Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Kakosa Mume wa ndoto yake: Mdogo wangu wa mwisho kakosa mume kisa ana mtoto

Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Kifupi mwanamke ukishazalishwa, wee jua ushaharibiwa maisha yako ya ndoa
 
Huyo mwanaume ni wa mfano. Yaani nampongeza sana. Anajua anachokitafuta ktk maisha yake na anajua hawezi kipata kwa mwanamke mwenye mtoto. Mwacheni kijana wa watu aende kwa amani. Alilelew vyema na akafuata malezi mazuri, safi kabisa.

Mimi sitaoa kabisa single mother, ni never kabisa. Nolikua na sababu zangu ila jamaa kaniongea sababu zingine kiwa hata kwenye malezi ni ngumu kuwakanya watoto wako.

Good maen with brain. Mwanaume anaejielewa hawezi kuoa single mother. Wewe mwenyewe umesema kabisa kuwa ulimwelekeza mdogo wako jinsi ya kumwambia. Hayo uliyomwambia inawezekana hayana ukweli ni kumpanga tu kijana wa watu.

Huyo kijana ni mtu na nusu. Safi kabisa.
Hii nimeshuhudia kuna brother alioa single mother mwenye mtoto wa kike.. Sasa wamefunga ndoa imebidi wakaishi kwenye nyumba ya huyo mwanamke, sasa balaa miaka imeenda jamaa karelax kajua mapenzi moto moto yataendelea mtoto amekua sasa akaanza vitimbi vya Foolish Age.

Sasa mwanaume akitaka kuwa mkali kama baba wa mtoto kuna muda mwanamke wake anavumilia anashindwa anaingilia mzozo kwa kutetea binti yake. Yaani anaumia tena kuona binti yake akikanywa.

Binti akaanza kuwa na kiburi maana anajua kwa mama yake yupo pekee yake na huyu sio baba mzazi so mama yake hawezi ruhusu amuadhibu wataishia tu kubishana na kumjibu jeuri.

Nilikuwa namuonea huruma sana yule brother namna ambavyo inabidi awe mpole eneo ambalo alitakiwa kuwa mtawala na mwenye sauti ya mwisho ila mwanamke anamnyang'anya ile sauti na mamlaka yake ya kiume na kuyavaa yeye kuwa na final say sababu wanaishi kwenye nyumba yake, na mtoto ni wake pekee.

Aiseee.
 
Usingle mother ni ugonjwa mbaya sana kila mwanaume mwenye akili timamu hawezi kuoa single mother. Kuna binam yang walimuotea wakamzalisha asee na ni pisi kweli ila mpka leo hajapata wa kumuoa na umri unakimbia. Sometimes mpaka anamchukia mwanae anasema ndio kamletea nuksi maishani mwake
Wakati anamwaga uno alikuwa hajui hatima yake au?
 
ukimuoa mwanamke ambae kazalishwa na mwanaume mwengine tena baba wa mtoto yupo hai hata akikwambia anakupenda maneno yake hayawezi kuingia akilini.
Ni heri tuwe wawazi mapema tuwaambie hatutaweza kuwaoa kuliko kuwapotezea muda.

jamaa kafanya maamuzi ya kiume pasipo na mapenzi dawa ni kuwa muwazi ili kuheshimu muda wa mwenzako aende akatafute mwingine atakaeweza kuvulimilia hilo.
Hata mimi nimemkubali sana mwamba ana roho ya kiumeni ile yenyewe. Amejua huyu binti hatutawezana hata iweje. Wacha tu yaishe mapema, atanilaumu ila atakuja elewa maana ubaya haupo kwangu upo kwake.
 
Akunyimae Kunde....

Partnership ni mapatano / makubaliano na partnership nzuri ni symbiotic kila mtu anapata kipenda roho bila sacrifice yoyote sasa unapotaka mtu ku-sacrifice kitu kwa ajili yako kwanza kabisa ni wewe kuwa selfish mbili ni ku-postpone the inevitable siku ukiachwa au mambo kwenda mrama usishangae...

To each his/her own....
 
Huwa nawafikiria single father's kwakweli na mm natak nione makaburi ya wanawake mlozaa nao [emoji3]
Kama wewe ukiingia kimahusiano na mwanaume mwenye mtoto au watoto na mwanamke au wanawake wengine halafu ukawajibika kumhudumia huyu mwanaume kwa mavazi, chakula, na mahitaji yake mengine muhimu ya kiume kama mitokonya kwenda out yeye na watoto wake, au kumtoa pesa anapokwenda kwenye mitoko na washkaji zake.

