Kalamu inavyoweza kumtuliza mume asiyetulia katika ndoa yake

Kalamu inavyoweza kumtuliza mume asiyetulia katika ndoa yake

Abtali mwerevu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
665
Reaction score
515
Wanawake wanapigana vita vingi. Kutafuta mume ni vita, ukimpata mume bado shida zinabaki palepale, mume hatulii, akipata visenti vyote anamaliza nje na wanawake wa kila aina. Pesa zinapotea, afya ya mume inazorota na hatari ya kupata maradhi inaongezeka.

Basi mwanamke usiwe na wasiwasi, leo nakupa dawa ya kumtuliza huyu bwana ambaye hakubali kupitwa na lolote. Ukifanikiwa kumtuliza, faida ni kwako wewe na yeye!

Kabla Hujatengeneza Dawa

Kabla hujatengeneza dawa, kwa muda wa siku saba fanya mambo yafuatayo:

Msamehe kwa matendo yake. Tambua kwamba asilimia 90% ya wanaume hutoka nje ya ndoa zao. Tatizo lake yeye kazidisha ndiyo sababu umefahamu.

Usigombane wala kuwasiliana na wanawake anaotembea nao.

Kila anapoongea jambo, msikilize. Kama linawezekana, lifanye. Yapo mambo hayawezekani mwanangu, akiomba nyuma usimpe. Utapata maradhi binti, Kwa mfano, UTI ya nyuma tunapata shida mno kuitibu. Basi we fanya yanayowezekana. Usimkatishe kauli akiongea, wala usionekane kuwa humsikilizi.

Anapokuwa ndani, weka simu yako mbali halafu nenda kakae pembeni yake. Kaa kimya bila kuongea. Fuata yeye atakachosema. Akisema kalete maji kalete, fanya hiki fanya na mengineyo. Unapokaa pembeni yake, acha kabisa kulalamika. Kaa kimya, kuna wakati hata kuanzisha maneno inamchosha, hujui kakutana na nini huko atokako, kaa kimya, subiri yeye aanzishe ndipo uchangie.

Oga, vaa vizuri upendeze.

Kula vyakula sahihi kama: ugali, wali, maharage na mboga za majani. Pia, kula tunda moja tofauti kila siku. Kwa mfano, kama leo umekula ndizi, kesho kula parachichi, inayofuata kula chungwa na mengineyo.

Baada ya Siku Saba Sasa Twende Kwenye Dawa

Nunua kalamu ya wino, hakikisha kalamu hiyo ina mfuniko.

Ingia chumbani wakati mume hayupo, lakini iwe muda ambao anakaribia kurudi.

Chukua meza yoyote, kama huna meza ya mbao, tumia hata ya plastic, hata sturi au kiti.

Hakikisha hakuna usumbufu, funga mlango, ziba madirisha iwe kwamba hakuna anayekuona.

Iweke kalamu yako ikiwa imefunikwa na mfuniko wake juu ya meza. Kama huna meza juu ya kiti au sturi.

Tunachukulia mfano labda mumeo anaitwa YAHAYA RUKANJIA, kama haitwi hivyo, basi utatumia jina lake halisi.

Kaa kwenye kiti, kama huna simama. Ikamate kalamu, zungumza maneno haya huku unafungua mfuniko taratibu, wakati unamaliza kuongea maneno haya, na mfuniko uwe umetoka.

Tamka hivi ukifungua mfuniko taratibu: YAHAYA RUKANJIA, MWISHO WAKO LEO. NGUVU YA KALAMU INAKUTULIZA, KALAMU INA NGUVU KUBWA NA HUTAWEZA KUSHINDANA NAYO. TULIA MUME WANGU, TULIA NA MIMI PEKE YANGU. NIONE MIMI TU. NJE ISHIA KUTAFUTA RIDHIKI. TULIA… TULIA YAHAYA RUKANJIA.

Ni vyema maneno hayo yakatamkwa kama yalivyo. Hivyo, unatakiwa uyanukuu sehemu na uyasome wakati unatamka au kama utaweza kuyakariri ni sahihi.

Baada ya kumaliza, na kalamu imeshatenganishwa na mfuniko, iweke juu ya meza ikiwa imetenganishwa na mfuniko.

Msubiri mume arejee. Afanye kazi zake na atakapoingia chumbani, wewe umevalia mavazi mafupi ya kuvutia, tena ukiwa mpole, mwambie kwa upendo, “Mume wangu, nisaidie kufunika hiyo kalamu isije ikamwaga wino hapo.”

Akiifunika kalamu hiyo… KWISHA HABARI YAKE.

Kwa msaada zaidi, Wasiliana Nami Hapa.
 
Naomba nyuma lishangazi kungwi,, kama hutojali lakini
 
Kwa sisi wa kristo dawa Ni kumkubali na kumkili YESU KRISTO WA NAZARETH kua bwana na MWOKOZI WA MAISHA YAKO
 
😁 kwahuyu wangu mpeni njia nyingine maana siku ananipa maagizo kuwa ni funge kalamu ndio siku ntazimia maana sijawahi ona kalamu humu ndani.
 
Huo ni ULOGI wa kiwango cha lami.

Tunatakiwa tumtegemee Mungu kwa maana yeye aliye juu ana wivu nasi kama tusipo muangalia yeye tu.
 
Akiifunika tu anakuomba tako.!!.
Ndio utakapojua kuwa huo ujinga hau apply hata kidogo kwenye character ya mtu😂
 
Back
Top Bottom