Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Atapata tu muda ukifika. Asiwe desperate sana kubusu mume. Na ajiulize kwa nini waliyezaa nae hakumwoa
 
Ili kuoa single mother lazima kuzingatia yafuatayo;

1. Lazima ushuhudie kaburi la baba wa mtoto.
2. Cheti cha kifo ( majina ya cheti yafanane na ya kaburi pamoja na kufuatilia uhalali wake ofisi za RITA)
3. Upate video ya mazishi kujiridhisha

NB:
Hakuna kitu kinaitwa mimba ya bahati mbaya.
SASA WEWE JICHANGANYE, HAKUNA RANGI UTAACHA IONA.
Acha nicheke.
 
Yaani hapo ni sawa na kuuliza kwann wanasiasa linapokuja swala la katiba wanaanza kutofautiana ingawa wanatakiwa kujadili ajenda za kitaifa na wanajenga taifa moja?
Mkuu huu mfano wako umenyooka sana, ingawa umenichekesha sana. Watu wanatoana jasho kwa jambo ambalo ni la kitaifa, kumbe ni itikadi zao na mtazamo wao jinsi ya kuangalia mambo😃😃. Mfano umenifurahisha sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] "...mwanangu mimi nakupenda sana, mama yako hakutaka niwe karibu na wewe. Chukua hizi laki mbili zitakusogeza[emoji23], na chukua hii iPhone 14 Pro bado ni mpya tu nimeitumia kama mwezi hivi[emoji23], na mwezi ujao utaniambia ni aina ipi ya laptop unataka, kama ni apple au lenovo... usisite kunikumbusha mwisho wa mwezi huu, na usisahau kunikumbusha suala la shoppong pia[emoji23], baba yako mdogo anataka sana kuonana na wewe..."[emoji28][emoji28][emoji28]
Daaaa nimecheka
 
Waanze mara ngapi, hujui P2 ndio vidonge vyenye mauzo makubwa huko Pharmacy?! Nenda kwenye hizi dispensary ndogo ongea na daktari au muuguzi wakupe data za idadi ya mabinti na wadada plus wake za watu wanaotoa mimba changa, then uje usome tena ulichoandika.
Wake za watu tena ni mimba ya mume au?
 
Hapo Bibi amepigiwa video call "Jamani Bibi yangu". Baba anasema save namba ya bibi, ya auntie hiyo na Baba mkubwa na ndugu zako hawa hapa.

Weekend nakuja kukuchukua tuna tafrija kidogo pale nyumbani ya kukupokea Baraka ya ukoo wetu. Umeandaliwa zawadi na ndugu watakusubiria kukuona kwa shauku.

Hapo mtoto utamwambia nini sasa kwa baba yake? Akienda huko anapokelewa kwa shangwe kama mkuu wa wilaya kaja kufungua Zahanati mpya.
Story tuu hii
 
Mkuu huu mfano wako umenyooka sana, ingawa umenichekesha sana. Watu wanatoana jasho kwa jambo ambalo ni la kitaifa, kumbe ni itikadi zao na mtazamo wao jinsi ya kuangalia mambo[emoji2][emoji2]. Mfano umenifurahisha sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama ipo ni ipo tu,haikuwa ridhiki,wake yupo anakuja awe mpole,hii ndio Dunia tuliopo sasa.
 
Kama ipo ni ipo tu,haikuwa ridhiki,wake yupo anakuja awe mpole,hii ndio Dunia tuliopo sasa.
Sasa mkuu hii falsafa ndogo lakini murua sana kwa nini dada zetu na mama zetu wengine wanashindwa kuielewa na wanajitia unyonge mkubwa wa kulazimisha mapenzi wasipopendwa?

Ujue wanaume wengi tukishamuona mwanamke anakuwa desperate hata kama kulikuwa na mapenzi yananyauka?

A desperate woman is so unsexy.


Mwanamke anatakiwa ajiamini kwamba atapata mwanamme wa aina yake, hata yule ombaomba mwenye ukoma naye anaweza kumpata wake.

Ya nini unilazimishe niwe na mwanamke nisiyemtaka kisa tunawekeana misingi ya "political correctness" ya kuogopa stigma tu?

Hatuoni hapa tunatengeneza tatizo wanaume waoe wanawake kwa kuwahurumia na kuogopa stigma, si kwa mapenzi, halafu ndoa hizi zije kuwa na matatizo makubwa hapo baadaye, kwa sababu mwanamme atajiona kaoa kwa pressure za jamii, si kwa mapenzi ya kweli?
 