Lakini pia kuwalipia Ada watoto wake wote bila kujali kuwa si wako. Yaani wewe kama mama wa familia ulipie 100% ya gharama. Then hapo utakuwa na haki ya kuulizia makaburi ya hawa wanawake.

Nje ya hapo utakuwa tu unaiga kauli za wanaume wanapohoji.
 
Upo sahihi kabisa. Hili tatizo si la upnde mmoja tu. Hivi vijogoo vinavyozalisha ovyo ovyo hivi tabu sana. Unamkuta binti ana 20 yrs ila tayari ni single mother. Aisee inaumiza sana.

Na wanawake anzeni kukataa kuolewa na single fathers.

Mm ni Me
Hakunaga single father hii dunia. Sijui umkute wapi labda awe padre.
 
Kama wewe ukiingia kimahusiano na mwanaume mwenye mtoto au watoto na mwanamke au wanawake wengine halafu ukawajibika kumhudumia huyu mwanaume kwa mavazi, chakula, na mahitaji yake mengine muhimu ya kiume kama mitokonya kwenda out yeye na watoto wake, au kumtoa pesa anapokwenda kwenye mitoko na washkaji zake.

Lakini pia kuwalipia Ada watoto wake wote bila kujali kuwa si wako. Yaani wewe kama mama wa familia ulipie 100% ya gharama. Then hapo utakuwa na haki ya kuulizia makaburi ya hawa wanawake.

Nje ya hapo utakuwa tu unaiga kauli za wanaume wanapohoji.
Umeanza unatak tuanze kubishana😂
Aya sawa wahoji tu
 
Uwezi amini jamani, nina mdogo wa mwisho anamika 27 miaka mitano iliyopita alipata mtoto wa kiume. Ila aliyempa ujauzito baadae alioa mwanamke mwingine.

Mwaka jana mwezi wa 8 alimpata kaka mmoja hivi ni mzuri sana na anamaisha yake. Mimi nilimpenda sana yule kaka, mdogo wangu aliniambie huyu ndo mume anayemtaka japo hakumwambia mapema kuwa anamtoto tayari.

Ila mwezi uliopita yule kaka alimwambia kuwa anahitaji kumjua zaidi kuusu familia yake na mahusiano yake ya mwanzo kabla hawajafika deep relationship.

Mdogo wangu akasema sawa, mimi nilimwambia kuwa mwambie mapema kuwa unamtoto tayari, pia usimfiche kuhusu uliyezaa nae mwambie tuu mahusiano yashakufa na tayari yeye anamke tayari. Mwembie mtoto wako hataaribu mahusiano yenu. Pia amwambie tuu kuwa haukupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu.

Sasa wiki iliyopita alimwambie kuwa yeye tayari anamtoto, na aliyezaa nae yani Baba mtoto hana mahusiano nae wamebaki kuhudumia tuu mtoto na kuwasiliana kuhusu mtoto tu.

Baada ya kumwambia hivyo yule kaka jamani, jioni yake hakuwa anajibu hata sms , hata akimpigia anamwambia yuko busy. Alimfanyi hivyo kama siku 4 hivi.

Sasa juzi wamekutana yule kaka jamani akamwambia kuwa wewe tayari unamtoto nje. Mimi nataka kuwa na mwanamke ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu wa ndoa peke yake.

Nilishangaa sana alimwambie kuwa kama unamtoto tayari tutawafundisha nini watoto wetu kuwa usizae kabla ya ndoa angali wewe tayari unamtoto kabla ya ndoa.

Huo ujasiri utautoa wapi. Lakini pia hata kuwaambia watoto usizini angalie wewe mama ushazini tayari.
Mawasiliano na baba mtoto yakizidi je mimi nitafanya nini. Mdogo wangu ameniambie hivyo.

Nimeshangaa sana jamani,

Hivi nyie wanaume mtoto anatatizo gani jamani. Kwani atazuia ndoa yenu isiwe na furaha jamani.

Kwa nini inakuwa ngumu kwenu kuoa mwanamke ambaye anamtoto tayari.

ACHENI UCHOYO NA ROHO MBAYA.
Sio lazima mtoto kuharibu mahusiano yao,ila inawezekana kwa asilimia 80 huyo mtoto akaja kuharibu hayo mahusiano mpka ukajuta,itafika mahali anaanzisha mahusiano na baba watoto kwa kigezo cha huduma ya mtoto,kwahiyo chanzo kitakuwa ni huyohuyo mdogo wako,hapo ndio utashuhudia rangi zote usizozijua,acha tu huyo jamaa achukuwe maamuzi magumu majuto yake huwa ni mabaya sana...
 
Safi sana mana siku hzi kupata demu ambae kavuka miaka 25 hana mtoto imekua shuhuli...

