PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
Wale wanaosema asiwe na mawasiliano na aliyemzalisha, hii inaweza ikakupeni furaha ya muda mfupi. Sababu kama mtoto anajua baba yupo hai na huna mawasiliano naye huku upo busy na mwanaume wako mwingine (mume wako), hii itampelekea mtoto kujenga chuki kwako na kwa mume wako na watoto wenu na hata akafikiria kuwadhuru.Kivipo sijakuelewa.
Yeye atakua anajiona ni outsider tu, ikifika wenzake wanaenda kutembelea upande wa baba yao, yeye ataachwa pembeni au hata akienda basi kule lazima kuna mambo watamtenga sababu ni mtoto wa watu.
Yeye pia akienda kumtembelea baba yake au upande wa baba yake lazima kuna mambo wenzake watatengwa tu.
Hiyo hali inakua inajenga mpasuko mkubwa sana kwa watoto siku za baadaye, huku nyinyi mkijidanganya mnapendana wakati mfumo wa maisha umekaa.
Mbaya zaidi baba yake awe na uwezo duni kuliko nyie ndiyo chuki itakua zaidi kwa kuhisi kuna dhurma ilifanyika.
Haya mambo siyo mepesi, bora aendelee na maisha yake tu, lakini si kutafuta ndoa bali ije yenyewe na hata ikija atatakiwa kutafakari sana.