Wanawake mnakosea padogo sana (naongea na singo maza) ninachojua mwanamke unatongozwa

wala hujipeleki,hivi kinachokufanya usimkazie huyo mwanaume ni nini? Mkazie haswaa akikuuliza sababu

za kumkazia ndipo unamwambia "nina mtoto" najua huwezi nipenda na mtoto wangu na hata ukinipenda sasa

baadae utanibadilikia "mjibu hivyo muache hapo" Kama kweli ana nia na wewe ataropoka Tu,MTOTO kitu ganiiii

Fresh tuuu,usimkubalie Tengeneza Bond kati yake na mtoto...ukishajiridhisha kamuelewa mwanao Basi nawewe fungua

Moyo mfunulie gauni hilo,Shida yenu singo maza ni 1... Unatongozwa huko unajisahaulisha una mtoto,unajikubalisha

baadae ushageuzwa kama samaki mikao yote ndio unakuja sema "deviii nikwambie kituuu" Hata kama mimi ndio Devi ukinletea hizo story nishakukula Nakuacha.

Niandae akili yangu tangu mwanzo nijue mwenyewe niingie au niache iende,shida yenu mnajitia maslay kwini halafu mwishoni mnasingizia mtoto.

Shida sio mtto shida ni hamjui wakati upi wa kutufikishia taarifa una mtoto au ushawahi zaaa nk,Endeleeni tu vaa maviatu yenu ya manyoya na sku izi mna mayebo yebo yenu mchina kayaleta mkivaaa kama mpo gorofani.]

kingo maza MMOJA wewe kazi kujitia kidada cha Pre form 1,na mtaachwa sana mkiendelea waweka watoto zenu namba mbili baada ya mapenzi.

Singo maza fahamu kuwa mahusiano baaada ya wewe kuwa na mtoto ni Nafasi ya 2,Nafasi ya 1 n Mwanao no.2 ndio mapenzi...Hata mimi kma nakupenda ukniambia tangu ile mwanzo nakutongoza naweza jikaza nikakuvaaa hvyo hvyo maisha yakaenda,ila Ukinfcha uje unletee story zako baada yakuniona niko serious natafuta Washenga kuja kwenu NAKUACHAAAAAAA....
 
Wanaume kuna wakati mnashangaza sana. Unakuta mtu anasema hawezi kuoa single mama…. Hebu tuambieni kipi bora kuoa single mama ambae Yes alikosea but katunza mimba Kazaa mtoto na sasa ametulia Kajifunza kutokana na makosa AU bora kuoa binti alie bwia ma contraception hadi kizazi kimepinda au katoa mimba mpka kizazi kina makunyanzi utamuoa hata msipate mtoto? Kipi bora???
Wengi humu ni wazazi wa mabinti na wazazi watarajiwa unajuaje binti yako hata zaa kabla ya ndoa? Je vijana wakija kuonyesha interest utawaambia usimuoe binti yangu ni single maza?
Wangapi humu ni zao la single maza? Hivi mnavyo andika humu ndivyo mnavyoangalia mama zenu kua huyu Hana thamani ni single maza?
Na mshawahi kujiuliza anaempa binti mimba akamuacha yeye akaenda kuoa a fresh girl (as you think) is he not as guilty as well ???
Natamani ifike mahala jamii yetu isimnyooshee binti kidole kisa ni single mom bali tujikite pia kwenye kuongea na vijana wetu as they are also “single dads” na kuna mabinti pia hawatataka single dads kwa kuogopa pia baby mama dramas so it goes both ways!!!
Single mamas sio shida kikubwa jiridhishe kwamba ametulia na anajiheshimu hata Kama baba mtoto yupo kwenye picha, kuliko kuoa binti ambae anabwia ma P2 kila mwezi na Maria Stopes Ana Loyalty card!

Disclaimer: Read this with an open mind maana mtahisi ni maoni ya single mom which is quite the opposite [emoji3577]
Swala ni lile lile, hatuoi single mothers au wasimbe,

Lazima tubebeshe ndo uolewe
 
Kuna wengine wana bahati wameolewa aisee na watt...nawajua wawili
 
Kwanza hajakutwa akiwa bikra,akasamehewa halafu tena anakuja baadae anasema pamoja na kunikuta siyo bikra,ila nimezalishwa kabisa.Aisee yataka moyo sana,wanaume tuna wivu sana,wadada mkitaka kuolewa kiroho safi,chungeni sana mienendo yenu kabla ya kuolewa.Ukute hata aliyemzalisha alivyoambiwa kua muoe huyu dada kwasababu umempa ujauzito,akajibu sikumkuta bikra,hivyo atakua na mahusiano na maex wake,ntaoa nitakayemkuta ni bikra,na akampata bikra akamuoa.
Enyi wanawake,ambao mnaolewa kwasasa,ukiolewa jua kabisa anayekuoa hajakutana na bikra,akikutana na bikra,ushindani wako nayeye(huyo bikra),unakua mkubwa.Nawewe single mother,ukiolewa na mwanaume,jua huyo mwanaume,hajakutana na mdada bikra au ambaye siyo bikra ila hana tabia njema ukilinganisha nawewe, ndiyomaana kakuoa wewe.Tambua mdada ambaye ni single mother au asiye bikra ni chaguo la pili baada ya mtu kukosa hitaji lake.
Jitunzeni.
Jokajeusi
 
Back
Top Bottom