Tulee watoto wetu kwny hofu ya Mungu wakuu wasije ishia kuwa masingo maza.. unakubali vipi kumwagiwa ndan na mtu sio mumeo afu siku za hatari...
Ukiuliza kutoka miaka 18 hadi hiyo 25 alikuwa anafanya nini cha maana kwenye mahusiano ni umalaya tu hakuna la maana.
 
Sijui nipo off topic , hivi kwanini watoto tuseme wanne waliozaliwa na baba tofauti ila mama ni mmoja ,Huwa hakuna ile family bond , yaani ule upendo baina ya ndugu na ndugu?[emoji848]
Damu ni nzito kuliko maji
 
Kwanza hajakutwa akiwa bikra,akasamehewa halafu tena anakuja baadae anasema pamoja na kunikuta siyo bikra,ila nimezalishwa kabisa.Aisee yataka moyo sana,wanaume tuna wivu sana,wadada mkitaka kuolewa kiroho safi,chungeni sana mienendo yenu kabla ya kuolewa.Ukute hata aliyemzalisha alivyoambiwa kua muoe huyu dada kwasababu umempa ujauzito,akajibu sikumkuta bikra,hivyo atakua na mahusiano na maex wake,ntaoa nitakayemkuta ni bikra,na akampata bikra akamuoa.
Enyi wanawake,ambao mnaolewa kwasasa,ukiolewa jua kabisa anayekuoa hajakutana na bikra,akikutana na bikra,ushindani wako nayeye(huyo bikra),unakua mkubwa.Nawewe single mother,ukiolewa na mwanaume,jua huyo mwanaume,hajakutana na mdada bikra au ambaye siyo bikra ila hana tabia njema ukilinganisha nawewe, ndiyomaana kakuoa wewe.Tambua mdada ambaye ni single mother au asiye bikra ni chaguo la pili baada ya mtu kukosa hitaji lake.
Jitunzeni.
Umekosea mtiririko. Kwanza umemkuta sio bikra, ukasamehe, then ukagundua alikuwa na mahusiano yaani kuna mtu alikuwa anamla, ukasamehe, then ukaja kugundua sio mtu m'moja ni watu zaidi ya 10 wameshachovya dudu zao kwake, ukasamehe, then unakuja kujua kuwa alishika mimba mara kadhaa na akatoa, ukasamehe, then akashika mimba na kuzaa,then ukaanza kujihoji huyu mwanamke ni mtu au jini, kabla haujapata jibu unagundua ana mawasiliano na baba mtoto wake na hao waliomla awali.

Enyi wadada, upo radhi kaka yako, mdogo wako wa kiume au mtoto wako wa kiume siku zijazo apitie situation kama hii ili umwite ni mwanaume wa ukweli?! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wanawake kweli mpo illogical mara nyingi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Single father sisi ndio tulikataa kuoa hao tuliozaa nao wakati kwa single mothers ni kinyume chake.
So, mara nyingi kama nimekataa kukuoa basi kuna kitu niliona hakiko sawa kwako. Halafu hatuna ile piga piga simu kuomba child support, hapa kwenye child support ndipo single mothers wanakokamatika.
Mimi ninaweza kumaliza hata miezi 4 sijawasiliana na mzazi mwenzangu. Kwanza hapa mwaka wa 4 hata kumwona sijawahi kumwona.
Ila sasa yeye from no where usku saa nne mara sms nimewamiss wewe na mwanangu. Nasikia umenenepa natamani nikuone na sms za ajabu ambazo mara nyingi sizijibu na hapo tayari yuko kwa mahusiano mengine.
Single mothers mna changamoto fulani fulani kwa kweli.
Sema hii kampeni ya kuwakandia single mothers itafanya madada wengi wawe wachoropoa mimba wazuri hivyo watakuwa mama wa marehemu
Hii ya kuchoropoa mimba ni mbaya sana aisee. Kuna watoto huwa wanarudi upya. Ulimtoa roho anarejea kama mtoto mwingine akija anakutesa watu wa nje wanashangaa mbona mtoto hana upendo na mama yake kumbe nafsi iliyouliwa imerejea tena Duniani imekuja kulipiza kisasi.
 
Mimi nimezalisha wanawake 3 tofauti ila kwa bahati mbaya hakuna ata mmoja tuliyepanga kuzaa wote wanakwambia bahati mbaya nimepata mimba..

Bahati mbaya zaidi wote wameolewa sasa na wanaume tofauti ila wototo nalea mahitaji bila kelele.

Huwa najuta some tyme ila napotezea ndio yameshatokea yaani hadi hamu ya kuwa na ndoa imeisha.
Ilibidi ulivyomzalisha huyo wa kwanza ungemuoa kabisa
 
Back
Top Bottom