimejifunza haya kuhusu singomothers,
° wanawake huwazalia watu waliowapenda sana, hivyo Hadi anazaa Maana yake amempenda sana, hakuna bahati mbaya.
° Singo mothers Wengi Huwa na mawasiliano na waliowazalisha, na hivyo hufanya ngono several times .
° Ukiwa singo mother ni vigumu sana kuolewa, unless singo mother uwe na hela.
Hahahah single maza bile hela ni mtihani. Uwoya ana 90% success rate ya kupata ndoa kuliko mwanamke singo maza wa mtaani ambaye ni kula kulala kwa mama yake.
 
Umeeleweka mkuu, lakini sio sngle mther wte wanauhusiano na wazaz wa bba zao, wengne waliachana kwa karaha sana so hata comm hamna, wengne walishakabdh mtt upande wa baba so comm hamna, kwahyo sio single mother wote wanauhusiano na baba zao na pia sio wte walipata mimba kwa makusud,


Kuna wengine walianza relation pasipo hata kujielewa kama 15yrs au 16 yrs nalo ni tatzo ambalo linaplkea mtoto.
Msichana wa miaka 15 au 16 kama haujielewi huruhusiwi hata kukaa na wavulana maana ni mtoto mdogo sana bado upo chini ya wazazi na hauna ruhusa ya kujihusisha na mahusiano.

Kwa upande mwingine, mwanamke ndie ana amua kupata mtoto na mtu ama la. Mwanamke ameshaelekezwa kuwa asiwe na mahusiano au makubaliano ya kuanza kulala kingono na mwanaume hadi pale amepata approval ya wazee wake ( aidha baba na mama au walezi wengine). Tukisimamia huu msingi hata mahusiano yatakuwa salama.
 
Ila unawalaumu zaidi wanawake lakini wanaowaribia future hao wanawake huwalamu [emoji23][emoji23]

Pamoja na hayo umesomeka
Ukitaka kujua akili za mwanamke mpindulie swali uone atakavyogeuka exactly alichokisema nitakupa mifano.

Muulize single mother single mother yoyote hapa kuwa yeye ana haki ya kuanza maisha ya hati safi baada ya kuzalishwa na muhuni mwenzake utaona atakavyoshabikia na kujitetea kuwa ni stahiki yake.

Sasa mgeuzie swali, muulize mfano wewe hapo ulivyo ni single mother, ukapata mtoto wako wa kiume. Ukasomesha kwa shida sana kwa kuuza vitenge, maandazi, kufanya shughuli za mama ntilie ukajinyima 90% ya mapato yako yakaenda kwa huyu mtoto na kweli mtoto akafanya jitihada na kufanikiwa ukaenda mbali zaidi hata kupigia magoti watu wazito mtoto wako apate ajira.

MUNGU akafunua njia na kusikiliza kilio chako single mother miaka 10 baadae mwanao huyu uliyempambania akafanikiwa baada ya kusota na mishahara ya laki tatu akapata contract nzuri ya milioni tano kwa mwezi. Akapewa nyumba na kampuni, gari nzuri ya kutembelea.

Then within a month baada ya kuhamia makazi mapya then akaja kukutambulisha kwa mwanamke kwanza kamzidi umri kidogo halafu ana watoto watatu wadogo sana kila mtoto na baba yake. Na huyu mwanamke anatokea familia ya kipato cha chini sana kwao ndie tegemeo na hajiwezi kuwasaidia kwao.

Then mwanao anakuja kukutambulisha kuwa huyu ndie love of his life na ameamua kuwachukua watoto kama wake na atawaandika kwa majina yake ya ukoo na kuwa asili kuwa wanae kinyaraka na warithi wa mali zake.

Wewe single mother utabariki huu uhusiano wa mwanao au utapinga?!

Kumbuka huyo nae ni Single mother kama wewe ila tu yeye ana watoto zaidi yako. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom